Nape amzodoa kwa aibu Mnyika kuhusu wanawake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape amzodoa kwa aibu Mnyika kuhusu wanawake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Apr 5, 2009.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape amzodoa kwa aibu Mnyika kuhusu wanawake

  Mwanasiasa shupavu na mjumbe wa NEC ya chama tawala(CCM) Nape Nnauye amemzodoa kijana wa CHADEMA, John Mnyika kuhusiana na kauli zake kuhusu uwakilishi wa wanawake katika siasa.

  Tukio hilo lilitokea katika Mkutano uliondaliwa na Kituo cha Demokrasia(TCD) uliofanyika hivi karibuni.

  Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto, Dr Nkya ambae pamoja na mambo mengine aliisifu CCM kwa kuwa mstari wa mbele kwa kuwajali wanawake kwa kupitisha mfumo wa uwakilishi wa 50 kwa 50 baina ya wanawake na wanaume. Waziri Nkya alivitaka vyama vyote kuiga mfano wa CCM.

  Baadaye ilifuatiwa na Mada iliyowasilishwa na waziri kiongozi wa zamani wa Zanzibar Dr Ghalib Billal ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati iliyotoa mapendekezo kuhusu namna ya kupanua uwakilishi wa wanawake bungeni. Dr Billal alieleza kuwa kamati yake imeiwezesha CCM kupitisha mfumo ambao utawezesha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 uwakilishi baina ya wanawake na wanaume kuwa 50 kwa 50.

  Majadiliano yalipofunguliwa kiongozi Nape Nnauye naye akaeleza kwa kina kuwa CCM iko mstari wa mbele katika kuweka viongozi katika nafasi za uongozi kupitia mfumo wa 50 kwa 50 na kwamba suala hilo limetokana na ilani ya chama hicho.

  Alipopewa nafasi ya kuchagia kwa upande wake, kijana Mnyika alitaka kwamba wajumbe wachangie bila kujali vyama vyao wakitanguliza maslahi ya taifa na kueleza ukweli wa hali halisi ilivyo Tanzania ili wadau washirikiane kuleta mabadiliko ya kweli.

  Kijana Mnyika alikwenda mbali zaidi kwa kubeza kwamba hakuna chama nchini ambacho kimepitisha mfumo wa 50 kwa 50 katika katiba ya chama chao. Alisema vyama vyote vikubwa, vya CCM, CHADEMA na CUF katika katiba zao hakuna mfumo 50 kwa 50, na kwamba kilichopo katika vyama hivyo ni uwakilishi wa asilimia 30 tu ya wanawake katika marekebisho ya katiba za vyama hivyo.

  Kijana Mnyika aliendelea zaidi kuwa hakuna dhamira ya kisiasa toka kwa chama tawala kuweka mfumo wa uwakilishi wa asilimia 50 kwa 50 katika uchaguzi wa mwaka 2010. Alisema kuwa amegusa dhamira ya chama tawala kwa kuwa chama hicho kina uwingi mkubwa bungeni kwa sasa hivyo mabadiliko yoyote ya kimfumo lazima yatokane na dhamira ya kweli kwa upande wa chama hicho.

  Alisema kwamba anao ushahidi wa CCM kutokuwa na dhamira hiyo kwa kuwa anayo maazimio ya kikao cha NEC chama cha hicho kilichofanyika tarehe 7 mwezi Machi, mwaka 2009 na maamuzi ambayo chama hicho kimefikia kuhusu mfumo wa 50 kwa 50.

  Aliituhumu NEC ya CCM kwamba imepitisha azimio la chama hicho kuielekeza serikali kufanya haraka marekebisho ya katiba yatayofanya bunge liwe na wabunge 360.

  Pia NEC imeitaka serikali kuongeza wabunge wa viti maalumu kufikia 109. Na Hatimaye NEC imeitaka serikali imuongezee zaidi Rais mamlaka ya kuteua Wabunge na sasa aweze kuteua Wabunge 14 na kati yao apewe nafasi ya kuteua wabunge wanawake 7. Bwana Mnyika akasema kwamba chini ya maelekezo hayo ya NEC ya CCM kwa serikali uwakilishi wa wanawake wa moja kwa moja utakuwa ni wabunge 109, na wabunge wengine 7 ambayo jumla ni 116 ambayo ni sawa na asilimia 33%. Bwana Mnyika alisema kwamba asilimia hiyo sio 50% ambayo ndiyo inatakiwa katika mfumo wa 50 kwa 50. Hivyo akaituhumu CCM kwa kufanya propaganda za kisiasa za kuwarubuni wanawake kuwa inawajali wakati ambapo tayari imeshapitisha maazimio ya marekebisho ya katiba ambayo hayaendani na kauli za CCM za majukwaani kuwa imepitisha mfumo wa 50 kwa 50. Kijana Mnyika alisema kuwa nusu ya 360 ni wabunge 180, hivyo kama mfumo wa 50 kwa 50 basi uwakilishi wa wanawake ungepaswa kufikia kiwango hiko. Kijana Mnyika alisema kuwa kuna tofauti kati ya maneno ya kwenye ilani ya CCM na matendo yanayofanyika kwenye maamuzi ya utekelezaji. Hivyo, alitaka vyama vyote kwa pamoja kukikiri kwamba kama taifa bado hakuna mfumo wa uwakilishi wa 50 kwa 50 kama hatua ya kwanza katika katika kujadili mwelekeo kuhusu suala hilo. Aliendelea kusema kwamba njia pekee ya kutekeleza ahadi hiyo ni CCM kukubali sauti ya wananchi ya kufanya mabadiliko ya katiba ili kuwa na katiba mpya. Akafafanua kwamba mabadililko hayo lazima yahusishe kuingiza katika katika mfumo wa uchaguzi utakaohusisha uwakilishi wa uwiano, lakini suala lisiwe idadi tu bali pia ajenda zinazogusa wanawake wenyewe na mustakabali wa taifa. Alitaka wajumbe kutazama picha kubwa zaidi ya wanawake.

  Kauli hiyo ilimfanya mjumbe wa NEC, kiongozi Nape Nnauye kuingilia kati na kumzodoa mwaka Mnyika kwa kutoa maelezo yasiyokuwa ya kweli. Kiongozi Nape alisema kuwa ni kweli NEC imepitisha maamuzi hayo lakini si kweli kwamba CCM haina dhamira ya kutekeleza mfumo wa 50 kwa 50. Nape alienda mbali zaidi kwa kumweleza wazi Mnyika kuwa CCM haifanyi propaganda katika suala hilo bali ina dhamira ya kweli ya kuweka mstari wa mbele wanawake. Nape alifafanua kuwa tayari asilimia 33 imepangwa kwa ajili ya wanawake pekee, lakini asilimia 17 iliyobaki NEC imeazimia kwamba wapatikane toka majimboni. Kiongozi Nape akataja majina ya wanawake wa CCM ambao wamefanikiwa kushinda uchaguzi katika majimbo mwaka 2005 na akafafanua kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2010 asilimia hiyo 17 ya wanawake itafikiwa na hivyo kufanya wanawake kuwa asilimia 50 katika Bunge. Pia Nape akaeleza kwamba pengine kijana Mnyika hajasoma katiba za vyama kwa kuwa CCM tayari ilishafanya mabadiliko ya katiba yake na kuwa katika uongozi wa ndani wa chama hicho kwa sasa uwakilishi ni asilimia 50 wa 50.

  Baada ya kuzodolewa kwa kiwango hicho, kijana Mnyika aliingilia kati kutaka kutoa taarifa, lakini Mwenyekiti wa Mkutano huo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mama Kidawa ambaye alimwakilisha Makamu Pius Msekwa alikataa taarifa hiyo.

  Mara baada ya Kiongozi Nape kumaliza kuzungumza kijana Mnyika alianza kuchagia bila kufuata utaratibu kuanza kutoa ufafanuzi. Kijana Mnyika alisema kwamba ana hakika kuwa hakuna katiba ya chama chochote hapa Tanzania yenye uwakilishi wa 50 kwa 50, alisema kuwa anachokisema Nape ni kuhusu wajumbe ambao hata kwenye katiba ya CHADEMA wapo 50 kwa 50. Akatolea kwa mfano Kamati Kuu ya CHADEMA inawajumbe 8 wa kuchaguliwa ambao katiba ya chama hicho inaeleza bayana kwamba lazima 50% wawe wanawake, na 50% wawe wanaume, lakini huo sio mfumo wa 50-50 unaozungumzwa. Akasema mfumo wa 50-50 unahusu muundo na uwakilishi wa kikao kizima cha maamuzi sio wajumbe wateule. Akauliza swali washiriki, je, kwa mujibu wa Katiba ya CCM nusu wa wote wanoshiriki kamati kuu ni wanawake?, nusu ya NEC je ni wanawake? Na Nusu ya Mkutano Mkuu nao ni wanawake? Kama jibu ni hapana basi hakuna mfumo wa 50 kwa 50 hapo. Akaanza kuzungumzia mfumo wa uwakilishi 50 kwa 50 katika bunge lakini Mwenyekiti wa Mkutano akamkatanisha na kuruhusu wachangiaji wengine, na kumfanya anyamaze kwa aibu.

  Akichangia Mada hiyo, Afisa wa Uchaguzi(CHADEMA), Mama Suzan Kiwanga alieleza kuwa kama serikali ina dhamira ya kutekeleza mfumo wa 50 kwa 50 badala ya kuanzia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 katika ubunge basi uanzie katika uchaguzi wa mitaa na vijiji unaofanyika mwaka 2009. Hii itawezesha kupata uzoefu kama mfumo huu unatekelezeka. Alisema kwamba ameshangaa katika makubaliano ambayo serikali imesaini na wadau Morogoro mwezi Februari mwaka 2009 kuhusu kanuni za uchaguzi wa 2009, suala la uwakilishi wa 50 kwa 50 wa wanawake halipo. Hivyo, akaitaka CCM na serikali yake kuzingatia suala hilo. Mama Kiwanga akaeleza kuwa kuna ugumu wa wanawake kushinda majimboni kwani yeye mwenyewe aliwahi kuwa mgombea ubunge katika jimbo la Kilombero.

  Wanaharakati mbalimbali wamekuwa wakielezea kuwa wanawake wanakosa nafasi ya kugombea na kushinda majimboni. Takwimu zao zinaeleza kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2005 takribani wanawake 300 walichukua fomu za ubunge na kuingia katika kura za maoni za CCM pekee lakini kati yao waliopitishwa ni chini ya wagombea 20 kupitia chama hicho. Katika takwimu zao wanaeleza kuwa vyama vidogo vidogo kama NLD ndivyo ambayo vinaongoza kwa kutoa nafasi zaidi kwa wanawake kugombea ubunge kupitia vyama hivyo.

  Akitihimisha mada hiyo, Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake hapa nchini(UNIFEM), Mama Salome alisema kwamba amesikia ufafanuzi wa Kiongozi Nape wa jinsi ambavyo CCM imeweka mfumo wa kutekeleza 50 kwa 50. Mkutano huo wa siku mbili, uliohusisha viongozi wakuu wa vyama, wizara, vyombo vya habari na asasi za kiraia ulipitisha maazimio mbalimbali ya jinsi ya kuweka uwiano wa kijinsia katika mifumo ya kisiasa.

  …………ndiyohiyo
   
 2. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hee, hawa CCM vipi? Yaani pamoja na bunge kuwa kubwa hivyo bado wanataka kuongeza idadi ya wabunge. Huu si mzigo kwa walipa kodi ambao wanabeba sasa malipo manono ambayo wabunge wamejiwekea? Halafu wanataka kumwongezea Rais mamlaka ya kuteua wabunge. Hivi kwanini wanashindwa kuelewa dhana ya mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili ya dola? Kwanini Rais apewe mamlaka ya kuingiza watu wengi zaidi kwenye mhimili wa bunge? Hao wateule wa Rais watateuliwa kwa vigezo gani? Si ndio mwanzo wa kuteua marafiki zake?

  Asha
   
 3. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  What is this alll about? Mwanasiasa shupavu/ Kiongozi Nape na ukienda kwa Mnyika anaitwa Kijana Mnyika, Kwani wana tofauti gani? Wote si viongozi kwenye vyama vyao? Yaani muandika habari anaonekana kabisa yuko upande gani! Toka nimeanza kusoma mwanzo najua kabisaa kwamba nitakutana na nini kuanzia intro mpaka mwisho. Tusiandikie mate tunasubiri hiyo 50/50 in 2010 na sio muanze kuweka vimada wenu naomba muweke kinamama ambao wataweza kusimamia wananchi sio ambao watakuwa wanawabeba tuu na hawajali maslahi ya wananchi.
  Na hii ya kuongeza Wabunge ni nomaaa, afadhali Mhe Dr. Slaa anaendelea kuongea kuhusu Mishahara ya wabunge ni mzigo mkubwa tuu na hao wa kuteuliwa sijui ni wanini?
   
  Last edited: Apr 5, 2009
 4. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nakwambia! Halafu kama Bunge litakuwa na wabunge 360, nusu yake si 180. Sasa ukiwa na wanawake 116 hapo 50-50 inakuwaje tena? Hakuna haja ya kusubiri 2010, wanawake tunapaswa kuamka na kuwaambia ukweli CCM kuwa hawajapitisha mfumo wa 50% kwa 50%, mfumo uliopo sasa ni 33% kwa 67%. Sasa hapo hakuna kipya kwa sababu hata bunge la sasa lina 30.3% kwa 69.7%.

  Hivyo CCM ni matapeli tu, waliahidi kwenye ilani yao kuwa ifikapo 2010 watakuwa wameweka katika nchi mfumo wa 50-50 ili kutoa nafasi kwa wanawake. Lakini katiba ya nchi haisemi hivyo na marekebisho hayatasema hivyo

  Asha
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sijaelewa mnagombea nini. This idea is based on a fallacious premises kuwa idadi ya MPs wake kwa waume ikilingana ndio mambo yataenda ipasavyo wakati tunajua kabisa hii haitasaidia kitu. Kwa mantiki hiyo basi conclusion yeyote itakayotoka kwenye mjadala kama huu is simply illogical.
   
 6. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwani nyinyi wanaume ambao ni 69.7% ya bunge hivi sasa mmefanya nini huko bungeni sasa hivi? Sana sana kati ya wabunge wote wanaume tunawasikia zaidi watu sita tu wakina Dr Slaa, Zitto, Sitta, Mwakyembe nk. Wenzetu wako kule 30.3% lakini tunawasikia sana watatu tu wakina Anna Kilango, Halima Mdee nk. Kwa hiyo haipaswi kukataa 50-50 kwa sababu ya ubora tu, kama ni ubora ujadiliwe kwa wote baada ya kuwa na uwiano kwanza humo bungeni

  Asha
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wasiwasi hicho kidogo kilichofanywa sasa huenda kikapotea. Hili suala la kulazimisha katika uongozi si sawa kwani si sote tunapiga kura? Sasa huu mkakati wa kusema jinsia fulani ndio iwe na haki fulani si sawa. Basi na tuweke mwanamke na mwanaume katika mchakato wa kura ili tuone haki iktendeka. Suala la kulzimishana katika uwakilishi ni udicteta.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Dada Asha, you are actually affirming my position.

  Kumbe umebaini over 90 ya wabunge wetu ni bogus, this reduces the issue of gender-based-ratio representation to redundant or secondary if not a non-issue.

  Pia kwa kuongezea hapohapo, suala la 'ubora' wa wabunge wetu sijui huu 'ubora' unapimwaje, na hata 'ubora' wa wabunge wetu ktk positive scale ni independent na issue nzima ya credibility, functionality, effectiveness,etc ya bunge letu ktk kuiweka sawa serikali yetu. Inafikia hatua serikali kuliambia bunge letu kuwa mikataba tunayoiingia ni 'siri' na bunge linaishia kusema 'hewala', na hakuna kinachofanyika.

  Kimsingi najuta kuwajua ninyi wanasiasa.Mmeliingiza hili taifa ktk umaskini mkubwa.
   
 9. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Post hii inahitaji kupepewa!! Sio siri aliyeianzisha naye anahitaji kupepewa too. WTF
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  huyu mwandishi anaonekana ni mpenzi wa nape mnauye sasa asitulazimishe eti nape ni kiongozi shupavu, wakati juzi tu amelia njaa ili wamsamehe arudi kundini!! Tuache ushabiki usiokuwa na maana, kuna tofauti gani kati nape na mnyika, labda majina otherwise they are at the same level. Tena bora mnyika ana uhuru wa kuamua lakini masikini nape hana uhuru wa kujiamulia mambo kisiasa kwa sababu amezoea kuishi kisiasa kwa favor ya wazee wa CCM. Pole nape.
   
 11. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna mtu yoyote ana hayo maamuzi ya NEC ya tarehe 7 Machi ayaweke hapa tuyajadili?

  Hapa hoja ni katiba mpya, na mfumo wa uchaguzi wa uwakilishi wa uwiano. "Kutazama picha kubwa zaidi ya wanawake", maana yake ni nini?

  Asha
   
 12. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  kaaazi kweli kweli! naona mwaka huu tutasoma
  mengi kwenye magazeti kwani ndio yamekuwa
  jukwaa kuu la kisiasa.
   
 13. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  jamani ubunge sio DECI

  haya mambo ya wabunge wakuteuliwa mimi siafikiani nayo kabisa lazima ubunge uwe umepigiwa kura. wabunge wa kuteuliwa ni wapambe wa watu waliowateua na hawana mchango wowote mfano angalia walioteuliwa sasa hivi.

  wanawake hacheni kupenda vya kupewa, jifunzeni ushindani, mbona hillary clinton alikua anashinda na obama.
  bunge linamagoigoi wengi wakuteuliwa halihitaji wengine.
  mbunge aliyeteuliwa hawezi kumpinga rais hata siku moja.

  hizo sera za 50-50 ni za kudumaza wanawake, na kuwafanya wawe tegemezi na zitaongeza ufisadi wa ngono
   
 14. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Najua mnyika anajiandaa kugombea ubongo je Nape naye yupo kwenye list 2010 ya ubungo. kwani sioni kwanini kichwa cha habari kipo kishabiki wakati sioni kinachoshabikiwa.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Apr 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ama kweli tumefikia mahala ambapo sasa Bunge itakuwa kijiwe cha watu badala ya wawakilishi wa wananchi..
  Hadi sasa hivi sieleiwi kabisa hizi habari za Kuteua watu kuingia Bungeni kwa jinsia zao wakati hawawakilishi kundi la jinsia hiyo ama maswala yanayohusiana na usawa unaotafutwa. Hivi kweli usawa huo unaotafutwa pale bungeni au ni ktk maamuzi yote yanayoipitiwa bungeni yasiwaache wanawake nje..

  Yawezekana mimi ndio nashindwa kuelewa, lakini nia na madhumuni ya Bunge ni UWAKILISHI... sasa ikiwa bungeni kwetu maswala mengi ya wanawake yanapuuzwa ni muhimu kwa rais kuteua mbunge wa vyombo vya wanawake kwa mfano Umoja wa Wanawake Tanzania (uwe wa nchi nzima sio chama kimoja), mjumbe wa wanawake ktk Haki Elimu, Afya ya watoto (Maswala ya Mimba na uzazi, chanjo na lishe) na kadhalika.. Hawa Wabunge wa taasisi kama hizi watawakilisha bungeni takwimu za taasisi hizo wakilenga nafasi ya wanawake ktk jamii na mapendekezo na miswada ambayo inakusudiwa kupitishwa ktk kufikia malengo yaliyokusudiwa..

  Haina maana kabisa kuwepo kwa wanawake bungeni kunawakilisha lolote zaidi ya kutafuta ruzuku, ndio hayo ya kugawana umaskini kwani kuna mifano midogo sana imeshindikana na viongozi wanawake wametazama pembeni kwa maslahi yao binafsi.. Hadi leo hii wanawake karibu wote Tanzania wanalia kwamba hawana chombo chao isipokuwa kupitia vyama vya siasa na hakuna wanawake viongozi wala wawakilishi wanaotetea haki hiyo..Kwa nini UWT ni chombo cha CCM?.. ni swali ambalo wanamama hao hao wanasiasa hulikwepa na wameshindwa kuliwakilisha bungeni sasa hiyo hesabu ya wanawake wengi bungeni itabadilisha kitu gani?..

  Siii kwamba napinga mpango wa quotas, ila nachopinga ni kuteua watu kwa sababu unataka kuondoa aibu badala ya kuteua watu kutokana na uwakilishi wake.. Wanawake kwa wingi wao wana matatizo mengi sana ktk kila ngazi ya masiha..Ni ktk kuwakilisha matatizo hayo ndio sababu tunahitaji wanawake bungeni, watu ambao through experience wanaelewa uzito wa matatizo hayo na mapungufdu yake yanatokana napi!.. i.e mwanamke kubeba mimba na hatari zinazoambatana hadi kufikia uzazi..
  Leo hii Tanzania kubeba mimba ni sawa kabisa na kushikwa gonjwa kubwa kama Cancer, anabeba Fifty chances za kuondoka duniani kutokkana na huduma mbovu ya vyombo vyote vya afya..kuwepo kwao wanawake bungeni kumesaidia nini!
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Je ni kweli kuwa nchi zenye idadi kubwa ya wanawake wabunge ama wawakilishi zina maendeleo na utawala bora kuliko zile zenye idadi ndogo ? Katika karne hii huu upendeleo maalumu unasaidiaje katika harakati za kutafuta usawa ? Kuna mwenye data kuhusu idadi ya akina mama kwenye vyuo vyetu vikuu - wanajiunga kwa kuhitimu ama kwa upendeleo maalumu. Na mwisho vipi kwenye nyanja zingine kama uanasheria, udaktari, uandishi wa habari, uhandisi, jeshini n.k.

  Mimi naona ni bora njia za kutoa fursa sawa zinazozingatia uwezo zikiimarishwa zaidi kuliko huu upendeleo unaoliliwa. Samahani akina mama kama kuna atakayekwazika - sina nia mbaya.
   
 17. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Hii kitu ya kupendelewa wanawake ndo unakuta watu wanapata ubunge kwa rushwa za ngono! Hii ni kumdahlilisha zaidi mwanamke!
   
 18. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #18
  Apr 5, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kwa miezi mingi sijachangia mijadala hapa JF kwa sababu mbalimbali. Aidha katika kipindi chote hicho mara chache nimekuwa nikipita hapa na kusoma mijadala ambayo imekuwa ikiendelea.

  Leo nitoe mchango wangu kidogo tu katika mjadala ambao jina langu limetajwa.

  1. Naomba nisitoe maoni yangu kuhusu habari ambayo imeandikwa na kuibua mjadala wenyewe na jinsi ambavyo habari yenyewe imeandikwa, aidha nisingependa kuingia katika mjadala wa majina.

  2. Kwa mtizamo wangu, demokrasia kama ni utawala wa watu kwa ajili ya watu basi mfumo mzima wa kidemokrasia lazima uhakikishe uwakilishi wa makundi muhimu ya kijamii, ni kutokana na mtazamo huu ndio maana toka miaka ya 90 nimekuwa nikuzungumzia haya ya makundi ya kijamii hususani vijana kupewa nafasi katika vyombo vya maamuzi. Na wakati wote nimekuwa nikisema kwamba vijana kwa kuwa ni wengi katika jamii lazima uwakilishi wao katika vyombo vya maamuzi uwiane na idadi yao na nafasi yao katika taifa. Ni kutokana na msimamo huo huo ndio maana naamini kuwa wanawake nao wanahitaji nafasi katika vyombo vya maamuzi

  3. Hata hivyo, miaka yote hiyo nimekuwa nikisema suala sio idadi tu ya vijana bali lazima kuangalia uwezo wao wa kiuongozi ikiwemo maadili yao, maono yao na mambo mengine yenye kuleta tija katika uwakilishi wao. Hivyo, suala sio uwepo wao katika vyombo vya maamuzi bali pia mchango wao katika ajenda zinazohusu taifa na hata ajenda zinazogusa kundi lao. Kwangu mimi ilikuwa ni afadhali mzee anayejali maslahi ya taifa na ya vijana kuliko kijana asiyejali maslahi ya vijana wenzake. Nina maoni hayo hayo katika masuala ya viti maalum na ushiriki wa wanawake. Suala si kuwa tu na wanawake wengi, bali kuwa na wanawake wenye kusimamia maslahi ya taifa na maslahi ya wanawake wenzao mathalani masala ya vifo vya watoto na wakina mama wajawazito kutokana na mfumo mbovu katika sekta ya afya

  4. Nimekuwa nikisisitiza kwamba tuna uongozi mbovu, hata katika kundi kubwa la wanaume wengi wao wakiwa wazee wanaongoza sasa katika vyombo vya maamuzi kuna wabovu wengi sana, nimekuwa nikisema tunahitaji mabadiliko ili kutoa fursa kwa kizazi kipya kuchukua nafasi za uongozi. Mwongelezo wa hoja hiyo ni haja ya kutoa fursa kwa makundi ya kijamii mengine ikiwemo wanawake

  5. Hivyo, hoja kuu wakati wote ni nimesisitiza kuwa ni kubadili katiba yetu, mifumo yetu ya kisheria na mitazamo yetu ili kuweka uwanja sawa wa kisiasa ili kuwezesha viongozi bora kuweza kushiriki katika uchaguzi na kushinda. Chini ya demokrasia ya kweli vijana, wanawake na walemavu walioviongozi wazuri wote watashinda na kuchangia katika kujenga taifa lenye kupambana na ufisadi, kutumia vizuri rasilimali na kutoa fursa kwa raia waliowengi. Hili ndio suala kipaumbele

  6. Kuhusu mfumo wa uchaguzi, ningependa katiba ibadilishwe kuruhusu mfumo wa wa mchanyato utakaokuwa na uwakilishi wa wengi wape na ule wa uwiano mpana badala ya viti vya uwiano kuwa ni vya wanawake pekee. Niliwahi kuandika mwaka 2006 mada ndefu kuhusu uendeshwaji wa uchaguzi ambayo nadhani ni rejea ya muhimu sana katika mjadala huu. Hata hivyo, hoja yangu niliyotoa siku hiyo kwenye mkutano ililenga kueleza wazi kwamba maamuzi ya NEC ya CCM ya Machi 7 ni kinyume kabisa na nadharia ya 50 kwa 50 na ahadi ambayo chama hicho kilitoa kwa wanawake na watanzania kwa ujumla. Hivyo, yanayosema jukwaani kuhusu suala hili ni propaganda tu zilizotofauti na hali halisi ya maamuzi ambayo CCM imeshayafanya ndani. Na nilichukua fursa hiyo kuwataka wadau bila kujali itikadi kuunganisha nguvu kupinga maelekezo ya mabadiliko ya katiba na sheria ambayo NEC imeshayatoa kwa serikali. Maelezo ambayo kwanza yanaongeza mzigo wa gharama kwa kuongeza idadi ya wabunge, yanaongeza mamlaka ya uteuzi kwa Rais lakini wakati huo huo hayatakelezi azma inayotajwa ya marekebisho hayo ambayo ni 50 kwa 50 badala yake yanapeleka kwenye asilimia 33 suala ambalo si kipaumbele cha marekebisho ya sheria ya uchaguzi ama ya katiba ya nchi yanayohitajika kwa sasa.
  JJ
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Najua una mambo mengi ambayo wakati mwingine yanakufanya ushindwe kushiriki mijadala mbali mbali hapa ukumbini, lakini tafadhali usipotee kwa muda mrefu kiasi hicho. Uchangiaji wenu unahitajika sana hasa wakati huu tukielekea kwenye uchaguzi Mkuu wa 2010.
   
 20. O

  Ogah JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  .......Unajua hata title ya mada yenyewe tu binafsi naona shida kuendelea kuchangia.........
   
Loading...