Nape aishukia serikali: Inatoa takwimu za uongo, inatumia uhakiki kama kichaka

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,779
18,747
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amesema Serikali inapaswa kujifunza kutokana na suala la korosho lilivyoenda.

Amesema pia Serikali inatoa takwimu kuhusu malipo ambayo haziendani na ukweli na kushauri iache kuzitoa.

Ameelezea jimboni kwake hali ya malipo ni mbaya japo Serikali inasema inawalipa vizuri.

Pia amesema zoezi la uhakiki limeanza kutumika kama kichaka cha kutumika kuchelewesha malipo na baadae inapotelea hewani.

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amesema serikali inapswa kujifunza kutokana na suala la korosho lilivyoenda

Amesema pia serikali inatoa takwimu kuhusu malipo ambazo haziendani na ukweli na kushauri iache kutoa

Ameelezea jimboni kwake hali ya malipo ni mbaya japo serikali inasema inawalipa vizuri

Pia amesema zoezi la uhakiki limeanza kutumika kama kichaka cha kutumika kuchelewesha malipo na baadae inapotelea hewani

Zitto anamtizama jamaa kama haamini vile!
 
Hata apige makelele namna gani Nape ni mnafiki sana. Hao wananchi wanateswa na chama chake ambacho Mwenyekiti wake ndiye aliyemtuma aende Buyungu kukitetea kwenye uchaguzi mdogo mwaka jana mara tu baada ya serikali kuchukua fedha kwenye mfuko wa kuendeleza korosho. Angekuwa mkweli si angegoma kwenda Buyungu?

Anachofanya Nape ni sawa na kufuga nyoka halafu wewe mwenyewe ulalamike ni kwa nini anawauma watoto wako na wa jirani. Njia rahisi ni kumuua tu huyo nyoka na si kulalamika hadharani kwamba watoto wako na wa jirani wanauawa na nyoka uliyemfuga wewe mwenyewe.
 
Mkuu kwani wewe ukiwa kwenye taasisi fulani mambo yote utakubaliana nayo?
Yeye Nape anaikubali CCM kama chama lakini pia kuna mambo ambayo serikali ya chama hiki inakosea, anasema.. Na ndivyo inavyotakiwa iwe
 
Katika hili alipotakiwa mwaka jana apige kura kwa maslahi ya wapiga kura wake aliungana na serikali. Kuna mambo ya msingi mtu unatakiwa uyapiganie dhidi ya taasisi uliyomo.

Ukiwa kwenye taasisi ya dini halafu watu wanabakwa na kiongozi wa dini ulilyomo na wewe unakaa kimya, usijifanye mbele ya safari kujali waliopatwa na UKIMWI kutokana na kubakwa ulikokukalia kimya!!
 
Hiyo ndiyo wanaitaga machozi ya mamba
Katika hili alipotakiwa mwaka jana apige kura kwa maslahi ya wapiga kura wake aliungana na serikali. Kuna mambo ya msingi mtu unatakiwa uyapiganie dhidi ya taasisi uliyomo.

Ukiwa kwenye taasisi ya dini halafu watu wanabakwa na kiongozi wa dini ulilyomo na wewe unakaa kimya, usijifanye mbele ya safari kujali waliopatwa na UKIMWI kutokana na kubakwa ulikokukalia kimya!!

In God we Trust
 
Hii nchi ilipofika ni pabaya sana. Imagine mtu korosho zake lakini hata kusema tu hajapata pesa ni kosa!!! Kila mkulima asiyelipwa pesa zake anaongelea tumbo kwani hata kumwambia jirani kama hajalipwa ni kos

Ukweli huko Mtwara jahazi linazama, kama hujafika huko huwezi amini inachotokea huko. Kama sio kile kipigo cha gasi walichokipata miaka ile, na huu mfumo wa awamu ya 5, Mtwara nzima ingelipuka lakini hawanamna hata kuongea na jirani tu wanaogopa!.

Ila acha na wakulima waisome namba kwani aliposema msinijaribu wakulima walishangilia eti upinzania sasa umekutana na mwanaume.! Sasa mwanaume yule yule yuko na wakulima wanalalamika!
 
Nappe kaamua kujitoa mhanga
Halafu ameuma kisha akapuliza. Kawalima nyundo ya uhakika kwenye suala la uhakiki, kisha akamalizia kwa kuwashukuru kwa kulifuta shamba lililokuwa limelala. Uma kisha puliza. Hii nayo ni hekima ya aina yake.
 
Katika hili alipotakiwa mwaka jana apige kura kwa maslahi ya wapiga kura wake aliungana na serikali. Kuna mambo ya msingi mtu unatakiwa uyapiganie dhidi ya taasisi uliyomo.

Ukiwa kwenye taasisi ya dini halafu watu wanabakwa na kiongozi wa dini ulilyomo na wewe unakaa kimya, usijifanye mbele ya safari kujali waliopatwa na UKIMWI kutokana na kubakwa ulikokukalia kimya!!
Kwa hiyo ukiwa Mwislam kisa shekhe kalawiti, uislam utakua mbaya sababu ya huyo shehe?
Hautahama, ila utakemea vitendo vya huyo shekhe...na ndicho anachofanya Nape
 
Back
Top Bottom