Nape aishukia serikali: Inatoa takwimu za uongo, inatumia uhakiki kama kichaka

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amesema Serikali inapaswa kujifunza kutokana na suala la korosho lilivyoenda.

Amesema pia Serikali inatoa takwimu kuhusu malipo ambayo haziendani na ukweli na kushauri iache kuzitoa.

Ameelezea jimboni kwake hali ya malipo ni mbaya japo Serikali inasema inawalipa vizuri.

Pia amesema zoezi la uhakiki limeanza kutumika kama kichaka cha kutumika kuchelewesha malipo na baadae inapotelea hewani.

Hawa jamaa wakiwa na nafasi serikalini hawaoni matatizo ya wapiga kura wanapokuwa nje ya serikali ndipo wanatambua matatizo ya wapiga kura. Nape mwanasiasa mzuri hawi kama kinyonga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Neno uhakiki ni kichaka cha kufichia kushindwa kutimiza uhakiki wa Watumishi ili mishahara ipande hola,uhakiki wa korosho hola
 
Back
Top Bottom