Inkoskaz
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 6,372
- 2,374
Tanzania nchi yenye kila rasilmali tunatimiza miaka 50 hatuna umeme kila mahali kelele na moshi wa genset za kichina!
Hatuna maji ya bomba kila mahali mikokoteni ya madumu ya maji na mabowser.nyumba zimeelemewa mapaa kwa uzito wa ma-simtank kama vile hatuna mvua,mito,maziwa nk!
Hakuna shule..wanetu wanaenda kusoma uganda,kenya na malawi.zilizopo ni miradi ya watu na kuwavalisha watoto graduation gowns kwa kuongea kingereza!..aibu
Hatuna hospitali zaidi ya vichaka vya rushwa na store za kuuzia dawa ndo maana wagonjwa hupelekwa appolo.
Mali asili kama wanyama,vivutio mbalimbali mapato yake haijulikani yanaenda wapi!
Dhahabu,almasi,tanzanite,chuma,makaa,nickel,cobalt,uranium,gas nk tunazichimbua na kuwapa na kubaki na mashimo! NASEMA HIVI..HATUHITAJI KUTOA HII DEPOSIT YETU INAYOONGEZEKA THAMANI KILA KUKICHA!
Tufanyeje?
Bandari na reli tu vinaweza hadi kumgawia kila mdanganyika ruzuku kama Libya. Tukiinvest katika reli na kusafirisha train 5 za mizigo kila siku kwa TRC na TAZARA tutaingiza mamilioni ya dola..kumbuka tumezungukwa na land locked countries like malawi,zambia,congo,rwanda and burundi.even sea locked kama comoro na tukawa ndio HUB yao kama Dubai tutaogelea dola!
Tukipanua bandari tukavunja ile soko ya DAGAA MCHELE-maana kamba kochi na jodari wanaishia juu kwa juu,tukavunja hata ikulu ikahamia Msoga na Chamwino mpaka kule kunapouzwa mihogo-coco beach ikawa ni bandari ya kisasa na miundo mbinu ya kileo na mitambo HAKI YA MUNGU tungetisha! Ajira zingekuwa bwerere na uharibifu wa barabara kwa malori ungekoma! Maintanance cost zingepungua!..
Ajali za kizembe za malori used na matairi na parts za kichina tungepunguza hii Misiba ya kila siku.bora ianguke train ya mizigo iliyokatiwa bima na sio maisha ya watz wasio na hatia!
HAKIKA NAWAAMBIA hatuhitaji ushauri wala hata utoke kwa bill gate ama marehemu Steve PJ kwani utafungiwa kabatini!
Tunahitaji watu jasiri wenye kuamua na KUTENDA pasipo woga wala subira.hivi unajua mtz bila kiboko haendi? Daladala zilitengenezewa kiboko kinaitwa Majembe auction zikaanza kunyooka ghafla waziri husika akapiga stop! Mh!
Weka sheria kali na zisimamie zitazaa matunda..eti watagoma. wakale wapi? Watagoma asubuhi tutatembea, tutapanda risk bodaboda na taxi njaa itawauma jioni watarudi barabarani bana. Msimamo muhimu aisee
Wallah nina mengi ya kusema lakini kitochi changu kimeisha chaji na ex rate ya dola kwa tshs 1820 sitarajii kumiliki generator maishani! But msg sent, delivery watajijua