Napata haja kubwa nyeusi na kutapika damu

Capslock

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,066
4,729
Habari zenu, poleni na mihangaiko ya siku.

Naumwa tokea jana. Shida ilianza asubuhi nikawa nahisi tumbo kuuma baadae nilipoenda kujisaidia ile haja ilikuwa nyeusi kama oil chafu, shida nini? Baadae pia nikaanza kutapika damu.

Mwenye uelewe na hili tatizo.
 
Kinyesi chote cheusi au baadhi ya sehemu ya kinyesi ndio nyeusi mkuu ?

Je hunq ugonjwa wowote sugu kama vile cancer n.k ?

Je kinyesi ni Laini au kigumu ?
 
Kinyesi chote cheusi tii kama oil chafu.

Sina ugonjwa wowote sugu.

Kinyesi laini.
Dah mkuu itakuwa una gastrointestinal bleeding(kuvuja damu kwa njia ya mfumo wa chakula)

Yaani kuanzia mdomoni mpaka kwenye anus kuna sehemu hapo ina tatizo la kuvuja damu.

Ila kwa kuwa kinyesi chako chote ni cheusi hii ina maana kuna bleeding katika upper GI track(mfumo wa juu wa mmeng'enyo wa chakula)

Damu itakuwa inavuja kabla ya kufikia katika hatua kuu za uvunjaji wa chakula,hii inapelekea damu kuchanganyika na chakula hivyo chakula kikivunjwa na seli za damu nazo huvunjwa na kupelekea chakula hiko kuchanganyika na damu ambayo imevujwa,hhii inapelekea kinyesi kuwa na rangi nyeusi chote.

Hii ni kwa ufupi tu ila kwa matibabu nenda hospitali ukaelezee tatizo lako utapata huduma za vitendo zaidi.

Usidharau kwenda hospitali mkuu
 
Nashkuru sana kwa ushauri.

Binadamu hana uwezo wa kuvunja seli za damu.

Mamalia mwenye uwezo huo na ambae anaishi kwa kunywa damu za wanyama wenzie ni popo bawa peke yao (Vampire Bats).

Hukuwa makini medical school.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom