Napata sana kiu ya maji wakati wa usiku

longi mapexa

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
3,003
2,000
Kama unaishi Dsm na hili jotoo ni kawaida tu wala usiogope japo ni muhimu kwenda hospitali.
Mimi binafsi kila saa tisa naamka napata maji vikombe viwili.... kisha nasali alafu narudi kulala tena.
Hii hunifanya asubuhi nikojoe mkojo usiokuwa na rangi mbaya wala harufu mbaya.
 

kyemo

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
571
1,000
Sasa hiyo note: ulikua una maanisha nini, kama hutoki jasho si ndiyo sababu pia ya kuwa na mkojo mwingi au uliwazaje, ukiwa sehemu za baridi unakojoa sana ukiwa sehemu za joto hukojoi sana
kutoka jasho ni kwamba unakuwa dehydrated so kiu ya maji inakua kubwa
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
4,068
2,000
Ni kisukari mkuu.Mungu niepushe na ugonjwa huu.Heri kuugua ukimwi kuliko kisukari.
Wacha kujiapiza kijana, sukari na ukimwi ni vitu viwili tafauti. Sukari inaweza kuwa regulated ukiwa na discipline ya kula na kufanya mazoezi.

Sijui nani amekudanganya hivyo
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
4,068
2,000
Unafanyaje mkuu .kuna ndungu yangu kisukari kinanitesa sana ushauri boss
Ni muhimu sana kujua aina ya vyakula vya kutumia ili kuweza kupunguza kiwango cha sukari mwilini. Mfano vyakula vyenye wanga (wali, muhogo, mikate na kadhalika) ni vibaya sana kwa wagonjwa wa sukari. Ukiweza kupunguza ulaji wa vyakula aina hii basi utaweza kupunguza sukari mwilini kwa kiwango kikubwa. Aidha vitu kama pombe, soda pia ni vya kutupa mbali. Mazoezi pia huwa yanapunguza sana kiwango cha sukari kwa vile yanaunguza ile sukari iliyomo mwilini.

Muhimu ni kufuata ushauri unaopewa na daktari basi unaweza kuishi maisha ya amani kabisa. Wengi wetu tunashindwa kufuata ushauri wa daktari na hapo ndipo tunaposhindwa.
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
4,068
2,000
Sukari hairithiwi kinacho rithiwa ni mfumo wa maisha ukifuata mfumo ambao alikua nao mgonjwa wa sukari hasa ulaji na unywaji huenda ikakufika hayo. Jitadhimini juu ya lifestyle na chukua hatua
Sukari inarithiwa kijana, ila mfumo wa maisha ndiyo unaongeza probability ya mtu kupata sukari.

Kuna diabetes type 1 ambayo ndiyo kwa asilimia kubwa inatokana na urithi na unakuta hata watoto wadogo wanayo.

Kuna type 2 ndiyo inayotokana na mfumo wa maisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom