Nape anapotoa Maagizo kwa Waziri Magufuli...

Nape amekuwa mwepesi Sana kutoa matakamko nilitarajia issue ya Mbuge wa Bahi aliyekamatwa kwa Rushwa angeshalitolea kauli!Mbona hili amepatwa na kigugumizi?
 
Sasa hivi nimeshagundua kuna ombwe kubwa sana la kiuongozi na utawala wa heshima ,kuna kauli ambazo zimetamkwa na viongozi mbalimbali wa serikali na Chama cha CCM ambacho kwa kiasi kikubwa kitasusha tija ya utendaji na uwajibikaji kwa sababu tuu viongozi wanataka waonekane wamekemea ,wana misuli ya kusema na kudhalirisha
kwa mfano Mkuu wa mkoa wa Tabora anaenda shuleni na kukuta waalimu haingii darasani anasema nitakufuza kazi ,nitakutia ndani unajiuliza afisa elimu yuko wapi hapo mmh

Mkuu wa mkoa aliyeteuliwa mpya anakuja anasalamu katika mkoa mpya aliochaguliwa nitavunja baraza la madiwani kama hamtawawajibisha watendaji na mkurugenzi ,je mtu huyu mgeni kwenye mkoa huo atapata ushirikiano kweli MMh

Mkuu wa wilaya mpya amechaguliwa juzi anasema wenyeviti wa vijiji na baraza la halmashauri nitawanq'oa sihitaji wezi mmh mmh
Madiwani wanatoka na mpya baada ya semina ya Aggrey Mwanri wanamfukuza mkurugenzi na watendaji kwenye TV na vyombo vya habari na matusi kede kede mmh mmh

Anakuja waziri mpya kwenye wizara ndio anaingia siku ya kwanza anasema mutang'oka nyie kabla yangu unajiuliza kasoma mazingira saa ngapi huyu siatafichwa mambo mengi ,si ni serikali yake zembe ndio imefikisha hali hiyo iwe hivyo

Anakuja Lukuvi natangaza mawaziri ,watendaji wa wizara jamani nunueni RAV 4 kama mtu fulani jamani hayo VX 8 ni gharama unajiuliza kwa nini waraka usipitishwe kusitisha kununua mashangingingi mmh mmh

Anakuja waziri mkuu anasema halmashauri za wilaya fukuzeni wakurugenzi na watendaji wote tumechoka unajiuliza mbona fedha nyingi za kutoka halmashauri zinarudi kwenye mawizara kwa maofisa na mawaziri kujineemesha kwa nini kusiwekwe njia sahihi ya kuhakikisha fedha inatengewa kazi fulani inafanyia hiyo kazi mmh mmh

Anakuja Raisi anasema sitamwachia mtu yeyete awe waziri,mkuu wa mkoa,katibu mkuu, mkuu wa wilaya mkurugenzi afanye ubadhirifu wa mali ya umma siwezi kabisa siwezi,I might wear a smile but....... unajiuliza hao wengine aliwachagua nani mmh mmh

Anakuja mkama anasema CCM imeshaparanganyika kuna ugomvi kama majeshi ya Nato na G-8 unajiuliza kama katibu mkuu anakiri chama kimekwisha kwa nini uchaguzi mpya usiitishwe mmh mmh

Anakuja Nape anaagiza watendaji wa serikali katika TV unajiuliza hivi mipango ya wizara siku hizi iko makao makuu ya CCM huku ni kuidharirisha taasisi ya serikali mmh mmh

Anakuja January Makamba anasema wapinzani hawawezi kukabidhiwa nchi ni wapasha misuli unajiuliza hivi CCM na wanachama wake wanadhani watanzania watakubali kudhulimiwa kura zake wakielezwa kwamba toka mwaka 1995 mumekuwa mukishinda bali hamlindi kura wakiamua kuzilinda CCM watasema wasemayo kweli mmh mmh
MY Take
The government is not functioning is just a failed state CCM the ruling party has fallen apart

Ni wakati wetu wananchi kuwanyamazisha waha wapuuzi kwa vitendo
 
Jambo usolijua CCM ndo ilikwenda kwa wananchi kuomba dhamana na ndio itakayoulizwa na wananchi 2015, Nape sasa unaifanya kazi ya chama vizuri ndio maana wapinzani haawachi kulalamika. Tuzidi kusonga mbele.
 
Huyu kijana ameajiriwa na Serikali au na chama,anashindwa kueneza masuala ya chama anaingilia utendaji wa serikali,shame on you!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kiitifaki chama tawala kiko juu zaidi ya serikali...so alichokifanya Nape ni sahihi.

Yaani hata mtoto mdogo ukimuuliza atakwambia si sahihi! Waziri anapokea maagizo kutoka kwa wafuatao:-

1. Rais(including makamu wake)

2. Cabinet

3. Waziri Mkuu

4. Kamati za bunge(mara nyingi huwa ni ushauri)

5. Spika wa bunge.

Kwenye ngazi ya chama Nape ni katibu mwenezi so hawezi kumwagiza waziri kama alivyofanya. Ataweza kufanya hivyo tu pale ambapo chama kimekaa katika vikao vyao na kutoa maagizo ya jumla kwa serikali na si kwa waziri mmoja mmoja, otherwise ipo siku atamwagiza hata Waziri Mkuu na Rais. Kwa kifupi Nape alilewa madaraka na ni mtu wa publicity sana, we mfuatilie records zake utaona!
 
Hii inaitwa verbal diarrhoea.

Ni ugonjwa unaowashambulia sana wanasiasa uchwara.

Dalili zake kuu ni kusema ovyo, kuropoka,kusema bila kufikiri,

Dawa ni kuachana na siasa

Nakubaliana na wewe kabisa,na kwa wengine mfano Wenje(juzi nasikia kaharisha tena dhidi ya NCCR) na Nasari ugonjwa huu umeshakuwa chronic kwao.
 
Kunya anye Kuku,akinya bata.....
Kila siku Viongozi wenu wanamwagiza Rais,Waziri Mkuu na Viongozi wengine wa ngazi za juu wa serikali lkn huwa hamuoni kama protocal inavunjwa,madaktari walimwagiza Rais hapa tena wakampa na siku za kutekeleza waliyomuagiza na wengi wenu humu mliwa'support,leo kuwa Nape imekuwa nongwa hizi ni akili kweli?
 
Kuna ukweli hufichwa hasa kwenye miradi ya barabara ambapo wakandarasi hutupiwa lawama kila mara ujenzi unaposuasua.Serikali yetu ina matatizo kwenye malipo ya makandarasi.Nape anza kuilalamikia Serikali yako kwanza,Nape acha kutafuta umaarufu sisi ni watu wazima tunaelewa kila kitu.
 
Nepi Hajitambui vizuri na bado anaakili ya mfumo wa chama kimoja kuwa Chama kushika hatamu.Maagizo yake yameanza kitambo na ziara zake hivi sasa mikoani ni kutoa maagizo kwa viongozi wa Serikali utafikri hakuna sera na mipango mikakati inayotekelezwa na idara za Serikali.Juzi alikuwa Singida kukagua hosptali ya rufaa na kutoa maagizo kuwa majengo matatu kati ya 37 yanayohitajika yaanze kutumika ,hapo yeye kesha kuwa bingwa wa mipango ya utawala wa hosptali,leo nimesikia ametoa agizo kurudishwa kwa kiwanda cha tumbaku mjini songea kutoka mjini Morogoro.Sasa unajiuliza yeye amewasiliana wakati gani na viongozi wa Serikali na kubaini sababu za kufanyika kwa mambo hayo na kuona hayafai au yabadilishwe.Viongozi wa ccm ni wajumbe wa vikao vya maendeleo na ushauri-DCC na RCC ngzi ya wilaya na Mkoa.Pia Wakuu wa Wilaya na Mikoa ni wajumbe wa Kamati za siasa za ccm je kwa nini wasiwatumie watu hao kutekeleza na kuwasilshs taarifa kwenye vikao vyao.Kwa ujumla NEPI ANATAFUTA UMAARUFU WA KIJINGA NA KUKOSHA WENDAWAZIMU KWAMBA ANA MAMLAKA YA KUTOA AMRI KWA VIONGOZI WA SERIKALI.HAKIKA NI UJINGA NA KAMA ANA MAMLAKA HAYO MAPACHA WATATU MBONA KASHINDWA NA WANAZIDI KUJIIMARISHA.
 
Wakuu anayejua JD-Job Descriptions ya Mwenezi atusaidie hapa maana mimi najua ni msemaje si mtendaji...
 
sasa mpaka waziri wa ujenzi hajui kuna tatizo kuhusu huo ujenzi wa barabara na mpaka aambiwe na katibu wa ccm..ni aibu
 
Yaani hata mtoto mdogo ukimuuliza atakwambia si sahihi! Waziri anapokea maagizo kutoka kwa wafuatao:-

1. Rais(including makamu wake)

2. Cabinet

3. Waziri Mkuu

4. Kamati za bunge(mara nyingi huwa ni ushauri)

5. Spika wa bunge.

Kwenye ngazi ya chama Nape ni katibu mwenezi so hawezi kumwagiza waziri kama alivyofanya. Ataweza kufanya hivyo tu pale ambapo chama kimekaa katika vikao vyao na kutoa maagizo ya jumla kwa serikali na si kwa waziri mmoja
mmoja, otherwise ipo siku atamwagiza hata Waziri Mkuu na Rais. Kwa kifupi Nape alilewa madaraka na ni mtu wa publicity sana, we mfuatilie records zake utaona!


Tatizo watu mnatumia mawazo yenu na wala si uhalisia, wenzenu tupo huku, tunakutana na watu wa chama na serikali tunayaona haya, msipende kubisha sana kwa mambo msiyoyajua. Chama tawala kiko juu zaidi ya Serikali hutaki huo ndo ukweli, na Nape anahaki ya kumuagiza mtendaji wa serikali including PM.
 
Nakubaliana na wewe kabisa,na kwa wengine mfano Wenje(juzi nasikia kaharisha tena dhidi ya NCCR) na Nasari ugonjwa huu umeshakuwa chronic kwao.

Wenje na Nasari wamesema kitu gani mpaka useme Wana ugonjwa sugu wa Nape. Sio kuwa Kama neno hulipendi basi Ndio linakuwa verbal diarrhea.
 
Back
Top Bottom