Nape aongea na vyombo vya habari, alalamikia masuala kadhaa!

Status
Not open for further replies.

firehim

Member
Oct 10, 2011
94
27Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye leo amezungumza na waandishi wa habari na kutoa tamko zito kuhusu wanaopiga sarakasi ili kujaribu kupotosha maamuzi ya CCM ya kujivua gamba. Ifuatayo ni taarifa yake aliyoisoma mbele ya waandishi, mjini Dar es Salaam.

Kumekuwepo na juhudi za muda mrefu sasa kutaka kupotosha au hata kushawishi kubadili kabisa maamuzi ya Chama juu ya dhana nzima ya kufanya mageuzi ndani ya Chama (KUJIVUA GAMBA).

Juhudi hizi zimekuwa zikifanywa na kikundi kidogo sana cha watu wachache ambao kwa namna moja ama nyingine wameathiri wanamageuzi haya tunayoyafanya.

Tatizo kakikundi kenyewe kana nguvu kiasi ya pesa jambo linalofanya kelele zao ziwe kubwa lakini zisizo na mashiko.

Juhudi hizi za kujaribu kuhujumu mageuzi haya ndani ya chama zimekuwepo kwa muda mrefu sasa na tumejitahidi sana kuzipuuza, lakini nadhani umefika wakati wana CCM na Watanzania kujua ukweli walau kwa kiasi ya kinachoendelea.

Wanaofanya juhudi hizi wanadhani hatuzifahamu kwa sababu tu tumekaa kimya wakati wakicheza sarakasi zao za kujaribu kuupotosha umma.

Chama tunafahamu na kufuatilia kwa makini kila kinachoendelea hakuna tusichokijua juu ya juhudi hizi na zingine nyingi zikiwemo jitihada za kutaka kumhujumu hata Mwenyekiti mwenyewe. Nasisitiza tunazifahamu.

Juhudi za hivi karibu ni zilikuwa za kutaka Chama kishindwe Igunga ili kujaribu kuhalalisha hoja ya kwamba mageuzi tuyafanyayo hayana tija kwa Chama. Juhudi hizi zilifanyika bila kificho, tunajua hazikuwa na nia njem akwa Chama ila zilisukumwa na uroho na ubinafsi zikiwa na ujasiri mkubwa wa kifisadi, bila kujali masilahi mapana ya Chama kama taasisi na nchi yetu kwa ujumla.

Baada ya kushindwa kwa juhudi hizo Igunga, sasa wanaanza kujaribu kutumia watu mbalimbali kuimba wimbo wao wa zamani kuwa tunapotosha dhana ya kujivua gamba bila kusema usahihi ni upi kama tunachokifanya ni kupotosha. Ikumbukwe huu sio wimbo mpya uliimbwa sana mara tu baada ya kutangaza maamuzi ya NEC.

Bahati nzuri vimeshakaa vikao vya Kamati Kuu karibu mara mbili, ambavyo vyote vimepongeza utekelezaji wa haya mageuzi ndani ya chama. Mapema mwaka huu Baraza Kuu la UVCCM Taifa chini ya Uenyekiti wa Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari walipongeza utekelezaji wa maazimio ya NEC.

Sasa pengine tujiulize kama wana CCM na Watanzania kwa ujumla hawa wanaodai tunapotosha maamuzi ya NEC ni kina nani na kwa masilahi ya nani?

Naendelea kusisitiza hakuna kilichopotoshwa. Ushindi wa Igunga kwenye uchaguzi mdogo, pamoja na ule wa chaguzi ndogo za Udiwani kwenye kata kumi na saba kati ya ishirini na mbili zilizofanya uchaguzi ni uthibitisho wa kukubalika kwa mageuzi tuyafanyao. Nachukua nafasi hii kuwashukuru sana wa na CCM nawananchikwaujumlakuungamkonomageuzituyafanyayokw aniMwalimualishatuasa “BILA CCM MADHUBUTI NCHI YETU ITAYUMBA”

Walikwenda na kaulimbiu Igunga “TUSHINDWE ILI TUHESHIMIANE” wakasahau kuwa Chama ni taasisi si mtu, ushindi ule Igunga na kwenye kata mbalimbali ni Ushindi wa wana CCM na wapenda nchi hii wote! …Hivyo basi “TUMESHINDA ILI TUHESHIMIANE” Bahati mbaya kwao hawa kutegemea kutokea yaliyotokea. Nawasihi wasiweweseke watulie na kutafakari upya wayafanyayo huku wakikumbuka…HAKUNA TUSICHOKUJUA.

Nichukue nafasi hii kuwaomba wana CCM nchi nzima kutulia na kuzipuuza juhudi hizi kwani tukifanyacho ni kwa masilahi mapana ya Chama chetu na nchi yetu, hakuna sababu ya kutiwa hofu, kila kitu kiko salama. SABABU YA KUSHINDA TUNAYO, NIA YA KUSHINDA TUNAYO NA UWEZO WA KUSHINDA TUNAO.

Malengo mengine makubwa waliyo kuwa nayo kupitia kushindwa kwa CCM Igunga kama kungetokea ili kuwa kuipa nguvu kampeni yao kubwa na ya muda mrefu ya kujaribu kujenga hoja ya kutenganisha Uenyekiti waTaifa wa CCM na Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bahati mbaya kwao na wapambe wao mambo yamekwenda kinyume na dua zao. Changa moto ni nayo itoa kwao, kwa nini wasitoke wenyewe kutoa madai wayatoayo hadharani badala yake wanatumia watu? Hii hoja ya kutenganisha kofia kama ina masilahi kwa chama nasi kwa kikundi kidogo kwa nini wanatumia nguvu ya pesa kutaka kushawishi wajumbe? Anayeamini kwa nini asiilete kikaoni bila kushawishi watu kwa pesa?

Mwenendo wa siasa nchini unadhihirisha kuwa upinzani hauna nguvu kiasi hicho ila unapata nguvu ndogo waliyo nayo kutoka kwa kikundi hiki kidogo sana cha Wanaojiita wana CCM lakini kwa kweli ni waasi. Wengi wao walianza kwa kuasi Imani ya CCM na sasa wana endesha kampeni ya watu kuasi maamuzi halali ya vikao halali vya Chama chetu. Naomba niwakumbushe TULIAMUA, TUKAAHIDI NA TUTATEKELEZA HAKUNA KINACHOBADILIKA KWA SARAKASI ZA BARABARANI, WANAPOTEZA MUDA.

Yaliyobaki yanayofanywa na wapambe na wanaotaka kutumiwa ya kimaadili tutayashughulikia kwenye vikao. Chama cha siasa makini ni vikao.
 
Last edited by a moderator:

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,467
1,164
Tatizo kakikundi kenyewe kana nguvu kiasi ya pesa jambo linalofanya kelele zao ziwe kubwa lakini zisizo na mashiko.

I can't believe Nape anaweza kusema haya, lakini uthibitisho wa nguvu ya kundi hilo analolisema:

1. Walimkataza asiende Igunga na hakwenda zaidi ya kujipenyeza kwa kificho eti ameenda kuhani msiba. Tulimwahidi mpaka $100 ya bureeee lakini hakukanyaga.

2. Uthibitisho namba mbili hawezi hata kuwataja hadharani zaidi ya kulalama, sasa kama yeye kama ana nguvu zaidi ya hao anaowasema kwa nini anauma uma meno??????

3. Huyu jamaa anaonekana ni mlevi, yaani mara waingizie nguvu ya upinzani imetokana na udini na sasa ghafla eti ni kutokana na kakikundi hako anakotaka watanzania wakadharau lakini on his choosing anakapa credit eti ndiyo kanaupa upinzani nguvu. Siasa za wapi hizi????

Mwisho nilitabiri, na the good thing nilimwambia Nape in face kwamba baada ya uchaguzi huu wa Igunga tutawaona mtakavyoanza kuparurana and this is exactly what is happening.
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,711
7,151
Huyu ni CCM A alafu inapingana na CCM B,alafu kuna CDM..naona hapa sasa kuna vyama vitatu vinavyopingana Tanzania...tunasubili magamba yavuliwe ama la lakini Nape hana chake tena,alipigwa ban Igunga sasa amebaki kuongelea Lumumba kama Tambwe.

Nepi,chupi inakuvuka,umekwisha,tunasubili umwambie Lowassa vua gamba
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Nooooooooo Way is Nape again wakuu .Huyu wa nini hapa jamvini ? Bora Malisa japokuwa aliongea akiwa viwanja huru vya Arusha akaogopa kubwabwaja kama kawaida yao .
 

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,467
1,164
Leo hajaitaja CHADEMA? Ajabu

Mwenendo wa siasa nchini unadhihirisha kuwa upinzani hauna nguvu kiasi hicho ila unapata nguvu ndogo waliyo nayo kutoka kwa kikundi hiki kidogo sana cha Wanaojiita wana CCM lakini kwa kweli ni waasi. Wengi wao walianza kwa kuasi Imani ya CCM na sasa wana endesha kampeni ya watu kuasi maamuzi halali ya vikao halali vya Chama chetu.

Ameitaja mkuu, ila hapo amedhihirisha dharau kwa watanzania maana walipotaja sababu za kupungua kura za JK mwaka jana kutoka 80% mpaka 60% hawakukataja kabisa haka the so called kakikundi. Huyu mkuu anakimbia kivuli chake na ndiyo maana kidume chao RA aliwaambia waache siasa uchwara.
 

KELVIN GASPER

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,066
453
Nape kaitisha mkutano na waandishi na kutoa tamko zito kwa wale wanaopinga dhana nzima ya chama hicho ya kujisafisha (kujivua gamba).

Anadai kuwa kuna kikundi cha watu wachache wameathiri mageuzi yanayoendelea ndani ya chama.

Anadai kuwa kikundi hicho ni kidogo ila kilatumia nguvu ya pesa inayopelekea kelele zao kuwa kubwa na kusikilizwa.

Anadai kuwa zipo juhudi zinafanywa na kikundi hiki kumuhujumu mwenyekiti mwenyewe.

Anaendelea kueleza kuwa kikundi kilikwenda igunga na kauli mbiu TUSHINDWE ILI TUHESHIMIANE , Nape anadai kuwa wamekuja na hoja ya kutaka kutenganisha kofia mbili.

Anaongeza kuwa upinzani hauna nguvu kama inavyodhaniwa ila unapata nguvu kutoka kwa kukindi hiki.

Kwa wale mliosikiliza taarifa ya habari saa kumi jioni TBC, Nape ametangaza kuwa, CCM wanapinga kwa nguvu zote malipo kwa kampuni hewa DOWANS.
 

sidimettb

Member
May 17, 2011
42
14
A shrub can never be a tree no matter what; huyu jamaa hawezi kukomaa kiakili, ni uwezo wake ndivyo ulivyo hata kama ikipita miaka mingapi na akapewa nafasi gani!

Kwa nafasi aliyo nayo ndani ya chama alitakiwa kuwa na busara ya kuepuka(Japo kwa maneno) chochote kinachoweza kukigawa zaidi chama. Kauli zake zinaonyesha kuwa anawakilisha kikundi flani kilichomweka pale kwa maslahi binafsi.Ila kwa upande mwingine, kuwepo kwake ndani ya magamba ni blessing in disguise kwa ustawi mzuri wa Taifa letu maana anasaidia kuisambaratisha hili janga la kitaifa-Magamba
 

msaragambo

Senior Member
Aug 6, 2008
127
17
Sasa Kama mnawajua na nikakikundi kadogo si muwafukuze Mnasubiri nini sasa………..Kazi kulalama tuu
 

Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,774
3,226
Yaani anaona wameshinda Igunga wakati chama chake kimeuwa watu ,kufuta majina 6000 na kuingiza ya kwao Nape tafadhali bwana tuachieni nchi yetu vyema,halafu akisema hawaaogopi hao walioasi ndani ya CCM mbona hawatajwi
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,641
116,804
Hii ni vita kati ya Nape Nauye na Beno Melisa. Pambaneni wenyewe kwa wenyewe mambo yakae hadharani na meli ya CCM izame kwa amani. Naona sasa ofisini hapakaliki kila kukicha kila upande unataka kuzindua matawi ili kujiimarisha vizuri kwa wanachama wao.

Mengi yataibuka na hiki ni kipindi cha MATAMKO NA TANZANIA TUNAYOITAKA.
 

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
19,608
24,182
Brother Nape,naomba unitajie majina ya hao watu wanaopingana na vikao vikuu vya chama.au una waogopa?ccm kwisha habari yake.mia
 

MPG

JF-Expert Member
May 12, 2011
483
53
Limbukeni mkubwa huyu NAPE yeye kazi yake na kuongea na vyombo vya habari
 

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
538
Ninamsikitikia sana Nape, kwani hajui anachokifanya wala hajui hatma yake hapo baadaye ndani ya CCM. Ni kauli ya woga na kukata tamaa tu. Ilikuwa busara kama Nape angefanya haya;

1. Angewataja kwa majina na uhusika wao watu hao.

2. Kwanini asijenge hoja ndani ya CCM watu hao wafukuzwe?

3. Kwanini asiwaumbue watu hao hadharani au kwenye vikao?
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom