Napata shida ofisini kwangu goba, majirani wameanza kunichukia

Iyo kawaida sana kuna jamaa yangu mmoja naye alikuwa kawaida tu

Sema alipiga kazi usiku na mchana akanunua gari lake la kutembelea na maendeleo kidogo wakaanza kumuita freemason

Huwa anawaangalia alafu anacheka tu

Hao achana nao piga kazi maskini hizo ndio tabia zao

#Nitauchukia umaskini paka nakufa
 
Mkuu wewe una ndumba za wazi halafu unakataa, unakataa nini?
Ndumba katika biashara/kazi NI wewe jinsi unavyotoa huduma kwa wateja wako kuanzia lugha, Bei zako nk. Hiyo ndiyo ndumba pekee na ya kweli katika biashara. Hivyo wewe fanya kazi habari za story na wao hiyo NI ziada yaani siyo lazima Cha lazima hapo NI kazi.
 
Kibongo bongo ogopa sana kitu au mtu wa jirani yako. Unaweza kuta kuna kiwanja cha jirani yako kinauzwa mfano na benki ukienda kukinunua tu kesi na ugomvi vinaanzia hapo. Au jirani kafukuza hausigeli wake ukamchukua inakua kosa.
 
Ofisi yako ni ipi pale nije kukuungisha?

Kuna hizi tatu zinazokaribiana ukiwa unatokea Mbezi, moja ya mwanzoni iko kushoto, ya pili kulia na ya tatu kushoto karibia na kituo cha daladala. Au kile kidogo pale pale Senta, au ile ya njia ya Makongo.

Wewe ni yupi hapo?
Natamani kukuambia Ila nna mashaka maana humu pia nipo jukwaa la siasa, huko tushazingua sana
 
Tatizo ni wewe mwenyewe, deal na mambo yako usipende kufikiria watu wanakuwazia nn? ''You must learn to ignore their words b'coz it won't degrade you but it degrade them and Forgive them for the love of God''.
Ahsante kwa ushauri
 
Sisi wa bongo wanafki hivyo basi fanya mishe zako hachana na sisi laasivyo ukimsikiliza kila mbwa anayebweka hutafanya kitu




Pia vijana tupo hapo wa kukodi ukitaka tukamvunjie duka jirani yako usiku tupo hapa Manzese

Viongozi wamesema tujiajiri hivyo tunatekeleza agizo

Wewe juha kabisa, unatakiwa kuchomwa moto! Unadhani ni sifa kuongea pumba. Nenda kavunje mlango wa nyumba ya baba yako!
 
Watanzania wenzangu tuwe na huruma, si kila aliyepata alipitia njia ya mkato wapo ambao wamehangaika usiku na mchana kufika walipo.
Nina ofisi ya hardware(vifaa vya ujenzi) kubwa tu hapa goba, nimehangaika nayo hii kuifokisha hapa ilipo kwa jasho.
Nakumbuka nilivyoteseka kuifikisha hapa ilipo, na ni mtaji mkubwa sana umelala hapo.
Hapo mwanzo wakati inaanza tulikuwa tunashirikiana sana Tena nathubutu kusema walinisaidia pia kupata connection kwa baadhi ya viwanda na kwa baadhi ya agents wakubwa wa viwanda.
Urafiki ulikuwa mzuri, Mimi sishindi Sana pale Ila kila nilipoenda lazima nisalimiane nao na kupiga story mbili tatu.
Sasa hivi Hali ni mbaya ni Kama tupo Vitani, Kuna kisa kimoja kilitokea Ila sikuwa najua kama pia inaweza kutufikisha hapa tulipo. Kuna kijana alikuwa kwenye hardware moja ambayo ni kubwa na ya miaka mingi, wakaja kushindana na mwenyewe, yule kijana akaja kuniomba kazi na kiukweli nilikuwa nahitaji kuongeza vijana maana walikuwa wapo wawili hivyo hawakutosha kabisa kutokana na kazi nyingi. Nikampa nafasi, we nilianza kununiwa na yule mzee wa kich......story zikaanza kuisha na kukoma kabisa.
Shughuli kubwa ikaja kwenye mauzo ya cement, Mimi nilipunguza 500 kutoka bei ya kawaida ambayo wengine pale wanauza.
Wakienda kwao hao wakishandana wanakuja kwangu nawauzia kwa kupunguza tena. Mfano; Kama watakuta huko ni 15000, wakija kwangu nawauzia kwa 14500.
Katika kuboresha zaidi biashara nikaona isiwe kesi ni vyema nikanunua gari ili wateja wapate nafuu zaidi kwa kuwa nawatoza bei ndogo kulinganisha na usafiri wa kukodi kwa wengine.
Nikanunua townace(Kaka yake kirikuu), nilinunua mil 11 mkononi lakini bado ilikuwa mpya na katika hali nzuri sana. Kijiweni wakichajiwa 40000, Mimi nawafanyia 30000. Hiyo ndio kazi ya gari, haitumiki kwa shughuli yoyote zaidi ya wateja wa hapa ofisini.
Chuki imekuwa kubwa hadi kwa watu wa kijiweni, eti najifanya mjuaji sana. Na yote hii imepandikizwa na hao wenzangu.
Sio Siri mzunguko wa biashara upo japo bado sijaridhika kwa kuwa eneo la kuhifadhi vitu(store) ni ndogo hivyo labda niwe na pesa nyingi ninunue eneo nijenge store nyingine(sidhani Kama ntaweza kwa kuwa ni ghali sana kumnunua Mtu eneo hilo).
Hakika watu ni wabaya sana, sasa hivi story zimeanza kugeuka kuwa natumia ndumba kijana mdogo, mara mwisho wake sio mzuri.
Hizi naambiwa na vijana wangu, maana wao wanaambiwa na vijana wa hao majirani.
Kuna surprise nimewaandalia hapo ili wateseke zaidi, mteja yoyote kija akanunua vitu kuanzia milioni 1 nampa taa moja ya bure (zile za 5000).
mkubwa Hongera hiyo offer ya Taa moja nimeikubali sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe juha kabisa, unatakiwa kuchomwa moto! Unadhani ni sifa kuongea pumba. Nenda kavunje mlango wa nyumba ya baba yako!
Shida nini mzee acha unoko

Au unataka nije kuiba kwako

Wazee wengine bhana ..mna maneno sana nyie subirini kufa tu kwanza umri ushaenda
 
Back
Top Bottom