Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Namshauri Nape kwa vile imeonekana vipindi vya television na redio mchana vinazuia watu kufanya kazi, basi aandae mswada ili upelekwe Bungeni haraka kuomba iwekwe sheria kuzuia vipindi vyote vya redio na television wakati wa mchana. Vyombo vyote vya habari vitangaze kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 12 asubuhi. Isiwe vipindi vya Bunge pekee yake bali pamoja na vipindi vingine vyote. Kama watu wapo kazini, hivyo vipindi vingine wanamtangazia nani? Tukifanya hivyo, naona Dunia itaielewa Tanzania kuwa sasa nchi hii imepata Waziri makini kuliko mawaziri wa habari wa mataifa yote waliowahi kupita, waliopo na watakaokuja. Na Waziri huyo si mwingine bali ni Mheshimiwa sana Nape.
Nape tangu alipooanza mpango wake wa kuwafuta haki ya Watanzania haki ya kuangalia vikao vya Bunge kadiri vinavyoendeshwa ametoa sababu nyingi ya kufanya hivyo. Sababu ya kwanza alisema kuwa ni kutokana na TBC kutokuwa na pesa ya kutosha kurusha matangazo ya moja kwa moja.
TBC ikaacha kurusha matangazo ya moja kwa moja. Vituo vingine vikaendelea kutimiza wajibu wa kuihabarisha jamii kuhusiana na mijadala ya Bunge kadiri ilivyokuwa ikiendeshwa. Hivyo usitishaji wa TBC kuwaletea mijadala ya wabunge kadiri inavyoendelea hakukuwa na athari yoyote kubwa. Hata hivyo wadau wengine wakawa tayari kulipia matangazo ya TBC, Nape akawa bubu. Watu walitegemea kuwa Nape angeshukuru kwa huo msaada lakini haikuwa hivyo.
Ilipoonekana dhamira ovu iliyokuwa imekusudiwa kwa kisingizio cha gharama haikufanikiwa, ndipo sasa ikabuniwa mbinu ya kueleza kuwa vyombo vya habari ni vingi mno, na hivyo havitaruhusiwa kuingia na kamera zao badala yake Bunge litakuwa na studio yake. Ikadhihirika kuwa suala la gharama ilikuwa ni kisingizio. Japo mimi siyo mtaalam lakini ni dhahiri kuanzisha studio inayojitegemea ya Bunge ni gharama zaidi maana vitahitajika vifaa na wafanyakazi wa studio hiyo.
Sasa inaelezwa kuwa sababu nyingine ni kuwafanya watanzania wafanye kazi mchana badala ya kukaa kuangalia vipindi vya Bunge maana huu ni wakati wa kazi tu. Hapa inaonekana kuwa kuna dhamira chafu na ovu ambayo inatafutiwa sababu halali kwa kuyataja mambo mazuri. Kwa kiongozi, dhamira ovu au chafu ni uhalifu dhidi ya nafsi na utu wa unaowaongoza.