Naona siasa zimehamia misikitini na makanisani

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
918
1,401
Kumekuwa na jitihada kubwa sana kwa viongozi wa kisiasa kuingia makanisani na misikitini kuhubiri siasa, huku wakitoa rushwa ya mamilioni ya hela kwa mgongo wa sadaka na misaada, hili jambo linahitaji kukemewa sana , makanisani na misikiti ni maeneo ambayo ni muhimu kwa kuwajenga watu kiroho ili waweze kumuelekea Mwenyezi Mungu, na wala si maeneo ya kwenda kujijenga kisiasa.

Kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 ,kuna kiongozi mmoja wa kisiasa alipita sana makanisani na misikitini, huku akitoa misaada, jambo hilo lili geuka na kuwa shubiri kwa chama Fulani cha siasa , viongozi wa chama hicho wali piga kelele sana na kulaani kitendo cha kiongozi huyo.

Leo tuna waona wale waliokuwa kuwa waki kemea jambo hilo ndio wanao ongozana kila siku kwa kupishana ndani ya taasisi hizo huku wakitoa matamko mbali mbali ya kisiasa na kutoa rushwa kwa mgongo wa misaada na sadaka.

Wito kwa viongozi wetu wa dini kuweni makini sana na hiyo misaada, kwani itafika wakati wa hao viongozi kufanya maovu na mkashindwa kuwa kemea.
 
Wanasiasa wa upinzani wamedhibitiwa sana. Daima huwezi kuzuia maji ama hewa kwa vidole,lazima itapenya.
 
Back
Top Bottom