Napata maumivu ya kende(korodani) ya upande wa kulia

funduku

Senior Member
May 2, 2013
131
36
Habari wana JF,

Naandika kuomba ushauri juu ya hili tatizo la maumivu ya korodani ya upande wa kulia ambalo mara nyingi hunitokea pale ninapokua natembea au kukimbia kwa umbali mrefu. Tatizo hili ni la muda mrefu pia hua linakuja na kupotea.

Pia korodani hua kidogo inavimba na maumivu huongezeka pale ninapokua naishika au kuiminyaminya na wakati mwingine maumivu hupanda mpaka eneo karibu na tumbo kwa chini upande wa kulia.

Asanteni wakuu kwa yeyote mwenye kufahamu hili tatizo naomba ushauri wa jinsi ya kulimaliza, maana naogopa nisije nikashindwa kujenga familia hapo baadae.

Asante
 
mbona dizaini kama mimi sema mimi napata maumivu flani na nikishika pia ila la kushoto na kuna kuwa kama kuna mshipa hiivi una uma
 
Habari wana JF,

Naandika kuomba ushauri juu ya hili tatizo la maumivu ya korodani ya upande wa kulia ambalo mara nyingi hunitokea pale ninapokua natembea au kukimbia kwa umbali mrefu. Tatizo hili ni la muda mrefu pia hua linakuja na kupotea.

Pia korodani hua kidogo inavimba na maumivu huongezeka pale ninapokua naishika au kuiminyaminya na wakati mwingine maumivu hupanda mpaka eneo karibu na tumbo kwa chini upande wa kulia.

Asanteni wakuu kwa yeyote mwenye kufahamu hili tatizo naomba ushauri wa jinsi ya kulimaliza, maana naogopa nisije nikashindwa kujenga familia hapo baadae.

Asante

hiyo itakua epididymorchitis
 
hiyo ni henia na mara nyingi huwa upande wa korodani ya kulia huwa inauma ukitembea na hata ukiishika kwa mkono na huvimba na huwa kubwa zaidi kuliko nyenzie nenda hospitali utapewa dawa na kama ikijirudia wsnakufanyia upasuaji
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom