Napata tatizo la kizunguzungu kikali nikilala chali

Aqua Man

JF-Expert Member
Mar 17, 2017
336
1,142
Habari za mida wakuu,

Nimekuja kwenue jukwaa hili kuelezea hali ya ajabu ilionikuta leo asubuhi. Nimeamka na kizunguzungu kikali sana na mwili kukosa balance hatimaye nikadondoka.

Baada ya dakika kama 2 ama 3 nilifanikiwa kuamka na kwenda kuoga, ila nilivyorudi tena kitandani nilindondoka tena kwa kizunguzungu kikali. Nikauliza watu nikapewa ushaur niende kupima wingi wa damu pamoja na presha lakini kote hamna kitu.

Sasa muda huu nimerudi kutoka kwenye mihangaiko nikajilaza kwakuangalia juu then nikaamka ikanitokea tena hali hyo hyo ya kizunguzungu kikali sana nikaanguka tena kwa mara nyingine. Nilivyoamka nikajaribu kulala kwa upande wa kushoto na kujaribu kuamka cha kushangaza sijapata kizunguzungu wala nini. Kisha nikajaribu tena kulala kwa kuangalia juu nikajaribu kusimama nikapata kizunguzungu tena.

Naomba kuuliza kwamba hili ni tatizo gani na nifanye nini ili niwe sawa?
 
Pole, kwa jinsi unavyoeleza inawezekana tatizo lako liko kwenye mfumo wa balansi ya mwili iliyoko kwenye sikio.
Hali hiyo huzidi pale unapobadili uelekeo wa kichwa.

Suluhisho: Pata dawa inaitwa Betahistamine/ Betaserc 8mg kila baada ya masaa nane kwa siku tano. Pia, pata muda umwone daktari ili aweze kuangalia masikio yako kama kuna shida yoyote.
 
1. Je unaona ni kama Mazingira yanazunguka mithiri ya ile michezo ya kujizungusha afu ukakosa balance kwa kuona mazingira yako/dunia inazunguka au wewe mwenyewe ndo unaona unapepesuka?

Kwenye Lugha za kitabibu tuna kizunguzungu ambacho tunasema ni Dizziness(Shida inaweza kuwa ya Mfumo wadamu na moyo mara nyingi) au ukasikia kizunguzungu kingine kinaitwa Vertigo na hii uashiria una shida katika mfumo wafahamu specifically kwenye balance system inayoanzia kwenye sikio mpaka kwenye ubongo.

2. Je, upatapo kizunguzungu unasikia kichwa kuuma, unapata kichefu chefu?
 
Kuanza na. Swali kwanza nakua naona dunia inazungua na kwny swali la pili mkuu sipati kichefu wala kichwa hakiumi kabisa
 
Kuanza na. Swali kwanza nakua naona dunia inazungua na kwny swali la pili mkuu sipati kichefu wala kichwa hakiumi kabisa
Nakushauri onana na daktari wa ENT takusaidia ku diagnose shida yako, mara nyingi Vertigo utokana na matatizo ya sikio maana ndo linalohusika na Balance.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom