NAPE akiwa Mwanza afunguka kuhusu CCM kupoteza mvuto

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
FRIDAY, SEPTEMBER 23, 2011

NAPE AKIWA MWANZA AFUNGUKA KUHUSU CCM.



Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kwamba licha ya madai kuwa chama hicho kimepoteza mvuto mbele ya jamii lakini takwimu zinaonyesha watashinda katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Igunga mkoani Tabora.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Mwanza, Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema kwamba wanaodai kuwa Chama hicho kimepoteza mvuto wanatumia hoja za jumla badala ya takwimu. Amesema kwamba utafiti mdogo alioufanya katika mikoa 12 kwa kuangalia matokeo ya chaguzi ndogo za serikali za mitaa zilizofanyika kati ya mwaka 2009 hadi 2011, unaonyesha kuwa CCM bado ina mvuto mbele ya jamii na ana uhakika wanashinda katika uchaguzi mdogo wa ubunge huko Igunga.




Mikoa ambayo amefanya utafiti ni pamoja na Mara, Pwani, Dar es salaam, Shinyanga, Mbeya, Manyara, Singida, Morogoro, Mtwara, Arusha, Tabora na Tanga pia katika mikoa hiyo kwa kipindi cha kati ya mwaka 2009 na 2011 zimefanyika jumla ya chaguzi ndogo za viongozi wa vijiji 84, mitaa 22 na vitongoji 248.

Kwa mujibu wa Nape, kati ya viti 84 vya wenyeviti wa vijiji, CCM kimefanikiwa kunyakua viti 83 sawa na asilimia 98.8, kati ya mitaa 22, CCM kimeshinda viti 17 sawa na asilimia 77.3 na kati ya vitongoji 248, CCM kimeshinda vitongoji 186 sawa na asilimia 75.




Akizungumzia kuhusu ukali wa maisha Mh. Nape anasema suala hilo linahusiana na uchumi wa dunia na si kwa nchi ya Tanzania.

Akizungumzia hatua ya aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kuachia nyadhifa zake za ubunge na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) akidai kuchoshwa na siasa uchwara lakini akarejea tena katika ulingo wa siasa kumnadi mgombea wa chama hicho Dk. Peter Kafumu, Nape amejitetea kwa kutoa mfano kwa kusema kuwa hata kanisani mtu akifanya kosa kuna adhabu maalum zilizo wekwa kama vile kutokushiriki meza ya bwana na kadhalika lakini siyo kwamba mtu huyo atakatazwa kuingia kanisani, ataingia kanisani kwa minajili ya kulishwa neno kuendana na utaratibu.




Amebainisha kubainisha kwamba Chama Cha Mapinduzi kinao mtaji wa wanachama ambapo katika kura za maoni kuwapata wagombea katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mgombea wa CCM alichaguliwa na wanachama 588 ilhali mgombea wa CHADEMA alichaguliwa wanachama 63.




Kupitia takwimu hizo Nape amejigamba kwa kusema kuwa CCM ina msingi mzuri iliyoujenga wa kushinda katika uchaguzi huo mdogo wa ubunge katika Jimbo la Igunga licha ya fitna zinazojitokeza kila kukicha toka kwa wapinzani wake, hivyo watu wasishangae siku chama hicho kitakapotangazwa kuwa mshindi.
 
Sasa kama CCM imeshapoyeza mvuto, wanasubiri nini kuwaambia wananchi kuwa wameshindwa kuiongoza nchi?...
Sababu wanavuana magamba halafu wanaombana msaada kukipigia tena debe kiti kinachogombewa, hii ni ajabu kabisa!!...
 
Ushindi unaopatikana kwa kuchakachua kura ndo unamfanya aamini kuwa bado wana mvuto?! Waache wizi wa kura basi zipigwe kavukavu waone Kama hawataumbuka. Kupoteza Mvuto kwa wananchi ni hali halisi, ushindi wa kuiba kura siyo hali halisi.
 
Yeah its like he's contradicting himself kwa kauli hiyo, Njaa mbaya sana. Ni kweli hakanyagi Igunga?
 
Hivi Nape amewahi kusoma somo lolote la sayansi? Just curious!!!!!!!!!
 
Nape watu siyo kama hisabati yaani 1+1=2. Inawezekana ukapata jibu la 1+1=1. People do change hata mke wako anaweza akakubadilikia wakati mnalalakitanda kimoja daily akampa mtu mwingine tunda
 
hivi huyu si alitakiwa kuwa igunga huyu..au kafukuzwa kwenye kampeni
 
Tuache utani,
Huyu jamaa mwanaamii mwenzetu hapa barazani mi hua simuelewi kabisa!!
Mtanisaidia kama nitakua nimekosea, nachojua chanzo cha falsafa nzima ya "kujivua gamba" ni baada ya kile kilichosemekana hiki chama kuanza (au kuendelea) kupoteza mvuto wake tofauti na hapo awali ambapo kilikua tegemeo la wanyonge!!
Sasa huyu Mwanajamii mwenzetu akiwa kama ndio mhubiri mkuu wa hii Sera ya kujivua gamba halafu anakua hajui chanzo/maudhui/mantiki ya hii sera ndio nazidi kutomuelewa kabisa.
Unless labda, mimi ndio nitakua sijaielewa hii sera mnieleweshe vizuri!!!
 
MUNGU awalaze mahali pema pepon,mafisid waliwapenda ila kifo kmewapenda zaid kwaheri ccm
 
HIVI HUYU JAMAA SINIMKUU WA WILAYA GANI SIJUI AU KUMBUKUMBU ZANGU SIYO SAWA Je kama ni ndiyo huko wanapataje huduma yake??Hii nchi!
Sijui nikimbilie wapi ugando ndiyo kabisa,Rwanda Mkono wachuma democrasia hakuna,Burundi huko mito yao inabidi ujaze mgrunedi ulalala nayo uchagoni!!Kulikobaki sifanani nako wataninyanyapaa!!
 
Nape... Naamini kabisa madaraka uliyopewa umeyakubali kwa ajili ya maslai yako lakini ukijua CCM inakoelekea siko, Naoomba utusaidia sisi watanzania wenzako, ni kweli chama chako kimekosa mvuto hakifai ni kichafu yani kinanuka.
 
Back
Top Bottom