Nape akataza wafanyabiashara ndogo Kigoma kutozwa ushuru

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

NA MWANDISHI WETU

24th July 2012

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye


Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amepiga marufuku wafanyabiashara ndogo ndogo kutozwa ushuru katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji.

Nnauye alitoa agizo hilo jana katika uwanja wa Senta, manispaa ya Kigoma/Ujiji.

"Lengo la kuja Kigoma na timu yangu ni kutatua matatiza ya wananchi na siyo marumbano na matusi, bali nikuhakikisha serikali ya CCM inawalinda wananchi wote wanaofanya biashara ya mchicha, nyanya, maandazi, vitumbua na vitunguu, ni marufuku kutozwa ushuru na atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria" alisema.

Aliyataja matatizo ambayo ni kero kwa wanachi wa Kigoma kuwa ni kuwatoza wakinamama wajawazito fedha wakati wa kujifungua, watoto chini ya miaka 5 kulipa fedha kwa ajili ya matibabu, wazee kulipa fedha za matibabu, akisema hayo ni makosa kwani serikali ya CCM ilishakataza siku nyingi makundi hayo kulipa fedha za matibabu.

Alisema kero nyingi ni watendaji wa kata kuchukua kitu kidodo kwa ajili ya kuandika barua za dhamana, wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa ajili ya michango mbalimbali pamoja na ada kuonya kuwa watakaobainika wanafanya hivyo watafukuzwa kazi.

Alisema kero kubwa kwa wananchi wa Kigoma ni maji ambayo hayatoki lakini wanatozwa fedha za bili na kueleza kwamba serikali ya CCM imeagiza mita 4,000 ili kila mwananchi afungiwe mita kuondoa malalamiko ya kutoa fedha bila ya maji kutoka.

Aidha alisema serikali ya CCM imeazimia kuimarisha reli, bandari pamoja na miundombinu ya barabara za lami ili kukuza kilimo katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Kagera.


CHANZO: NIPASHE


 
Kumbe Nape Cheo Chake Kikubwa... Alipokuwa Mtwara aliongelea Juu ya Kiwanda kuondolewa - Acting Waziri wa Viwanda

Sasa Anaongelea Kodi - Acting Waziri wa Fedha/ Nakitaka hicho cheo
 
Bado andhani CCM nao ni muhimili wa dola

"Lengo la kuja Kigoma na timu yangu ni kutatua matatiza ya wananchi na siyo marumbano na matusi, bali nikuhakikisha serikali ya CCM inawalinda wananchi wote wanaofanya biashara ya mchicha, nyanya, maandazi, vitumbua na vitunguu, ni marufuku kutozwa ushuru na atakayekiuka agizo hilo
atachukuliwa hatua kali za kisheria
" alisema.


 
Alisema kero kubwa kwa wananchi wa Kigoma ni maji ambayo hayatoki lakini wanatozwa fedha za bili na kueleza kwamba serikali ya CCM imeagiza mita 4,000 ili kila mwananchi afungiwe mita kuondoa malalamiko ya kutoa fedha bila ya maji kutoka.


Kwa hiyo akifunga hizo mita maji yatatoka au
Maana hapo sijaelewa kabisa
Maji hayatoki wananchi wanatozwa bill bila kuyaona maji na then mtu anaagiza mita ziletwe ili wananchi wafungiwe
Kwani tatizo hapo ni mita au maji kutotoka

 
Kwa hiyo akifunga hizo mita maji yatatoka au
Maana hapo sijaelewa kabisa
Maji hayatoki wananchi wanatozwa bill bila kuyaona maji na then mtu anaagiza mita ziletwe ili wananchi wafungiwe
Kwani tatizo hapo ni mita au maji kutotoka
Nape na dhaifu uwezo wao wa kufikiri unafanana
 
Kilichobaki sasa ni kujaribu kila linaloweza kurudisha heshima, hata kama ni kuingilia wizara za wengine!
 
juzi katibu mkuu wa ccm mukama,katishia kujiuzulu kisa kuingiliwa majukumu na nape, leo tena anaingilia kazi za mkurugenzi wa halmashauri.
TUSUBIRI KUSIKIA NAPE KASAMEHE WAFUNGWA
 
sijawahi kusikia nchi yoyote hapa duniani katibu mwenezi wa chama anaongea kwa niaba ya serikali au mawaziri hivi huyu nape anajisahau kwamba yeye he's only a katibu mwenezi, anapiga marufuku kama nani? ndio maana akina mukama na makamba wanammaindi
 
Huyu bwana mDogo anaijua bajeti ya halmashauri ya Kigoma kweli?

Hivi vyanzo vya mapato mimi najua ni kodi sasa kama tunasamehe kodi ili kupendezesha watu itafika mahali nchi itashindwa kujiendesha, maana badala ya kung'ang'ania vyanzo halali tunaona ni heri tukope benki na taasisi nyingine kuliko kuwatoza kodi wafanya biashara ndogo ndogo lakini mfanyakazi wa kima cha chini unamlima kodi.
 
ama kweli hii nchi kila mtu anamaamuzi yake ,na mimi naamuru kuanzia leo hakuna BAN JF
 
ivi nape ana authority gani kwa wananchi wa tanzania as general ???ngoja na mimi kesho nikafute ushuru kwenye haka ka soko mjinga hapa kwenye uwanja wa fisi
 
Back
Top Bottom