Nape ang’aka uvujaji siri vikao vya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape ang’aka uvujaji siri vikao vya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Sep 22, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha Mpinduzi (CCM) kinahaha kuzuia uvujaji wa siri za vikao vya juu vinavyoendelea mjini hapa kwa kuwaelekeza walinzi wake kuwazuia waandishi kuingia ndani ya viwanja vya Jengo la White House, wanaoripoti habari ambazo hazijathibitishwa na viongozi wake.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

  “Tumetoa wito kama chama tangu jana (juzi) kwa vyombo vya habari na wale wote wanaotafuta habari za chama, hatutamvumilia yoyote ambaye anapublish (anachapicha habari ), atafute habari katika vyanzo sahihi ,”alisema.

  Alisema chama chake hakitamvumilia yeyote anayechapisha habari alizoziita za barabarani na kuonya kuwa anayetaka kufanya hivyo akae huko huko aliko na kuzitafuta.

  “Na tumewaelekeza walinzi wetu kama kuna chombo kilichoandika habari za barabarani basi wasiruhusiwe kuingia ndani humu kwasababu ukweli vikao hivi ni vya muhimu, tusingependa kucreate tension (kutengeza hofu) mtaani ambayo haina sababu,” alisema Nape.

  Alisema mwandishi atakayesikia jambo, yeye yupo na simu yake iko wazi saa 24 na kuwataka kupata uhakika wa jambo kabla ya kuandika, “Ukiandika kwa maslahi ya kumbeba ama kumchafua mtu hilo halitavumilika.”

  Akizungumzia kuhusiana na vikao vinavyoendelea mjini Dodoma, Nape, alisema kwa muda wa siku tatu wamekuwa na kikao cha sektarieti ya Halmashauri kuu ambapo kazi yake kubwa ni kupokea taarifa ya mapendekezo kutoka wilayani na mikoani na kuziunganisha pamoja na kuziboresha.

  “Kwa ajili ya kuziandaa na kujiandaa kushauri vikao vinavyofuatia, hivi leo mchana (jana), tutakuwa na Kamati ya Maadili ambayo itaongozwa na Mwenyekiti wa Chama, tunategemea kati ya saa 6.00 mchana na saa 7.00 mchana atawasili mjini Dodoma na kesho (leo) tutakuwa na Kikao cha Kamati Kuu ya chama ambayo itakaa kwa siku mbili,” alisema.

  Alisema kitafuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ambacho kitakuwa cha siku mbili.

  Alisema nafasi ambazo ziliombwa na zitajadiliwa na vikao hivyo ni wajumbe wa Halmashauri kuu kupitia wilaya na wale wa Zanzibar na Tanzania Bara, nafasi ya uenyekiti , katibu uenezi na uchumi za mkoa na wagombea kutoka jumuiya mbalimbali za chama hicho.
   
 2. b

  bagwell Senior Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hyo ndio kauli ya Mmiliki wa Chama Cha Mabwepande....
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Well. he has a right to speak as he did given his position. But he should know that enemies are within. Leaks are coming from those who take part in meetings, and that does not take a reporter to be in the meeting to get leaks published. He should remember that we are leaving in a different era. One click is more than enough to do the job.
   
 4. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sometimes nashindwa kuelewa majukumu ya katibu mkuu wa chama na katibu muenezi...
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  nape bwana....sasa walinzi wanini wakati wanakaa milangoni na taarifa zinavujishwa na wajumbe wa vikao wenyewe
   
 6. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nilimiss nepi siku za karibuni alitoweka kwenye vyombo vya habari!! now he back, gamba @ work
   
 7. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Na bado atang'aka sana mwaka huu....
   
 8. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Watu wamechoka kuandika propaganda, ndiyo maana wanafanya jitihada kutafuta habari za uhakika toka jungu kuu.
   
 9. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  chama kimetoboka toboka hata taarifa zinavuja kwanza ccm hawana uhalali wa kuwa na jambo la siri, hv ukikuta genge la majambazi wamekaa mahali wanapanga kufanya uhalifu utakaa kimya?
   
 10. Root

  Root JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,119
  Likes Received: 12,828
  Trophy Points: 280
  mambo hayoooooooo
   
 11. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hahahahahaha
  Eti hataki ktengeneza tension/hamaki kwa wananchi kwa habari zisizokuwa na uhakika.

  Huyu jamaa bana mpuuzi kweli. Yani kuna kitu gani kutoka kwa ccm kinachoweza kutengeneza tension? Labda tension ndani yao wenyewe.
   
 12. the blower

  the blower Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi napita tu- kwetu hakuna kijani kiangazi kimeshika kasi
   
 13. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Well said Bongolander. We are living in a totally new era. I don't think Nape will manage all those holes I see in his party leaks are coming out of. No reporter is going to get scared I don't reckon. All reporters will do is to tell the public any leak is a believable unconfirmed story...which then gives Nape the freedom to deny it if so he chooses, and the reporter is safe! To reporter I have this one call: let's get those leaks out !   
Loading...