Napata maumivu ya kifua upande wa kushoto shingo pamoja na mikono yote miwili

Kapime h.pyrol maans hizo ni dalili za vidonda vya tumbo
Asante mkuu nlishawah kupima h pyrol mwaka juzi Nilikutwa nao nikapewa dawa lakin mwaka jana mwezi Wa 12 nilipima tena nikakuta negative
 
Tumia chlorophyl ya edmark. Sio dawa lakini inatoa sumu mwilini, na mauchafu yote. Utakuwa poa. Mi nilihangaika, hii nilitumia tu kutoa sumu, nikashangas nimepona
 
Nenda hospitali ulafanye vipimo viwili vya moyo
1.Echo
2.Ecg

Kuna shida kwenye moyo na hasa inaonekana moyo haupati oxygen ya kutosha, mara nyingi hii hutokana na moyo kutanuka cardiomypath.

Na ukichunguza sana hali hiyo huambatana na kupiga miayo mara nyingi mfululizo na pia kupata shida ya kukaa muda mrefu hasa kwenye safari ndefu.

Nenda kafanye hivi vipimo ndio vina majibu kamili ya tatizo lako.

Ila unatatizo kwenye moyo hii nina hakika nayo kwa 99%
Mkuu hivi mtu mwenye cardiomyopathy.. anasaidikaje hospitali? Yaani dawa gani inaweza tibu au huduma gani inasaidia?
 
Mkuu hivi mtu mwenye cardiomyopathy.. anasaidikaje hospitali? Yaani dawa gani inaweza tibu au huduma gani inasaidia?
Mimi sio mtaalamu sana wa tiba ya moyo.

Ila tiba yake ni kuhakikisha wana i control presha kwa hiyo utapewa dawa za Beta blocker kama Propranolol au Atenol ili ku control Presha.

Ukiweza kui control presha basi tatizo linakuwa limedhibitiwa kwa zaidi ya 90%
Kwa kuwa kuta zile za moyo hazitotanuka tena kwa kuwa presha ya damu itakuwa imekuwa regulated.

NB.
Tatizo hili halitibiki kwa kuwa kuta za moyo zikishatanuka hazirudi tena ila unaweza ku control zisizidi kutanuka kwa ku control presha hadi kuwa normal.
Usisahau kuwa kwa zaidi ya 90% tatizo la cardiomypath husababishwa na shinikizo la juu la damu lisilo dhibitiwa na kuachiwa kwa muda mrefu ambalo hupelekea kuta za moyo kutanuka.
 
Wakuu Habari za mida.

Mimi Nina umri wa miaka 31 nimekua nikiambulia na tatizo la maumivu ya kifua upande wa kushoto. Maumivu hayo pia nayapata kwenye mkono wa kushoto wakati mwingine mkono wa kulia. Inafikia muda shingo inakua inauma muda mwingine inakua kama inakakamaa dizain kama nimekabwa na kitu.

Wakati wa kuamka asubuh nahisi tumboni kama panavuruga sana.. Nimejaribu kwenda hospital ya rufaa ya Bugando Mwanza nikapata vipimo vya moyo.. Daktari bingwa ananiambia haoni tatizo lolote kwenye moyo.. Akaenda mbali ananiambia itakua nasumbuliwa na anxiety disorder. Wakuu napata maumivu sana inafikia hatua nikiongea sana shingo inauma sana mpaka nakua kama naishi wa nguvu nataka kuondoka.

Daktar aliniambia nitumie dawa za ant acid itakua nina acid nyingi tiumbon.. Wakati mwingine kooni nahisi kama kuna kitu kimekwama.. Nateseka nimerudi hospital zaid ya mara kumi. Naombeni ushauri nifanyeje.. Kila nikipi a presha iko normal. Mwili unakua unaishiwa nguvu kabisa..

Asante sana
umeshapata heart attack nenda kwa dr wakakuchunguze usije ukajifia
 
Pole kwa kuumwa.
Kuna mambo ambayo naweza kuyahusisha na maumivu unayopata:
1: Tatizo la moyo
2: Tatizo la tumbo/gastritis
3: Tatizo la pingili za shingo/cervical disc disorders
4: Sternum bone disorders

Hivyo, unahitaji daktari asikilize kwa makini na kupata majibu mengine ya maswali zaidi kuhusu kuumwa kwako, jinsi maumivu yanavyotokea, kazi, vyakula nk.

Hapo ataondoa baadhi ya shida kulingana na maongezi yenu na kubaki nazo chache ambapo ndo ataagiza vipimo kwaajili ya kukanusha au kuthibitisha tatizo halisi.
 
Mkuu pole sana kwa tatizo hilo.

Labda niandike kilichonisaidia mimi.
Kwanza kabisa nilipatwa na dalili kama zakwako nilipokuwa chuo Saut mwaka 2014 na niliteseka sana. Dalili zangu zilikuwa kali mno hadi maumivu yalisambaa hadi kwenye bega na mkono wa kushoto.Mara nyingine yalishuka hadi kwenye miguu na unyayo. Hospitali za bongo niliishia kupewa vitamin b12 na kuambiwa labda ni Acid reflux. Nilikata tamaa sana pale watu waliponimabia labda nimelogwa. Nilifikia mahali nikasema acha tu nikae hivyo. Maumivu yalikuwa mara nyingi yanakuwa makali mfululizo wa siku 5 hadi 6 masaa 24.

Mungu siyo athumani nilipata nafasi ya kuja abroad na ndipo nikaamua kulipa uziti tatizo hilo kwa sababu nina insurance. Nilienda hosiptali nikafanya vipimo mbalimbali kuanzia, full blood profile, glands,ct scan,mri ya kichwa na spine, cadiac stress test, ECG,angiogram,lumbar puncture na nyingine nyingi. Hawakuona chochote. Wakani refer kwa Chiropractor. Basically, Chiropractor aligundua kwamba nina muscle knots mgongoni na pia ribs cartilage zilikuwa zinatatizo wanaita (Costochondritis). Ebana ehh, tukaanza mazoezi ya mgongo, yapo mengi ila kuna hili moja ambalo aliponifanyia tu maumivu yaliondoka within dakika 4. Unalala kwa tumbo (hakikisha umelala sehemu flat, kama vile sakafuni, usilale kwenye godoro) kisha aku crack. Angalia video hii maana ni ngumu kueleza kwa maandaishi. Pia hakikisha unamwambia anaye ku krack afanye hivyo unavyopumua hewa nje.

Pole sana kwa uhandishi wangu, mimi siyo mwandishi mzuri ila natumaini utafaidika na nilichokiandika.
 
Ninayo bro nilipimwa nikakutwa nayo naomba basi namba zako kama unaweza kunishauri au tiba
Sikupata tiba za haraka kwa hospital nikapata za asili kwa bei ya juu
kidogo ila zilisaidia sana, japo ratiba yake n ngumu sana.
And mostly ni hizo ni ulcers za utumbo mdogo au mpana.
 
Sikupata tiba za haraka kwa hospital nikapata za asili kwa bei ya juu
kidogo ila zilisaidia sana, japo ratiba yake n ngumu sana.
And mostly ni hizo ni ulcers za utumbo mdogo au mpana.
Karbu dm huko mapema mana maisha ya bando sio marefu
 
Back
Top Bottom