Nape ampinga Makamba kwamba hata JK sio maarufu kuliko Chama

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Makamba aliwahi kusema “CCM hatuwezi kamwe na wala hatuna mpango wa kumtosa katika kinyang’anyiro cha mwakani Rais Kikwete kwa kuwa ni maarufu kuliko hata chama chetu, huwezi kumtosa mtu kama huyu na wanaosema hivyo ni wehu wasioitakia mema CCM,” alisema Makamba.(Habari leo, Jumanne Agusti 02, 2011 - HabariLeo | Mwacheni Kikwete, ni mtaji – Makamba)

Nape nimemsikia live ITV akisema tena kwa msisitizo "hakuna mtu aliye maarufu kuliko chama".

Nape unachotaka kutuambia ni kwamba Makamba alipotoka kutuambia kwamba JK ni maarufu kuliko chama?, au umaarufu wake sasa umeshuka kwamba haya yeye akileta mchezo mnamtimua?.

Hapo kwenye red nape panakuhusu kwa kuwa umesema hakuna mtu maarufu kuliko CCM na hukutoa exception. Inawezekana kweli huitakii mema CCM na unajiandaa kuanzisha CCJ mpya CCM ikifa.

Poleni CCM, sisi tuko makini na popcorn zetu tunafuatilia hili movie.
 
Watanzania mnakera kwa kuendekeza kujipendekeza.

Uongo wa Nape uko wapi hapo?

Nape, keep it up. Unatuonyesha kwamba kipindi cha kujipendekeza kwa kutoa kauli tamutamu kwa viongozi kimepitwa.

Kama ni kweli JK si maarufu kuliko CCM basi simamia ukweli huo.

Wanaochukia waambie 'They can go to hell'
 
Nape big up, kila mstari ukiongea kesho JF ni thread, upo vizuri sana. BAAASII
 
Watanzania mnakera kwa kuendekeza kujipendekeza.

Uongo wa Nape uko wapi hapo?

Nape, keep it up. Unatuonyesha kwamba kipindi cha kujipendekeza kwa kutoa kauli tamutamu kwa viongozi kimepitwa.

Kama ni kweli JK si maarufu kuliko CCM basi simamia ukweli huo.

Wanaochukia waambie 'They can go to hell'

Nape kasema ukweli uliopo katika kila taasisi ya umma. Mtu mmoja anaweza kuwa maarufu kuliko wengine katika individual capacities zao na ndivyo ilivyo kwa JK na CCM lakini, hakuna mtu mmoja mmoja ambaye ni mkubwa kuliko taasisi anayoiongoza. Nape has stated the obvious.
 
chama cha siasa kisichokuwa na watu wenye umaarufu wa fikra za kuwakomboa wa wananchi chama hicho
hufa na kupotea,umaarufu wa mtu hujengwa hujengwa na kubomolewa na norms and values za chama, the roots of become maarufu is the structures of the party but broadly individual is just the agent of the party structure
 
Nape anarapu tu. Kumbe hajui itikadi za wanamagamba wenzake.! Niwajuavyo mimi chama cha magamba, nape akiendelea kuropoka itamkosti. Hivi anadhani wengine wote hawaoni au hawaelewi..ha ha haa. Sikio la kufa.!
 
Nape kasema ukweli uliopo katika kila taasisi ya umma. Mtu mmoja anaweza kuwa maarufu kuliko wengine katika individual capacities zao na ndivyo ilivyo kwa JK na CCM lakini, hakuna mtu mmoja mmoja ambaye ni mkubwa kuliko taasisi anayoiongoza. Nape has stated the obvious.

Si taasisi za umma pekee. Niko katika private sector.

Tunapaswa tutangaze hali ya hatari kwamba 'Kujipendekeza' kwa mkubwa ni janga la kitaifa.
 
Ligi ya magamba imefika pazuri huyu anaongea hili kesho kaibuka mtu mwingine anakuja na lingine mimi nasubiri "the end will tell the truth"
 
Makamba aliwahi kusema "CCM hatuwezi kamwe na wala hatuna mpango wa kumtosa katika kinyang'anyiro cha mwakani Rais Kikwete kwa kuwa ni maarufu kuliko hata chama chetu, huwezi kumtosa mtu kama huyu na wanaosema hivyo ni wehu wasioitakia mema CCM," alisema Makamba.(Habari leo, Jumanne Agusti 02, 2011 - HabariLeo | Mwacheni Kikwete, ni mtaji – Makamba)

Nape nimemsikia live ITV akisema tena kwa msisitizo "hakuna mtu aliye maarufu kuliko chama".

Nape unachotaka kutuambia ni kwamba Makamba alipotoka kutuambia kwamba JK ni maarufu kuliko chama?, au umaarufu wake sasa umeshuka kwamba haya yeye akileta mchezo mnamtimua?.

Hapo kwenye red nape panakuhusu kwa kuwa umesema hakuna mtu maarufu kuliko CCM na hukutoa exception. Inawezekana kweli huitakii mema CCM na unajiandaa kuanzisha CCJ mpya CCM ikifa.

Poleni CCM, sisi tuko makini na popcorn zetu tunafuatilia hili movie.

Vuvuzela haliitaji kufikiri, linapiga kelele tu. Hata MKiti wake anamdharau.
 
kwa mara ya kwanza leo namuunga mkono Nape. Mtu hawezi kuwa maarufu kuliko chama chao. Hata Dr wetu wa ukweli si maarufu kuzidi CDM
 
aiseee Asiye kupenda hawezi kukusaidia...Wanajaribu kila sababu kuonesha CCM haifai,,..Nape kawashika pabaya.
Kawashika pabaya akina nani? Labda akina RECHAL na sasa anamshika pabaya mwenyekiti wake wa chama.
 
Back
Top Bottom