Nape anaposhangiliwa bungeni baada ya kutambulishwa...!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape anaposhangiliwa bungeni baada ya kutambulishwa...!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eiyer, Aug 1, 2011.

1. Eiyer

Eiyer JF-Expert Member

#1
Aug 1, 2011
Joined: Apr 17, 2011
Messages: 28,237
Likes Received: 3,654
Trophy Points: 280
Kumekuwa na lawama siku hizi kuhusu nidhamu bungeni kuwa bunge letu limekosa nidhamu na uvumilivu na wamekuwa wakiacha shughuli nyeti za bunge na kubakiza ushabiki wa vyama,hali hiyo iliendelea leo asubuhi wakati katibu wa uenezi wa CCM Nape Nnauye alipotambulishwa kama mgeni aliposhangiliwa na wabunge wa CCM mpaka spika aliposema inatosha lakini waliendelea na makelele na spika akarudia kauli hiyo mara 3 bila mafanikio!

2. S

SEAL Team 6 JF-Expert Member

#2
Aug 1, 2011
Joined: Jun 10, 2011
Messages: 655
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Tunaomba utujuze mkutano wa CC /NEC wakujivua gamba na mkakati wa Igunga umefikia wapi?

3. F

Froida JF-Expert Member

#3
Aug 1, 2011
Joined: May 25, 2009
Messages: 7,900
Likes Received: 1,328
Trophy Points: 280
Ndio wanachokifahamu wabunge wa CCM,makofi ,vigelegele,kuzomea,na kutoa shukrani na kumpongeza spika,wenyeviti na raisi wao, makubwa wanachi tunajionea ha ha ha ha ha hawajitambui hao

4. Mkwawa

Mkwawa JF-Expert Member

#4
Aug 1, 2011
Joined: Jun 8, 2011
Messages: 1,290
Likes Received: 193
Trophy Points: 160
Taratibu. CCM wakivunja meza ni ajali. CDM wakipanga na kutengeneza meza baada ya kuvunjwa na CCM wanaambiwa ni watovu wa nidhamu. Waacheni wapigiane makofi kwani ndio kazi wanayoweza. Mengine yote wameshindwa. CCM+kulala+kupiga makofi+kuomba mwongozo+makelele= Ufisadi mkubwa

5. zumbemkuu

zumbemkuu JF Bronze Member

#5
Aug 1, 2011
Joined: Sep 11, 2010
Messages: 8,999
Likes Received: 582
Trophy Points: 280
Lazima ataiweka hiyo kwenye wall yake ya FB

6. Crashwise

Crashwise JF-Expert Member

#6
Aug 1, 2011
Joined: Oct 23, 2007
Messages: 22,172
Likes Received: 862
Trophy Points: 280
Mbona hajawatoa au wanao takiwa kutolewa ni wachdema peke yake....

7. Zak Malang

Zak Malang JF-Expert Member

#7
Aug 1, 2011
Joined: Dec 30, 2008
Messages: 5,410
Likes Received: 18
Trophy Points: 0
Wabunge wa CCM hufikiri kwa kutumia makalio yao.
Kwa mfano akiingia na kutambulishwa Shy-Rose na Jafari wake watapiga makofi.
Paka akikatisha ukumbi watapiga makofi.

Hii ndiyo imekuwa hulka yao miak nenda miaka rudi...

8. M

Mapujds JF-Expert Member

#8
Aug 1, 2011
Joined: May 12, 2011
Messages: 1,291
Likes Received: 3
Trophy Points: 135
Ukiwa mbunge wa ccm unatakiwa uwe unajua kupiga kelele sana na kugonga meza tu.

9. Mkirua

Mkirua JF-Expert Member

#9
Aug 1, 2011
Joined: Sep 9, 2010
Messages: 5,667
Likes Received: 24
Trophy Points: 135
magamba type

10. M

Mwanaweja JF-Expert Member

#10
Aug 1, 2011
Joined: Feb 8, 2011
Messages: 3,576
Likes Received: 10
Trophy Points: 135
hawa wanajambo lao maana ingekuwa CDM, wangetolewa nje lakini kwa kuwa wao ndio binadamu wengine watu hatushangai sana time will tell

11. Mungi

Mungi JF Gold Member

#11
Aug 1, 2011
Joined: Sep 23, 2010
Messages: 16,985
Likes Received: 441
Trophy Points: 180

Hahaaa Mkuu umenikumbusha jamaa anapenda masifa balaa! India alienda kusomea umbea nyambaf yake.

12. Riwa

Riwa JF-Expert Member

#12
Aug 1, 2011
Joined: Oct 11, 2007
Messages: 2,601
Likes Received: 232
Trophy Points: 160
Umenivunja mbavu hapo kwenye nyekundu mkuu...

13. Nebisirwe

Nebisirwe Senior Member

#13
Aug 1, 2011
Joined: Jul 27, 2011
Messages: 169
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Ila Kijana anachapa mzigo! as per CCM requirements

14. Donyongijape

Donyongijape JF-Expert Member

#14
Aug 1, 2011
Joined: May 28, 2010
Messages: 1,451
Likes Received: 180
Trophy Points: 160
we jamaa unatisha kupredict,nimetoka huko FB,tayari keishatupia muda si mrefu! anawashukuru sana wabunge kwa kuonesha upendo na kumshangilia sana! wakati huo naona mimi hakukuwa na comment za marafiki kuona mawazo yao na cpia siwezi kupost link hapa coz natumia simu!

15. TUKUTUKU

TUKUTUKU JF-Expert Member

#15
Aug 1, 2011
Joined: Sep 14, 2010
Messages: 11,852
Likes Received: 43
Trophy Points: 145
Hiyo ndiyo kawaida ya wabunge wa CCM!!

16. Eiyer

Eiyer JF-Expert Member

#16
Aug 1, 2011
Joined: Apr 17, 2011
Messages: 28,237
Likes Received: 3,654
Trophy Points: 280

Nilikua nasubiri kwa hamu sana hili tukio lakini sikuliona!Nikabaki mdomo wazi

17. kadoda11

kadoda11 JF-Expert Member

#17
Aug 1, 2011
Joined: Jan 6, 2011
Messages: 16,217
Likes Received: 8,292
Trophy Points: 280
kuna dhihaka flan huku mtaani kwetu kuwa kati ya wabunge ambao vganja vyao vmeota sugu kwa kubamiza mabench(vti) vya bungeni kwa kushangilia kishabik ni wabunge wa CCM.Kwa hiyo hata hilo la nape pia linaingia humohumo,sitashangaa nitakapo sikia baadhi ya wabunge wa ccm wakipelekwa india kulekebiswa makoo yao kutokana na madhara ya kupiga kelele kwa kushangilia hata hoja za kipuuzi ilmrad tuu zipo kiccm.

18. M

Miruko Senior Member

#18
Aug 1, 2011
Joined: Feb 8, 2008
Messages: 173
Likes Received: 3
Trophy Points: 35
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imemaliza kikao chake cha siku moja usiku wa tarehe 31/07/2011 mjini Dodoma chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeamua yafuatayo; 1. Imefanya uteuzi wa makatibu ishirini na saba (27) kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika wilaya hizo. (majina na wilaya zao yameambatanishwa). Pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu imetengua uteuzi wa Makatibu wa Wilaya watatu (3) katika kuboresha ufanisi wa kazi katika wilaya hizo.(majina na wilaya zao yameambatanishwa). 2. Kamati Kuu imepokea na kuridhia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwakilisha Mkoa wa Tabora, Ndugu Rostam Aziz. Aidha imempongeza kwa uamuzi huo uliozingatia maslahi mapana ya chama chake. 3. Kamati Kuu imepokea pia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Ndugu Rostam Aziz na kuagiza chama kupanga ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga itakayozingatia ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya uteuzi wa mgombea. Aidha Kamati Kuu imeagiza shughuli zote za kampeni kutafanywa na CCM Mkoa, Wilaya na ngazi zote za chama wilayani Igunga. CCM Taifa watashiriki kuongeza nguvu. Chama kinatoa wito kwa wana CCM, wapenzi na wakereketwa wa chama chetu kushiriki kwa pamoja kuhakikisha jimbo linabaki kwa CCM. 4. Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwa kwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine. Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha bei ya mafuta ya taa kama suluhisho. 5. Kamati Kuu inasikitishwa na tatizo la umeme nchini kwani athari zake kwa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja ni kubwa. Hivyo basi imeitaka Serikali kutumia muda iliyopewa wa kurekebisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kuja na mpango wa dharura wa kunusuru hali hii na kisha kulimaliza kabisa tatizo la umeme nchini. 6. Aidha Kamati Kuu imejadili masuala mengine kama; migogoro ya ardhi, tatizo la bei ya pamba, tatizo la uuzaji wa mahindi, migogoro migodini, masuala yanayohusu kero za Muungano na kuagiza Serikali kuyashughulikia kwani yanatatulika. 7. Kamati Kuu imeipongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kazi nzuri ya kutekeleza maamuzi ya NEC na kuitaka iongeze kasi katika utekelezaji huo, ili kuhakikisha mageuzi yaliyokusudiwa yanatekelezwa kwa wakati. Aidha imejadili na kupitisha miundo mipya ya Idara ya Itikadi na Uenezi na Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. 8. Kuhusu suala la maadili ndani ya Chama, Chama kinaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama. Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inatarajiwa kukutana wakati wowote mwezi Septemba, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake. Imetolewa na:-
Nape M. Nnauye (MNEC)
KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI
DODOMA
1/8/2011

19. T

The Priest JF-Expert Member

#19
Aug 1, 2011
Joined: Dec 8, 2010
Messages: 1,026
Likes Received: 23
Trophy Points: 135

keshaweka kule fb,anawashukuru kwa "heshima kubwa " waliyompa leo.

20. Eiyer

Eiyer JF-Expert Member

#20
Aug 1, 2011
Joined: Apr 17, 2011
Messages: 28,237
Likes Received: 3,654
Trophy Points: 280

Hawa jamaa kwa mipango kiboko,tatizo ni utekelezaji ni matatizo matupu!

Loading...