Nape akata rufaa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape akata rufaa CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 29, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,407
  Likes Received: 81,436
  Trophy Points: 280
  Date::9/29/2008
  Nape Nnauye aitambuka Umoja wa Vijana akata rufaa CCM
  Na Kizitto Noya
  Mwananchi

  BAADA ya kimya cha muda, mgombea uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV-CCM), Nape Nnauye ameibuka tena baada ya kukata rufaa CCM kupinga maamuzi ya Baraza Kuu la umoja huo ya kumvua uanachama.

  Nape alikuwa gumzo kubwa wakati CCM ilipoitisha vikao vyake vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) baada ya kuvuliwa uanachama baraza hilo kutokana na kuilaumu jumuiya hiyo ya vijana ya chama tawala kuingia mkataba usio na maslahi kwa chama wa uwekezaji wa jengo la makao makuu ya UV-CCM.

  Baraza hilo, ambalo lilimtia hatiani kwa kusema uongozi, lilisema uamuzi wake ni wa mwisho, huku katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akieleza kuwa hawezi kukata rufaa "mbinguni na duniani" kabla ya Rais Jakaya Kikwete kuieleza NEC kuwa Nape anaweza kukata rufaa na kuzima mgogoro ulioonekana kuanza kuwa mkubwa.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Nape alisema kuwa amewasilisha rufaa yake CCM badala ya mwenyekiti wa UV-CCM, akisema kuwa hawezi kuirejesha rufaa hiyo kwenye kikao kilichomwadhibu.

  "Ni kweli nimekata rufaa lakini rufaa hiyo nimeiwasilisha kwenye chama na sio UV-CCM kwa kwa kuwa siwezi kuipeleka kesi ya nyani kwa ngedere," alisema mtoto huyo wa mwanasiasa maarufu wa zamani wa CCM, Moses Nnauye.

  Nape aligoma kutaja tarehe badala yake alisisitiza kuwa ameipeleka na anaamini itafanyiwa kazi kwa muda muafaka.

  "Nisingependa kwenda mbali... elewa tu kwamba nimekata rufaa kwenye chama na sio UVCCM," alisema alipoulizwa aliwasilisha lini rufaa hiyo lakini akaongeza kusema:

  "Naamini adhabu itabatilishwa na haki itatendeka."

  Akimwaga sera zake wakati wa kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa UV-CCM, Nape alimwaga shutuma nzito dhidi ya viongozi wa juu wa CCM, akiwemo waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, mwenyekiti wa umoja huo, Emmanuel Nchimbi na katibu wa jumuiya hiyo kuwa walihusika katika kuingia mkataba ambao hauna maslahi kwa chama.

  Nape, ambaye alishindwa na Nchimbi kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti wa UV-CCM, pia alisema mkataba huo wa uwekezaji wa jengo la ofisi za makao makuu ya jumuiya, haukupitishwa na vikao halali vya umoja huo.

  Hata hivyo, Nchimbi alijibu tuhuma hizo kuwa mkataba huo ulipitishwa kwenye vikao halali na kwamba una maslahi kwa jumuiya hiyo.

  Hata hivyo, Kamati Kuu ya CCM iliunda tume ya watu watatu ambayo imepewa jukumu la kuhakikisha kuwa maslahi ya UV-CCM yanazingatiwa katika mkataba huo baada ya kuliangalia kwa makini suala hilo kwenye kikao chake kilichofanyika Dodoma.
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nape anatwanga maji kwenye kinu, kishalikoroga alinywe tu sasa ndio matatizo ya wanasiasa magazeti. Haya kiko wapi sasa....
   
 3. P

  Paullih Member

  #3
  Sep 29, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni kama vile amechukua muda mrefu kukata rufaa. maamuzi ya UV CCM kumvua uanachama yametokea takribani mwezi sasa.

  My take ni kwamba amewapa wabaya wake muda muafaka wa kupanga mikakati mbadala. Wajua msemo wa kiswahili hunena, supu yafaa inywewe ikingali moto.

  kwa vyovyote vile, rufaa yake ni sahihi na maamuzi ya haki nadhani yatafanyika ya kumwondolea korokoroni ile ya kutokuwa mwanachama. na hatimaye ashiriki katika kinyang`anyiro cha kugombea uongozi/uenyekiti wa jumuiya hiyo.

  je, mafisadi wataweka mkono wao tena kwenye hiyo rufaa? Mie na wewe hatujui. Tuvute subira!!!!
   
 4. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  We unalako na vijana. Mbona Tinga Tinga aka Mzee Malecela ameshatangaza kuwa atamtetea kwenye kikao? Hukusikia hotuba yake UWT? Yeye ndiye amemwambia akate rufaa CCM.

  Halafu ambae aliona hotuba ya Mzee Malecela, mbona kama alikuwa anawafokea wanawake wenzetu jamani?

  Asha
   
Loading...