Nape amzodoa kwa aibu Mnyika kuhusu wanawake

Jee tunaitaji wanake kuwa viongozi sababu ya credibility au sababu ya gender equality? I feel sad kuona kwamba vijana wanaingia katika mabishano ya kahawa badala ya kubishana kuhusu substance. Hata kama tukiwa na wanawake 75% as long as wana credentials za kuwa hapo walipo then hakuna tatizo. Lakini mpango wa kuset goal sababu ya gender is total wrong. Matokeo yake hakuna litakalo fanyika......
 
Unategemea substance kutoka kwa "Wanasiasa". Thubutu!!
 
Jee tunaitaji wanake kuwa viongozi sababu ya credibility au sababu ya gender equality? I feel sad kuona kwamba vijana wanaingia katika mabishano ya kahawa badala ya kubishana kuhusu substance. Hata kama tukiwa na wanawake 75% as long as wana credentials za kuwa hapo walipo then hakuna tatizo. Lakini mpango wa kuset goal sababu ya gender is total wrong. Matokeo yake hakuna litakalo fanyika......

Ungekuwa mwanamke ungeona substance. Hivi nyinyi mbona mnajipendelea hivyo? Bunge sasa limejaa asilimia 70 wanaume wasiofanya chochote cha maana. Asilimia 90 ya wabunge wanaume ni mafisadi, hebu nieleze sasa mafisadi wanawake kule bungeni ni wakina nani? Nchi za Scandnavia wameweka hizo goals sasa ona wanawake wanavyofanya kazi vizuri tu sambamba na wanaume kwa maendeleo ya nchi zao. Hebu badilini fikra huko. Ndio ubaguzi huo huo ambao CCM inaufanya dhidi ya wapinzani kwa kusema kuwa kwani hao ni wanini. Na hata kwenye CCM yenyewe vigogo na watoto wao wanawabagua wengine kwa kuhoji ni kwanini wapate uongozi

Asha
 
.........mfumo wa ubunge wa viti maalum haufai kwani unaleta hisia kuwa baadhi ya jinsia nia dhaifu zaidi kuliko ,kabla ya kuongeza uwakilishi wa wanawake ni bora tufanye tadhmini kuona mchango wa wale waliopo bungeni sasa....

kinachonitatiza nadhani tutakuwa tunabaka uwakilishi wa wananchi kwa kupeleka wawakilishi wasio na uwezo bungeni ,waliofunga zipu midomo yao........wengi wa wabunge wa viti maalum waliopo bungeni hasa wa ccm hata hawajuwi wanachokifanya pale ...huo ndio ukweli,wengine hatujuwi kama wapo...........sasa tutaendelea kuongeza idadi yao kisiasa ....lakini tujuwe ubunge ni kazi ngumu.....ndio maana wanapewa maofisi na wanakuwa na wasaidizi,wanatakiwa kusoma miswada,kufanya tafiti,kukutana na wananchi na makundi mbali mbali...lakini wengine wanaenda pale kulala tu.....

kila mwanasiasa mwenye nguvu anapeleka mpenzi au mkewe pale...uchahidi upo kwani kila kipindi cha uhai wa bunge harusi za wabunge zimekuwa nyingi...achilia mbali wanyonge wanaolalamikia kuachwa na wake zao.....

nafikiri heshima ya mbunge mwanamke itakuja tu kama atapewa nafasi apigiwe kura.....ndio maana hata ccm kwenyewe wabunge wote wanawake waliopita majimboni utendaji wa unaridhisha sana!!!!...tena kuwashinda hata wanaume!
 
- Mkuu PM, maneno mazito sana haya.

Respect.

FMES!
 
Ungekuwa mwanamke ungeona substance. Hivi nyinyi mbona mnajipendelea hivyo? Bunge sasa limejaa asilimia 70 wanaume wasiofanya chochote cha maana. Asilimia 90 ya wabunge wanaume ni mafisadi, hebu nieleze sasa mafisadi wanawake kule bungeni ni wakina nani? Nchi za Scandnavia wameweka hizo goals sasa ona wanawake wanavyofanya kazi vizuri tu sambamba na wanaume kwa maendeleo ya nchi zao. Hebu badilini fikra huko. Ndio ubaguzi huo huo ambao CCM inaufanya dhidi ya wapinzani kwa kusema kuwa kwani hao ni wanini. Na hata kwenye CCM yenyewe vigogo na watoto wao wanawabagua wengine kwa kuhoji ni kwanini wapate uongozi

Asha

Hoja ni kuwa huo mgawanyo wa 50 kwa 50 uangalie uwezo. Kama wanaume waliochaguliwa tayari wana matatizo je na wanawake nao wachaguliwa kwa sababu ya gender balance tu? Bila kujali kama wana uwezo? Hapa inabidi kuweka umimi pembeni. Unasema wanawake si mafisadi uko bungeni una DATA au unaongea tu? Huyo Meghji huyajui yake? Mlaki je? Mongera je? Mwangunga je? Daftali? Au unataka wawe kama Rostam ndiyo wawe mafisadi? Itabidi ukacheki definition ya mafasadi. Acheni kutetea uozo kwakuwa eti ni wanawake nao wanamatatizo tena makubwa tu.

Hata hao wanawake wa viti maalum kama unavyowaita ni asilimia ngapi wanaofanya kazi? Mimi naona wameongeza mzigo ilitakiwa kama taifa linataka gender balance then walewale waliokuwepo wagawanywe bila kuongeza namba. Kwani wanayofanya sasa hivi ni kuongeza mzigo na hakuna linalofanyika. Kwani tangu wameongeza hao wabunge wa viti maalum kuna nini jipya? Si wanalala tu kama wengine? Ukweli ni kwamba percent ni ndogo. Hivyo ni vizuri utaratibu utakapoanza bora uwe mzuri ili wanawake wakifanya vizuri then na wanaume wataona aibu wafuate. Lakini tukitumia siasa kama ilivyosasa sidhani kama tutafanikiwa kama nchi ulizotolea mifano.

Harafu kingine mimi nilifuatilia wale wa nje si kuwa walipewa tu nafasi. Kilichofanyika ni kuwa kule hakuna hiki ni cha mwanamke au mwanaume. WOTE WAKO SAWA TENA KUNA NCHI KAMA DENMARK MWANAMKE NDIYO YUKO JUU YA MWANAUME. Kafuatilie ni percent ngapi wako kwenye uongozi? Nao hao waliopo kama walibebwa? WALIPIGANA WENYEWE KUWA KUWA WALIONYESHA KUWA NI VIONGOZI WAZURI.

Issue hapa si kulazimisha eti kwakuwa ni uongozi unatakiwa then lazima wanawake wawepo. Je wako tayari? Au utayari ni kupewa tu nafasi za bwelele? i think hii nayo ni manyanyaso kwa wanawake. Inatakiwa wapewe nafasi wakijitokeza wapewe wao tu. WAKIJITOKEZA WAPEWE KIPAUMBELE SI KUPEWA NAFASI ZA BURE HIYO SI HAKI.

KWAHIYO WANAWAKE INABIDI WAJUE KUWA CCM INAONA IKISIMAMISHA WANAWAKE KWENYE MAJIBO LABDA ITASHINDWA HIVYO NI BORA WAANZIE HUKU VITI MAALUM WALE WATAKOJITOKEZA KUWA WAZURI THEN WAPELEKWE MAJIMBONI. Mfano Jenista Mhagama, Dr. Nagu, na wengine. CCM IFANYE KAMA RWANDA KAMA KWELI INATAKA KUSAIDIA WANAWAKE NA VYAMA VYOTE IWE HIVYO.
 
Vyama vya upinzani visifumbwe macho na ruzuku wanayopata toka serikalini; ni muhimu kwa sasa washupalie katiba ya sasa ibadilishwe ili iendane na mfumo wa vyama vingi, wasikubali kwenda kwenye uchaguzi na CCM kabla ya mabadiliko ya katiba . Itakuwa bora wakasusia chaguzi zote mpaka katiba imebadilika ama sivyo kukubali kwenda kwenye hizo chaguzi kichwa kichwa CCM itawachinja kama mbuzi machinjioni!!
 
Naomba tu kusema kuwa hiyo idadi ya wanawake na wanaume 50/50 bungeni, siyo agenda ya nyumbani bali ni moja ya agenda za kidunia ambapo nchi zilikubaliana kuwa ifikapo mwaka 2010 uwakilishi uweze kuvuka kile kiwango kilichowekwa kufuatia makubaliano ya Mkutano wa UN wa Wanawake uliofanyika Beijing 1995, cha asilimia 30 ya wabunge wanawake ( 30% inachukuliwa kuwa ni critical mass kuweza kuwa na sauti ya uwakilishi wa agenda zinazohusu wanawake) na kufikia 50% .Kuna kinachojulikana kama Global campaign for 50/50.Makubaliano hayo yalifikiwa mwaka 2000 katika kikao cha kamisheni ya wanawake ya UN.
Kwa msingi huu, hakuna chama chochote kinachoweza kujidai kuwa kimebuni huo mpango.
Serikali kupitia mfumo wake - wizara ya wanawake na hata ilani yake ya chama maana ndicho kipo madarakani wanachofanya ni kutekeleza makubaliano ya kimataifa kama wajibu.
 
Last edited:
Huyo HabariNdiyoHiyo post zake nyingi huwa zimekaa kiuswahili swahili hivi, najaribu kupata picha jinsi alivyo, na naweza kuona ni mtu gani. Hata vimisemo vyake ni kama uduku udaku hivi, hebu angalia kama "KUZODOA" ni lugha zinazotumika kwenye taarabu zinapopigwa uswazi. Hata signature yake "Ndiyo hiyo", uswahili mtupu !!!
 
Bi. Asha na WomenofSubstanc,

Dada zangu, ndugu zangu hizi habari za 50/50 ni hadithi ambazo zimeandikwa na wanaume kuwapozeni tu. Kitu hiki hakiwezekani sii leo wala kesho ni bora sana kupoteza muda wetu ktk maswala ambayo yanawezekana na yanajenga nchi badala ya kufikiri Uuwiano wa swala zito kama hili.. Hiyo Marekani na nchi za magharibi itachukua miaka 100 ijayo kufikia hata asilimia 40 ya Wabunge wanawake..

Tatizo langu hapa ni uwakilishi, kitu kinachotakiwa ni nafasi sawa meaning hiyo 50/50 inalenga kutazamia UWEZEKANO wa uwakilishi, kuwa mwanamke habaguliwi isipokuwa ana 50/50 chance za kuiandikisha/kugombea na hata Ku win kiti..

Kwa mfano hadi leo hii nchi nyingi zinapuuza na pengine kuondoa majina ya wagombea wanawake..na utakuta nchi za magharibi wanajaribu kwa kiola njia kuboresha mfumo mzima wa Uchaguzi kwa ngazi za vyama hadi Kitaifa lakini sio kulazimisha mfumo utumike ktk swala ambalo linahitaji baraka za wananchi unaowaongoza.

Binafsi naamini kabisa kwamba wanawake wana uwezo sawa kabisa na wanaume ktk uwakilishi wa Wabunge na nina hakika kama vyama vitawaandikisha zaidi ktk kila majimbo kuna uwezekano mkubwa wa wanawake kushinda kutokana na kipaji chao kikubwa ktk ushawishi..

Sasa tunapotaka kutumia kile kinachotokea bungeni na kukilazimisha kuwa sababu ya msingi kuwapa nafasi wanawake kwa sababu tu ni wanawake tunakuwa tunapotosha maana na nguvu ya wanawake ktk jumuiya zetu. Ni kosa kubwa kwa mwanamke kufikiria gender kama sababu ya kugombania kitu ambacho yeye mwenyewe hana mbinu ya kukitatua..Hivyo sababu kubwa ya kuwepo kwa wanawake Bungeni inatanguliwa na sifa na uwezo wa mtu huyo kuwakilisha kwa sababu matatizo mengi ya ndani, mwanamke ndiye yupo karibu zaidi ya mwanaume...

Ni hoja ambayo ina mjadala mkubwa lakini ndio ukweli kama vile majumbani mwa watu. Matatizo mengi ya ndani ya nyumba huyajua mwanamke na ndiye mwakilishi bora wa matatizo ya ndani ikiwa ni pamoja na watoto kuliko mwanaume..lakini huwezi kutambua ubora wa nyumba moja kutokana na uwakilishi wa mtu mmoja, kila nyumba na kila familia ina mwakilishi bora wa matatizo yake kuliko mzazi mwingine..
Na mwisho mtanisamehe, ktk hili nalokusudia kusema...Mwanamke fisadi ni hatari zaidi kuliko mwanamme..kwa sababu she controls the house!..
Waswahili wanasema ni bora mtoto anayeteswa na baba wa kambo kuliko yule anayeteswa na mama wa kambo!
 
Mkuu Mkandara,
Msimamo wangu kuhusu 50/50 representation nimeuweka -reserved maana I have my own standpoint.Nilichoonyesha kwenye post yangu ni genesis ya hizo asilimia - kwamba siyo a novel/creative idea ya chama chochote cha siasa - iwe chama tawala au upinzani.Ni matokeo ya michakato ya kimataifa.
 
Kwani title ya mada ina tatizo gani? Si inaripoti tu kilichotokea!

.........ndiyohiyo

Your Credibility is questionable here at JF!

Ulianza na

1: Lwakatare kuhamia CHADEMA

2: Ukaja na CHADEMA mbioni kubomoka

HabariNdiyoHiyo wewe ni MWONGO, MCHONGANISHI, MSHAKUNAKU, MBEYA, MGOMBANISHI, MZUSHI na MWENYE WIVU na KIJICHO. Na Utakufa nacho KIJIBA cha ROHO
 
Mkuu Mkandara,
Msimamo wangu kuhusu 50/50 representation nimeuweka -reserved maana I have my own standpoint.Nilichoonyesha kwenye post yangu ni genesis ya hizo asilimia - kwamba siyo a novel/creative idea ya chama chochote cha siasa - iwe chama tawala au upinzani.Ni matokeo ya michakato ya kimataifa.

Nauliza!

Why Men 50 nad Women 50 kwa nini isiwe Men 40 and Women 60
 
Womenof Substanc,
Sipingi wala sikatai msimamo wako lakini nilichosema mimi ni kwamba unavikwa kilemba cha ukoka..ni jambo ambalo haliwezekani ktk dunia inayotawaliwa na wanaume.. Ni hadithi ya kufikirika japo inafaa kuweka hope, afadhali hata Palestine kupata Uhuru wake naweza sema labda kesho itakuwa.
 
Kwamba Hakuna uwezekano wa kufikia 50/50 bila kuteuana? Kwa nini usiwekwe utaratibu Mzuri wa Wanawake kugombea Majimboni? Hivi wateuliwa watawajibika kwa Wananchi au kwa waliowateua kumbuka na wao watapenda next time Wateuliwe tena so ni Ngumu kwa wao kwenda against Waliowateua. Hivi hakuna Hasara ya kuwa na Watu karibu 40% Bungeni ya Watu wanaowakilisha Waliowateua.

Just Curious
 
Nasema hivi kwa Maana tumeona Wateuliwa ( Hasa wa Chama Tawala) walioko Bungeni, wao wanafeel a certain Obligation kwa Walio Wateua yaani wanaona kwamba wanastahili kulipa Fadhila Fulani kwa Serikali
 
..eti wanawake na wanaume 50/50 bungeni!!

..waendeleze basi ratio hiyo hiyo mpaka mashuleni na kwenye ajira.

..hizi ni siasa tu, na wala hakuna nia ya dhati ya kumkomboa mwanamke.

NB:

..au kwanini wasipitishe azimio kwamba baraza la mawaziri liwe 50/50? i think that can be implemented a lot quicker kuliko hii habari ya wabunge.
 
Nadhani kama kweli kawa Wanaume wana Dhamira ya kweli ya 50/50 represenation Mjengoni, basi watengeneze a Level Playing Field kuanzia kwenye Vyama vyao ili kuwe na Uwiano mzuri wa WAGOMBEA nafasi za Wabunge, lakini tuking'ang'ania nafasi NYINGI za Upendeleo hapo tutakuwa tunapeleka Misukule ya Serikali Mjengoni.
 
Back
Top Bottom