Nape ahudhuria sherehe za kuagwa wanafunzi wa UDOM ambao ni makada wa CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Monday, May 23, 201j

Monday, May 23, 2011


Katibu wa NEC, Itidai na Uenezi, CCM, Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa CCM tawi la CCM, Chuo cha Sanaa, Lugha na Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Dodoma, katika sherehe ya kuwaaga wahitimu wa mwaka wa tatu wa chuo hicho, iliyofanyika jana kwewnye ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnayue akimkabidhi cheti cha mwanachama mwaminifu wa CCM, Dotto Omari, katika sherehe hiyo
. Mwenyekiti mstaafu wa CCM tawi la CCM, Chuo cha Sanaa, Lugha na Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Dodoma, Salum Nyambi, ambaye anasoma shahada ya Uhusiano wa Kimataifa, akimkabidhi kitabu cha Azimio la Arusha, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, katika sherehe ya kuwaaga wahitimu wa mwaka wa tatu wa chuo hicho, iliyofanyika jana kwewnye ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Sanaa, Lugha na Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakimsikiliza Nape alipounzumza nao, katika sherehe yao ya kuagwa, iliyofanyika jana kwewnye ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma.


Posted by: Bashir Nkoromo
 
Kukubali Nape awe mgeni rasmi imekulwa kwao. Hao wahitimu sijui nani ataawajiri maana wote product za MAGAMBA.
 
Kukubali Nape awe mgeni rasmi imekulwa kwao. Hao wahitimu sijui nani ataawajiri maana wote product za MAGAMBA.
cheki nguvu ya uma huko kitaa
Nadhani sehemu kubwa ya usalama wa taifa ilikuwa huko. Kwa hiyo nguvu ya umma ikaona ni bora kutumia sauti yao. Sauti ya nguvu ya umma ikawa kubwa kuishinda ile ya Mkama na magamba wenziye.
Tena akina Mkama wanadai Mbunge wa chadema Mh. Vincent Nyerere (Chadema) eti amewaibia madawati yao, na hapo ndipo walipochokoza nyuki.
 
Hata wange muita gamba kuu jk, still tunawapa warning na vindoto vyao vya kuitawala tz milele kuwa the time is over for them and their dadiz, mamaz n' suga mamaz n' dadiz. Poleni saaaaaana na mwambieni na huyo nauyee udom sio tena pahala penu pa kujidai ila ndo cimetry yenu milele
 
Huo sasa ni uchokozi sidhani Kama Watanzania tuna kawaida ya kujua makabila ya watu,upo nje ya mada mkuu

Hivi siku hizi kusema ukweli ni uchokozi? kwani wewe ni kiziwi au kipofu? hujui kama wakristo na wachaga hawatakiwi ccm?
 
Hivi siku hizi kusema ukweli ni uchokozi? kwani wewe ni kiziwi au kipofu? hujui kama wakristo na wachaga hawatakiwi ccm?

Mawazo hayo mabaya tuwaachie ccm na ujinga wao,wenye akili tusonge mbele sbb athari za ukabila/udini hakuna asiezijua.
 
Hamna kosa hapo maana anaimarisha chama kupitia UVCCM kama CDM wanavyoimarisha kupitia BAVICHA.
 
Hawa makada jamani mjue walishakata tamaa na lichama lao ila tu kuna vijisenti ccm walitumbukiza hapa vya uchaguzi wakashindwa na nguvu ya umma ndio wakavitumia kupeana vyeti na Nnape akawapa sh.5 million.Kimsingi hawaishi kwa raha hasa ukizingatid kuwa chama chao kimepoteza utamu na UDOM lema kaigeuza ngome kuu ya CHADEMA.Hawa vijana mnaowaona pichani na wengine ni kama mavuvuzela wawapo darasani kwani hata argument zao zimelala kama chama chao.Kuunga sentensi 2 za english kwao ni kazi mno.Wengine wanategemewa kubebwa kwenye mitihani kama baadhi wanavyoonekana pichani.
 
hawa makada jamani mjue walishakata tamaa na lichama lao ila tu kuna vijisenti ccm walitumbukiza hapa vya uchaguzi wakashindwa na nguvu ya umma ndio wakavitumia kupeana vyeti na nnape akawapa sh.5 million.kimsingi hawaishi kwa raha hasa ukizingatid kuwa chama chao kimepoteza utamu na udom lema kaigeuza ngome kuu ya chadema.hawa vijana mnaowaona pichani na wengine ni kama mavuvuzela wawapo darasani kwani hata argument zao zimelala kama chama chao.kuunga sentensi 2 za english kwao ni kazi mno.wengine wanategemewa kubebwa kwenye mitihani kama baadhi wanavyoonekana pichani.
mtu mzima akisema uongo si vibaya kumwambia ametekleza. Haya ya mapesa vyuoni mwizi hudhani kila mtu mwizi.....
tusisahau chuo cha udom kimejengwa kwa juhudi za serikali ya ccm ili wale ambao walikuwa hawapati elimu ya juu sasa wapate kwa kuwepo chuo hichi....lakini pia wale ambao walihitajika lakini hatukuwa nao wapatikane hapa.....ukikosa shukrani wewe sio wote
 
mtu mzima akisema uongo si vibaya kumwambia ametekleza. Haya ya mapesa vyuoni mwizi hudhani kila mtu mwizi.....
tusisahau chuo cha udom kimejengwa kwa juhudi za serikali ya ccm ili wale ambao walikuwa hawapati elimu ya juu sasa wapate kwa kuwepo chuo hichi....lakini pia wale ambao walihitajika lakini hatukuwa nao wapatikane hapa.....ukikosa shukrani wewe sio wote
Nnauye,
Hebu nipite nia tu lakini nichangie hapa kidogo tu.

Ukiona mtu amedanganya,ukatumia lugha ya staha kumwambia 'si sahihi' au 'umeteleza' na ama 'hujafanya tafiti' inapendeza zaidi.

Kuhusu suala la shukrani,nadhani serikali ikitimiza wajibu wake kwa kutumia kodi ya watanzania hakuna haja ya kungoja shukrani.Serikali hiyo ilitoa wapi hizo hela zilizotumika?Kujenga taasisi za elimu au zozote zile ni wajibu wa taifa lolote linalojitambulisha ni la kijamaa ktk Sheria mama (katiba). Sasa sidhani kama ilikuwa ni hisani kutoka serikalini.
 
mtu mzima akisema uongo si vibaya kumwambia ametekleza. Haya ya mapesa vyuoni mwizi hudhani kila mtu mwizi.....
tusisahau chuo cha udom kimejengwa kwa juhudi za serikali ya ccm ili wale ambao walikuwa hawapati elimu ya juu sasa wapate kwa kuwepo chuo hichi....lakini pia wale ambao walihitajika lakini hatukuwa nao wapatikane hapa.....ukikosa shukrani wewe sio wote

Nnauye JR. Mbona hauongelei Matabaka yako? kukanusha au kutetea? au Unajificha kama Mafisadi CCM? Kwanini hautuambii kama wewe ni Mkabila au Mdini? Nyenzo hizo mbili mbona hauzizungumzii? Inaonyesha jinsi CCM inivyo na wababe? na wewe ni kijana damu mpya??

 
Duh!!
hicho chama kimechoka kwa kweli..yaani mbinu mnazotumia zinatia huruma, huwezi amini ni chama kilichopo madarakani kwa miongo mitano sasa..
 
Hivi nyie wanasiasa watanzania lini mtaacha malumbano yasio na maana na kuongelea matatizo ya watanzania na jinsi gani yakuyatatua. Hii JF nikama sehemu moja inaitwa mabwawa 7 karibia na Chuo Kikuu UDSM. Papo karibu na akili za Tanzania lakini pamejaa mavi matupu. Tuongeleeni matatizo makuu ata ma 5 au kumi ambayo yanakabili Tanzania na jinsi ya kuyatatua. Wenzetu wanafanya mambo ya nano-engineering huko sisi tunashindwa ata kuchonga madawati mpaka vodacom waje watufanyie wakati kuna jeshi lisilo pigana vita, vijana chungumzima hawafanyi kazi yoyote. Acheni kujadiliana propaganda. TUAMKE BASI JAMANI!
 
Back
Top Bottom