Nape abeba gunia la kokota, atalitua wapi au kumwuzia nani?

NAPE ni limbukeni wa maisha hajui alitendalo,anaupenyo finyu sana aende akafanyiwe kichenipati.
 
Nape si lolote si chochote,sasa hana pa kukimbilia kwani kote ameisha haribu.Hicho ndicho chama cha magamba kinachotumia wanachama wake kuwavuruga akili wanachama walopokaji kama Nape.Hongera Said Kubenea kwa kumpa elimu Nape ambayo alikuwa haijui.
 
Ni uamuzi wa kawaida tu kwa mtu mwenye akili ya kawaida ya kuishi na watu, tulia kwanza, jifunze kazi ya ofisi yako, ongea na wafanyakazi wa kazi yako, jaribu kuyatazama matatizo yaliyomo ndani ya ofisi yako, pata ushauri kwa wazee wenye uzoefu katika masuala ya uongozi na mahusiano na watu, changanya na uwezo wa fikra, uzoefu na elimu yako, utajua wapi pa kuanzia kazi yako, na nini useme na yapi usiyaseme kwa manufaa ya chama chako, serikali na wananchi ukitilia maanani kutunza heshima na jina lako.

Zaidi ya hayo angetakiwa kwanza ajiulize ni nini walichoshindwa na kuwaponza waliomtangulia, na hivyo asahihishe kasoro hizo. Yeye anakuna na gear babu kubwa ya kuropoka jukwaani kitu kile kile na speed ile ile ya akili Chilingati na Makamba. Wenzake walao mang'amuzi ya maisha yanayoendana na umri wao ilisaidia kumung'unya baadhi ya mambo ambayo wanao ni nyeti kwa taifa, lakini yeye ni kanyaga twende tu.
 
Back
Top Bottom