Napata mtoto wangu nikiwa nina miaka 35 huku ramani za maisha bado hazijasoma

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Ninavyozungumza hivi sasa kuna binti tayari ana ujauzito wangu mpaka anakuja kujifungua nitakuwa nina miaka 35 na huyo ndio atakuwa first born wangu na mpaka sasa sijui kama nimewahi au nimechelewa.

Kiukweli ramani zangu za kuhusu maisha bado hazisomi hapa najiwazia mtoto akishazaliwa majukumu mpya.

Hivoo kama una neno la kunishauli uniambie.
 
Nachokushauri ni pambana tu, maisha sio lazima uwe na ramani, kabiliana na lile lilioko mbele yako mpambanie mwanao huko mbeleni atakushukuru sana na kukufaa wakati wa dhiki !
 
Kazi ulizoziona za ajabu na hazina hadhi yako huenda zikawa ndio kimbilio lako maana dogo atakulazimisha kuzipenda
 
Tatizo unataka uishi kama watu wengine. Ishi maisha yako wewe kama wewe. Kama maisha hayataki uwe na mtoto kwa umri ulio nao basi subiri umri sahihi. Ukisikiliza jamii utaanza kuishi kwa presha. Ila huo ndo umri sahihi wa kuwa na watoto. Kila la kheri mkuu.
 
Nakazia
 
Back
Top Bottom