kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 14,112
- 15,990
Naona hii tabia ya kutetea wanaokosea na zikichukuliwa hatua stahili.,
Wapo mapuruzai kibao wanajitokeza kutetea utopolo wa huyo mkosaji.
Tumeshuhudia hapa mafisadi, watakatisha pesa, wauza madawa, yule mwandishi wote hawa walipata watetezi kwa makusudi kwa makusudi kutaka kuonyesha kama wanamkomoa mtu kumbe wanazidi kuchochea moto
Hivi sasa kuna mmoja kafanya kosa la kucheka picha ya Rais bado kuna watu badala ya kujaribu kutoa rai kumshauri kijana asirudie makosa, kuna watu wanataka kufanya kama hakufanya kosa
Kama hakudhamiria kwanini hakuchukua picha ya mzazi wake wa kike au kiume akaanza kucheka. lakini kwa kuchukua picha na kuanza kuidhihaki hapo ametumbukiza mguu wenye kiatu kwenye sufuria la ubwabwa lazima awatambue wenye shughuli ili kesho asirudie tena afunzwe sana!
Mtoto hakanywi akienda hukanywa akisharudi wakati yameshamkuta ya kumkuta!
Bakora haichagui pa kutua kwa mtoto mtukutu!