Napata maumivu ya tumbo kila nikimeza hizi dawa

miss chuga

Senior Member
Dec 25, 2019
172
250
Habari za muda huu?

Mimi ni mama kijacho miezi 3.5 nilienda klinic nikapewa hizi dawa zinaitwa FERROUS SULPHATE+ FOLIC ACID, Nikashauriwa kila siku nimeze vidonge 2 Mara moja Ila Cha kushangaza kila nikimeza baada ya nusu saa tumbo linauma sana linavuruga mpaka naharisha Ila siku nisipomeza hata siumwi.

Nikimeza tu tumbo linauma sana sasa nashindwa kuelewa nifanyaje maana naskia hizi dawa ni muhimu kumeza naombeni mnisaidie ushauri nakosea wapi au nifanyaje ili nikitumia nisipate maumivu ya tumbo.
 

TheGreatGenius

Senior Member
Jul 6, 2011
111
250
Nausea (Kichefuchefu) ni side effect ya kawaida kwa wengi wanaotumia Iron Supplements. Mwambie Daktari wako akubadilishie akupe Chelated Iron (Iron integrated with aminoacids) - ambayo haina hizo side effects na inafanya kazi kwa uharaka zaidi japo ni gharama kubwa zaidi
 

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
6,644
2,000
Pole, jaribu kutumia Ferrotone, zina less side effects. Kikubwa zina ingredients za ferrous sulphate na folic acids but zipo in capsules.
 

Lukonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
508
1,000
Moja ya vitu unaweza kufanya na kuzingatia ni:

1: Kumeza kidonge kimoja kila baada ya saa 12 (kidonge kimoja mara mbili kwa siku). Utakua umechukua kiasi kilekile kwa kupunguza kiasi cha dawa kwa wakati mmoja kwenye tumbo.

2: Kuwa makini kwenye matumizi ya vitu vyenye kuleta muwashawasha kwenye njia ya chakula kama: pilipili, tangawizi, matunda mabichi/yenye ukakasi. Hivi kama unavitumia sana vyaweza kuwa chanzo pia.

3: Kama itaendelea kuleta shida, mwone daktari kwa ushauri zaidi ikiwemo kuangalia uwezekano wa brand au form/aina ya mfumo wa dawa (majimaji vs vidonge).
 

miss chuga

Senior Member
Dec 25, 2019
172
250
Nausea (Kichefuchefu) ni side effect ya kawaida kwa wengi wanaotumia Iron Supplements. Mwambie Daktari wako akubadilishie akupe Chelated Iron (Iron integrated with aminoacids) - ambayo haina hizo side effects na inafanya kazi kwa uharaka zaidi japo ni gharama kubwa zaidi
Asante
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom