NAPE aache lugha za kibabe na u 'mimi'...

Bb YangeYange

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
337
184
Tangu Mawaziri wateuliwe na kuanza kazi mara nyingi nimekuwa nikimsikiliza Waziri Nape akiongea anatumia sana neno 'mimi' badala ya kutumia maneno kama 'serikali, serikali yetu, serikali ya awamu ya tano' nk... U ' mimi' huo unaoambatana na ubabe usio wa lazima ndio unaopelekea kuleta migongano isiyo ya lazima na upinzani na kuharibu mantiki ya hoja anazowasilisha. Hata hili la kusitisha Bunge kuonyeshwa live naamini ubabe wake ndio uliosababisha ashindwe kupata namna nzuri ya kuliwasilisha bungeni na kwa Watanzania kwa ujumla. Mbali ya gharama za uendeshaji zipo sababu zingine ambazo kama angeziwasilisha vizuri ingesaidia serikali kueleweka na kuungwa mkono na wananchi wenye kutakia mema juhudi za Rais Magufuli anazozionysha kujali maslahi ya wananchi walio wengi. Kuonyesha bunge live kunawachukulia wananchi muda mwingi wa kazi maofisini, wakulima nk. Wananchi hawa wala si wote wanaoyafanyia kazi wanayosikia bungeni zaidi ya kuchochea malumbano ya kivyama yasiyo na tija kwa taifa.

Katika nchi maskini Tanzania ambayo Rais wake amekuja na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU kwa nia ya kuirejeshea nchi heshima iliyokuwa imepotea na kujaribu kuwaletea wananchi maskini maendeleo kazi kubwa ya wasaidizi wake ni kutafuta mbinu za maneno na vitendo kumsaidia. Nape kwa kiasi fulani angezishtaki dhamira za upinzani kama angeangalia maudhui ya tamko lake bungeni ama popote yawe ya kuonyesha kujenga hoja zitakazoweza kukubalika hats na upinzani badala ya kuonyesha kuwa kuwa serikali ya awamu ya tano inafanya mambo kiubabe. Siri ya mafanikio ya uongozi uliotukuka ni unyenyekevu kwa wananchi hata wawe wapinzani wako. Mawaziri na wasaidizi wengine wa Rais waige unyenyekevu anaounyesha Rais kwa wananchi wote bila kujali vyama, jinsia maeneo nk. Wakifanya hivyo upinzani wataona soni kuleta vurugu zisizo na tija na wananchi wenye nia njema watazidi kuelewa juhudi za serikali yao na kuunga mkono maamuzi hata kama yanawanyima Uhuru kidogo.
 
Back
Top Bottom