Naondoka nyumbani kwenda kutafuta maisha. Naenda Iringa kwanza, mwenye kazi au connection tafadhali

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
1,457
2,435
Heshima kwenu nyote.

Nimeamua kuanza maisha mapya baada ya kukaa nyumbani kwa muda sasa.

Sina chochote ninachomiliki kama asset na comfort zone imekuwa kikwazo kikubwa sana kwangu kiasi cha kunifanya niwe muoga.

Leo nimeamua kuondoka nyumbani, naelekea Iringa kwanza. Huko ninakoenda sina sehemu maalumu ya kufikia, sina ndugu wala rafiki.

Mwenye kazi yoyote ya halali au anayeweza kunipa connection popote naomba tuwasiliane.

NB: Sina taaluma (proffesion) yoyote nina elimu ya darasa la 7.

Natanguliza shukurani!
 
Bora ungebaki Nyumbani ungeanza kufanya kazi ngumu kama kubeba tofali, viwandani (kibarua) nenda stand kapige debe fanya yote hayo ukiwa nyumbani kwanza ukishapata uzoefu ukishapata chimbo ndo uondoke sasa! unapoenda huko unaweza kufa hivi hivi watu wanakuangalia tu! Na baridi ya Iringa ulale njaa stand hata wiki hautafikisha.

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Bora ungebaki Nyumbani ungeanza kufanya kazi ngumu kama kubeba tofali, viwandani (kibarua) nenda stand kapige debe fanya yote hayo ukiwa nyumbani kwanza ukishapata uzoefu ukishapata chimbo ndo uondoke sasa! unapoenda huko unaweza kufa hivi hivi watu wanakuangalia tu! Na baridi ya Iringa ulale njaa stand hata wiki hautafikisha.
Ushamkatisha tamaa mwenzako.
 
Uamuzi mzuri maana hata mimi niliamua kutoroka nyumbani kuelekea mjini nikiwa sina ndugu wala rafiki wala makazi. Na mfukoni nilikuwa na nauli tu.

Nilifika stendi nikashuka nilibaki na jero mfukoni ikabidi nipige chai kwa wauza chai wale wanaotembeza. na hao ndo wakanipa mchongo na nikaanza kazi ya kutembeza chai na vitumbua.

But leo niko kwangu na nimeoa na nina kazi nzuri tu.

Usikate tamaa mzee kapambane.
 
Million dollars said:
Bora ungebaki Nyumbani ungeanza kufanya kazi ngumu kama kubeba tofali, viwandani (kibarua) nenda stand kapige debe fanya yote hayo ukiwa nyumbani kwanza ukishapata uzoefu ukishapata chimbo ndo uondoke sasa! unapoenda huko unaweza kufa hivi hivi watu wanakuangalia tu! Na baridi ya Iringa ulale njaa stand hata wiki hautafikisha
Mkuu baba yangu ni mkali sana, amekuwa akininyima nafasi ya kufanya chochote au kwenda popote kwa lengo la kumsaidia tu kazi za nyumbani huku nikiwa siijui future yangu.

Yeye ana mifugo, amewahi kunionyesha (kunipa) ya kwangu huku bado nipo kwake.

Mbali na hapo, sina maamuzi ya kufanya juu ya hiyo mifugo aliyonipa na amekuwa akiiuza pia.

Nikijaribu kuhoji kwa nini anauza, anadai kuwa mimi ni mwanae na sina mamlaka ya kumpangia maana yeye ndio aliyenipa hiyo mifugo na ananilisha pia.

Nimechoka kuwa tegemezi huku nikiwa siijui future yangu, bora niende mbali na huyu mzee wangu.
 
Back
Top Bottom