Napata kikohozi na mafua nikinywa pombe, tatizo nini?

Mzee Shirimaa

JF-Expert Member
Sep 12, 2018
1,539
3,440
Ndugu zangu naomba msaada weekend iliyopita nilipiga pombe sana, ratiba yangu ya kunywa bia ni kuanzia Ijumaa mpka Jumapili ila nimepata tatizo moja weekend iliyopita nilipiga Sana vyombo asubuhi nikaamka nina kikohozi na mafua, nikanywa dawa za kikohozi siku mbili kila kitu kikatulia.

Nilijua ni mafua ya kawaida ila leo kama kawaida nilitaka niendeleze ratiba yangu, nimepiga bia nne kikohozi kikaanza. Je hii nini?? Ni ugonjwa Ninao? Je ni ugonjwa gani huu kuzingua starehe yangu? Au ni maombi ya Bi mkubwa wangu make amekua akipiga vita Mimi kula chombo.

Msaada please
 
Kama ulizoea kunywa za kienyeji basi ondoa hofu ni ushamba tu wa koo lako baada ya kuingizwa mjini na bia hivyo lina shangaa mataa.
 
Ukishajua tatizo nini.....Tafadhali usije kufikiria kuacha bia🍻🍻🍻🍻🍻🍺🍺🍺🍺🍺
 
Kama unakunywa pombe na glasi ya bar, kapime TB fasta.

Usianze kujitetea kwamba wanaosha na maji moto. Kwanza kapime ngwengwe kisha kapime kama umejikwaa kwenye miwaya.
 
Back
Top Bottom