Naona Rais Magufuli anataka kufuta kabisa ajira zisizo rasmi nchini | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naona Rais Magufuli anataka kufuta kabisa ajira zisizo rasmi nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by stellahthatcher, Jul 17, 2017.

 1. stellahthatcher

  stellahthatcher Senior Member

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 14, 2015
  Messages: 169
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Serikali yake inafanya kila njia kudisturb atmosphere ya watu waliojiajiri ktk sekta isiyo rasmi. Wamachinga, wauza mkaa, wachoma mahindi, bodaboda, Shoe shiners, waosha magari, madobi etc ni watu wanaopita kipindi kigumu sana ktk utawala huu.

  Serikali imepiga marufuku kuosha magari maeneo ambayo si rasmi kwa ajili ya shughuli hizo. Yani kuanzia sasa ukikutwa unaosha gari eneo ambalo sio car wash unatozwa faini ya TZS 50,000/=. Pamoja na sababu za uchafuzi wa mazingira zilizotolewa, pia serikali imeeleza "issue" ya mapato. Kwamba hawa wanaoosha magari mitaani hawalipi kodi, biashara zao hazijasajiliwa, hawana leseni, wanaipotezea serikali mapato.

  Serikali inaamini magari yote yakioshwa kwenye maeneo maalumu ya kuoshea magari "car wash" zitapata mapato makubwa na kulipa kodi kubwa serikalini. Hii ni habari njema kwa wamiliki wa "Car Wash" na kwa serikali pia. Lakini ni habari mbaya sana kwa vijana waliokua wamejiajiri kwenye biashara hii na ni habari mbaya pia kwa wamiliki wa magari.

  Kwa upande wa ajira naona maelfu ya vijana wakipoteza ajira zao. Hawa wanalazimishwa kwenda kuwa wahalifu. Vijana hawa walikua wanapatikana zaidi maeneo ya mahotelini, Club, bar, au kumbi za starehe. Ukienda pale Seashells Hotel, Rombo Greenview hotel, Coco Beach, au B-Bar Sinza kwenye kitimoto, ukipaki gari yako nje anakuja kijana anakuuliza akuoshee? Ukikubali anakuoshea wakati wewe ukiendelea na shughuli zako nyingine. Ukimaliza unakuta gari tayari.

  Hii ni fursa ya ajira ambayo vijana waliiona. Na gharama zao zilikua nafuu. Ukipeleka gari "Car wash" ni 15,000/= lakini ukiosha kwa vijana hawa ni 3,000/= tu na gari inang'aa. Wana vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kazi hiyo. Kuna vijana walikua wanaosha hadi magari 20 kwa siku, maana yake walikua wanatengeneza karibu 60,000/= kila siku. Kupitia pesa hizo wanalipa kodi ya nyumba, wanasomesha watoto, wanavaa, wanakula etc. Sasa leo wamepigwa marufuku waende wapi?

  Serika inasema vijana hawa hawalipi kodi na hivyo kuipotezea serikali mapato. Ukweli ni kwamba hawakupaswa kulipa kodi ktk mfumo rasmi (direct tax) kwa sababu wao ni sekta isiyo rasmi. Duniani popote kuna ajira rasmi na ajira zisizo rasmi. Waliopo kwenye ajira rasmi hulipa "direct tax" lakini waliopo kwenye ajira zisizo rasmi hulipa "indirect tax" kutokana na vipato vyao.

  Watu kama wachoma mahindi, waosha magari, waziba pancha, mafundi viatu, hawawezi kulipa kodi directly TRA zaidi ya ushuru mdogo wanaotozwa na Halmashauri husika. Hawa ni tabaka la chini ambalo hutakiwi kuwadisturb. Waache watalipa kodi indirectly kupitia bidhaa watakazonunua.

  Muosha magari akiosha magari 10 kwa siku akapata 30,000/= atanunua sukari kupeleka nyumbani tayari amelipa kodi, atanunua nguo tayari kalipa nauli, atalipia umeme tayari kalipa kodi. Sasa kwanini tumlazimishe alipe direct tax TRA? Maana yake ni kwamba wachona mahindi nao waanze kutafuta leseni TRA, wanaobrush viatu nao waanze kusumbuliwa na TRA, waziba pancha nao, makonda wa daladala, bodaboda, wachoma mkaa. Hii si sawa. Hakuna mahali popote duniani wanakofanya upuuzi wa aina hii.

  Nenda hapo Kenya uone walivyo smart kwenye issue ya kodi na namna wanavyotambua sekta rasmi na zisizo rasmi. Pale Fort Jesus, Mombasa kwa nje kuna "Tour Guides" ambao hawajasomea popote. Ni wazee wa kiarabu waliokulia maeneo yale na wanafahamu historia ya ngome hiyo si kwa kusoma bali kwa kuona na kuhadithiwa. Wazee hawa wanafahamu mengi kuliko Tour Guides waliosomea darasani maana wao ni wazawa wa eneo lile.

  Wazee hawa waneamua kujiajiri wenyewe (sekta isiyo rasmi) kwa kuelekeza wageni. Serikali ya Kenya haiwasumbui wala kuwatoza kodi. Inajua watalipa kodi indirectly kupitia bidhaa watakazonunua. Lakini hapa kwetu tunataka hadi bodaboda walipe kodi, hadi wanaotembeza magazeti, na wanaobrush viatu. Tuwasajili TRA tuwape TIN number. Huu ni Wendawazimu.!

  Labda nieleze kwa kifupi madhara ya uamuzi huu wa "kukurupuka" wa serikali kufukuza vijana hawa wanaoosha magari maeneo yasiyo rasmi;

  #Mosi; Kuongezeka kwa wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana (Unemployment rate). Hali hii itafanya ugumu wa maisha kuongezeka, maana si kila muosha magari ataweza kutafuta fursa nyingine au shughuli nyingine ya kufanya. Ukosefu wa ajira ukiwa kwa kiwango kikubwa means hali ya maendeleo ya nchi itadumaa. Ukumbuke moja ya factor zinazopima maendeleo ya nchi ni pamoja na ajira.

  #Pili; mzunguko wa pesa kuzidi kuwa mdogo ktk jamii, na hivyo kusababisha mdororo wa uchumi. Mtu aliyekua anapata 30,000/= kwa siku akatumia kwa mahitaji mbalimbali ya nyumbani kwake means alikua anasaidia pesa kuzunguka. Just imagine kwa Dar peke yake kuna vijana 10,000 waliojiajiri kwenye shughuli hiyo. Kama vijana hao wanapata atleast 30,000/= kwa siku, ni jumla ya TZS milioni 300. Yani kuna TZS Milioni 300 zilikua zinazunguka kila siku kutoka kwa wamiliki wa magari kwenda kwa waosha magari, kutoka kwa waosha magari kwenda madukani, kwenda TANESCO kulipia luku, kwenda Dawasco kulipia maji, kwenda mashuleni kulipia ada etc.

  Lakini kuanzia sasa hiyo circulation imekufa rasmi. Yani pesa zitakuwepo lakini si katika mzunguko huo tena. That means kuna watoto watashindwa kulipiwa ada, kuna watu watashindwa kulipa kodi ya pango, etc. Hii itasababisha pesa kuadimika sana mtaani (intensive scarcity of money) kitu ambacho ni kiashira cha mdororo wa uchumi. Pesa inapaswa kuadimika lakini si kuadimika sana (Scarce but not very scarce).

  #Tatu; Kuongezeka kwa vitendo vya Uhalifu. Kumbuka kundi kubwa la watu waliokua wakifanya shughuli hii ni vijana ambao wengi wao wana nguvu. Hawa hawawezi kukaa "idle". Baadhi yao watatafuta shughuli za kufanya lakini wengine watajiingiza kwenye vitendo vya kihalifu ili kukabiliana na ugumu wa maisha. Hapa serikali inatengeneza bomu ambalo kulipuka kwake ni hatari kubwa kwa jamii. Tutegemee kusikia vikundi vya "Panya Road" "Watoto wa mbwa mwitu" etc vikijirudia.

  #Nne; Kuongezeka kwa tabaka kati ya wenye nacho na wasiokua nacho.

  #Tano; Kuongezeka kwa hali ya Uchafu unaosababishwa na magari mengi kutokuoshwa kwa muda mrefu. Kuanzia sasa kukutana na gari chafu itakua jambo la kawaida. Mtu aliyekua anaosha gari yake kila siku ataosha mara moja kwa wiki. Kwanza hatakua na muda wa kutosha kwenda Car wash kila siku. Mtu anatika kazini saa 12 jioni, anamua kupitia mahali apate chakula hapohapo anaosha na gari yake. Sasa hivi ni ngumu. Pili gharama anayolipa "Car Wash" kwa siku moja, alikua anaitumia kuosha kwa vijana wa mtaani wiki nzima.

  #Sita; Kudorora kwa shughuli nyingi za maendeleo kutokana na watu kupoteza muda. Watu wengi walikua wakitumia muda wa kuosha magari kufanya shughuli nyingine. Una kikao na mtu pale Regency Hotel, unaenda kukutana nae wakati mnaongea gari yako inaendelea kuoshwa. Mkimaliza kikao na gari imeng'ara. Lakini kuanzia sasa watu watalazimishwa kupoteza muda. Uende car wash masaa mawili ukitoka ndo uende Regency kwenye appointment. Kupoteza muda bila sababu.

  Nadhani serikali inapaswa kutizama upya utaratibu huu. Sina tatizo na wamiliki wa "Car Wash." Hoja yangu ni kwamba watu wasilazimishwe kwenda "Car Wash." kuosha magari yao. Kwanza hazitoshi. Takwinu zinaonesha Dar ina magari zaidi ya laki 9, lakini Car wash zote Dar hazifiki 100. Hii ina maana ili kila gari ioshwe inatakiwa Car wash moja ihudumie magari 900 kwa siku. Nani anaweza??

  So tusilazimishe watu kwenda Car Wash. Anayeweza kwenda aende, asiyeweza aoshe gari yake kwa utaratibu mwingine anaoona inafaa ikiwemo kuruhusu hawa vijana waliokua wakiosha maeneo yasiyo rasmi, kuendelea na shughuli zao.

  Ameandika Godlisten Malisa.
   
 2. k

  konyola JF-Expert Member

  #81
  Jul 18, 2017
  Joined: Dec 13, 2016
  Messages: 739
  Likes Received: 876
  Trophy Points: 180
  Itafika hatua ukienda kuji-help toilet uwe na EFD vinginevyo tuonane 2020
   
 3. k

  konyola JF-Expert Member

  #82
  Jul 18, 2017
  Joined: Dec 13, 2016
  Messages: 739
  Likes Received: 876
  Trophy Points: 180
  Huyu sio chaguo la Mungu bali ni chaguo la mungu
   
 4. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #83
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 13,651
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri. Ila kwa uwepo wa asilimia kubwa ya watanzania kutokuwa na anuani za makazi, ni vigumu kutekelezeka. Kwa wenzetu, mfano Marekani na nchi kadhaa za Ulaya, wana utaratibu wa kujaza tax returns forms kila mwisho wa mwaka. Mtu unajaza mapato yako yote ya mwaka na kuyalipia kodi. Usipofanya, utakamatika tu kwani serikali inafahamu unapoishi. Labda uhame nchi moja kwa moja. Gharama za kuhama nchi na kwenda kuanzisha makazi mapya zitakufanye ulipe tu kodi.

  Sasa hapa kwetu, hao vijana utawapataje wasipolipa kodi? Ukisema serikali iwatafute mmoja mmoja, gharama za kuwatafuta zinaweza kuzidi kodi itakayokusanywa. Ni kwa watu vichaa na wehu tu ndiyo wanaweza kufanya hivyo. Kama kichaa na mwehu Bashite anavyotaka kufanya: ati msako wa wasio na ajira rasmi! Gharama za hiyo misako sijui nani atalipia!! Najua ni serikali ndiyo italipia. Hivi huko serikali hakuna hata mwenye akili ya kindergarten?

  Nimeshawahi kusema humu, ili kuwa na ukusanyaji wa kodi wa uhakika, ni lazima upangaji wa miji na makazi yetu uboreshwe. Hadi mwaka jana, ni asilimia 15 tu ya ardhi ya Tanzania ilikuwa imepimwa!! Na sijaona nia ya serikali kubadili hali hii! Ndiyo maana siyo ajabu kuwa na waziri wa ardhi anayekaa eneo ambalo halijapimwa!!
   
 5. edu88

  edu88 JF-Expert Member

  #84
  Jul 18, 2017
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 707
  Likes Received: 506
  Trophy Points: 180
  Bila kuja na juhudi kama hizi, sekta isiyo rasmi itaendelea kuwa sio rasmi. Lazima mambo yakae vizuri ili kwanza waosha magari wajulikane na walipe kodi kulingana na kipato chao. Hii ni sheria na jitihada ya kuongeza tax base. Ushauri kwako Malisa, tumia lugha ya staha au kuwa professional unapotoa hoja zako, matumizi ya maneno kama "upuuzi" kwenye hoja zako zinakuondolea credibility kabisa na kuharibu mawasiliano. Ndio maana mnaonekana ni wapinzani tu mliozoea kupinga kila kitu. Hebu badilikeni. We ni kijana na umesoma, kuwa mfano.

  Sent from my HUAWEI CUN-L21 using JamiiForums mobile app
   
 6. zee Don

  zee Don JF-Expert Member

  #85
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 31, 2016
  Messages: 473
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 80
  Kuna watu wanataka jua atawale milele

  sent from my iPhone 6
   
 7. c

  chikundi JF-Expert Member

  #86
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 8,222
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Anamaanisha direct tax sio vat ya kununua soda

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 8. c

  chikundi JF-Expert Member

  #87
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 8,222
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Wajiajiri Kwa kutiririsha maji machafu mijini?

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 9. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #88
  Jul 18, 2017
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,617
  Likes Received: 1,439
  Trophy Points: 280
  Mwenye mshahara wa sh.laki tano kwenye ajira rasm analipa takribani elfu hamsini kwa mwezi, huyu mwosha magari anaye pata milioni na zaidi asilipe????,......... indirect tax hakuna asiye lipa.
   
 10. Manjagata

  Manjagata JF-Expert Member

  #89
  Jul 18, 2017
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 4,276
  Likes Received: 1,814
  Trophy Points: 280
  Mkuu utaratibu uko hivi,, tukikuta gari lako linang'aa tunakuomba risiti ya EFD ukikosa maanake umekaribisha faini ya elfu 50. Tunataka magari yote yaoge kwenye car wash!! AKILI ZA PIMBI HIZI!!
   
 11. Ms.Lincoln

  Ms.Lincoln JF-Expert Member

  #90
  Jul 18, 2017
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 8,577
  Likes Received: 7,316
  Trophy Points: 280
  Sijui kwa nini huwa najiuliza shule yao imekaaje...lakini basi.Mama ntilie wajiandae.
   
 12. Ngushi

  Ngushi JF-Expert Member

  #91
  Jul 18, 2017
  Joined: Jul 8, 2016
  Messages: 6,831
  Likes Received: 12,810
  Trophy Points: 280
  [
   
 13. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #92
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,240
  Likes Received: 3,602
  Trophy Points: 280
  Serikali ndio inapaswa kuwezesha/kutengeneza mazingira watu kulipa hiyo direct tax. Sasa hivi biashara zinavurugwa kweli kweli sijui mwisho wake nini!
   
 14. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #93
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,240
  Likes Received: 3,602
  Trophy Points: 280
  Hata wale wanaotumia mobile machine zisizotiririsha maji hawatakiwi!
   
 15. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #94
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,240
  Likes Received: 3,602
  Trophy Points: 280
  Mamantilie wanaingizwa kwenye mfumo wa kulipa kodi! Serikali imedai itawapa vitambulisho maalum pamoja na wauza machungwa!
   
 16. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #95
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,240
  Likes Received: 3,602
  Trophy Points: 280
  Hata maneno kama "wajinga na wapumbavu" kutoka kinywani mwa Rais mstaafu wa awamu ya tatu una tatizo nayo?
   
 17. Isanga family

  Isanga family JF-Expert Member

  #96
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 25, 2015
  Messages: 5,520
  Likes Received: 4,758
  Trophy Points: 280
  Uchambuzi mzuri sanaa kwa kweli bongo ni shida juu ya shida...watu wanatafutiwa shida ili maisha yawe magumu kwao ni Nchi gani utakuta wote ni wasomi na wameajiriwa serikalini...
   
 18. B

  Boss Mdogo Member

  #97
  Jul 18, 2017
  Joined: Jul 14, 2017
  Messages: 52
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 25
  Alisema watu wataishi kama mashetani na watalimia Meno, Anatekeleza Ahadi yake, Inabd muandamani kumpongeza kwa kulinda kodi ya nchi isiishie vichocholoni!

  Akili zikakaa vzr tutaelewa tu!

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 19. hazole1

  hazole1 JF-Expert Member

  #98
  Jul 18, 2017
  Joined: Jan 3, 2015
  Messages: 4,113
  Likes Received: 3,327
  Trophy Points: 280
  Muheshimiwa alisema atakaye bakia mjini hadi mwezi wa 7 huyo mwanaume.

  Baada ya plani yake ya kwanza kufail naona saizi amekuja na plan B.

  Sent from my E6883 using JamiiForums mobile app
   
 20. edu88

  edu88 JF-Expert Member

  #99
  Jul 18, 2017
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 707
  Likes Received: 506
  Trophy Points: 180
  Tofautisha kati ya huyu Malisa anayetaka kuishawishi serikali na Raisi mstaafu aliyetoa kebehi kwa wapinzani. Kama una akili utanielewa.

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 21. rr3

  rr3 JF-Expert Member

  #100
  Jul 18, 2017
  Joined: Mar 19, 2015
  Messages: 2,028
  Likes Received: 1,696
  Trophy Points: 280
  Kabla ya uchaguzi nadhani clip ilivuja...akasema akichukua ...tutalimia meno.....
  nadhani wengi hawakuilewa kauli hiyo.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...