Naona Rais Magufuli anataka kufuta kabisa ajira zisizo rasmi nchini | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naona Rais Magufuli anataka kufuta kabisa ajira zisizo rasmi nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by stellahthatcher, Jul 17, 2017.

 1. stellahthatcher

  stellahthatcher Senior Member

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 14, 2015
  Messages: 169
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Serikali yake inafanya kila njia kudisturb atmosphere ya watu waliojiajiri ktk sekta isiyo rasmi. Wamachinga, wauza mkaa, wachoma mahindi, bodaboda, Shoe shiners, waosha magari, madobi etc ni watu wanaopita kipindi kigumu sana ktk utawala huu.

  Serikali imepiga marufuku kuosha magari maeneo ambayo si rasmi kwa ajili ya shughuli hizo. Yani kuanzia sasa ukikutwa unaosha gari eneo ambalo sio car wash unatozwa faini ya TZS 50,000/=. Pamoja na sababu za uchafuzi wa mazingira zilizotolewa, pia serikali imeeleza "issue" ya mapato. Kwamba hawa wanaoosha magari mitaani hawalipi kodi, biashara zao hazijasajiliwa, hawana leseni, wanaipotezea serikali mapato.

  Serikali inaamini magari yote yakioshwa kwenye maeneo maalumu ya kuoshea magari "car wash" zitapata mapato makubwa na kulipa kodi kubwa serikalini. Hii ni habari njema kwa wamiliki wa "Car Wash" na kwa serikali pia. Lakini ni habari mbaya sana kwa vijana waliokua wamejiajiri kwenye biashara hii na ni habari mbaya pia kwa wamiliki wa magari.

  Kwa upande wa ajira naona maelfu ya vijana wakipoteza ajira zao. Hawa wanalazimishwa kwenda kuwa wahalifu. Vijana hawa walikua wanapatikana zaidi maeneo ya mahotelini, Club, bar, au kumbi za starehe. Ukienda pale Seashells Hotel, Rombo Greenview hotel, Coco Beach, au B-Bar Sinza kwenye kitimoto, ukipaki gari yako nje anakuja kijana anakuuliza akuoshee? Ukikubali anakuoshea wakati wewe ukiendelea na shughuli zako nyingine. Ukimaliza unakuta gari tayari.

  Hii ni fursa ya ajira ambayo vijana waliiona. Na gharama zao zilikua nafuu. Ukipeleka gari "Car wash" ni 15,000/= lakini ukiosha kwa vijana hawa ni 3,000/= tu na gari inang'aa. Wana vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kazi hiyo. Kuna vijana walikua wanaosha hadi magari 20 kwa siku, maana yake walikua wanatengeneza karibu 60,000/= kila siku. Kupitia pesa hizo wanalipa kodi ya nyumba, wanasomesha watoto, wanavaa, wanakula etc. Sasa leo wamepigwa marufuku waende wapi?

  Serika inasema vijana hawa hawalipi kodi na hivyo kuipotezea serikali mapato. Ukweli ni kwamba hawakupaswa kulipa kodi ktk mfumo rasmi (direct tax) kwa sababu wao ni sekta isiyo rasmi. Duniani popote kuna ajira rasmi na ajira zisizo rasmi. Waliopo kwenye ajira rasmi hulipa "direct tax" lakini waliopo kwenye ajira zisizo rasmi hulipa "indirect tax" kutokana na vipato vyao.

  Watu kama wachoma mahindi, waosha magari, waziba pancha, mafundi viatu, hawawezi kulipa kodi directly TRA zaidi ya ushuru mdogo wanaotozwa na Halmashauri husika. Hawa ni tabaka la chini ambalo hutakiwi kuwadisturb. Waache watalipa kodi indirectly kupitia bidhaa watakazonunua.

  Muosha magari akiosha magari 10 kwa siku akapata 30,000/= atanunua sukari kupeleka nyumbani tayari amelipa kodi, atanunua nguo tayari kalipa nauli, atalipia umeme tayari kalipa kodi. Sasa kwanini tumlazimishe alipe direct tax TRA? Maana yake ni kwamba wachona mahindi nao waanze kutafuta leseni TRA, wanaobrush viatu nao waanze kusumbuliwa na TRA, waziba pancha nao, makonda wa daladala, bodaboda, wachoma mkaa. Hii si sawa. Hakuna mahali popote duniani wanakofanya upuuzi wa aina hii.

  Nenda hapo Kenya uone walivyo smart kwenye issue ya kodi na namna wanavyotambua sekta rasmi na zisizo rasmi. Pale Fort Jesus, Mombasa kwa nje kuna "Tour Guides" ambao hawajasomea popote. Ni wazee wa kiarabu waliokulia maeneo yale na wanafahamu historia ya ngome hiyo si kwa kusoma bali kwa kuona na kuhadithiwa. Wazee hawa wanafahamu mengi kuliko Tour Guides waliosomea darasani maana wao ni wazawa wa eneo lile.

  Wazee hawa waneamua kujiajiri wenyewe (sekta isiyo rasmi) kwa kuelekeza wageni. Serikali ya Kenya haiwasumbui wala kuwatoza kodi. Inajua watalipa kodi indirectly kupitia bidhaa watakazonunua. Lakini hapa kwetu tunataka hadi bodaboda walipe kodi, hadi wanaotembeza magazeti, na wanaobrush viatu. Tuwasajili TRA tuwape TIN number. Huu ni Wendawazimu.!

  Labda nieleze kwa kifupi madhara ya uamuzi huu wa "kukurupuka" wa serikali kufukuza vijana hawa wanaoosha magari maeneo yasiyo rasmi;

  #Mosi; Kuongezeka kwa wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana (Unemployment rate). Hali hii itafanya ugumu wa maisha kuongezeka, maana si kila muosha magari ataweza kutafuta fursa nyingine au shughuli nyingine ya kufanya. Ukosefu wa ajira ukiwa kwa kiwango kikubwa means hali ya maendeleo ya nchi itadumaa. Ukumbuke moja ya factor zinazopima maendeleo ya nchi ni pamoja na ajira.

  #Pili; mzunguko wa pesa kuzidi kuwa mdogo ktk jamii, na hivyo kusababisha mdororo wa uchumi. Mtu aliyekua anapata 30,000/= kwa siku akatumia kwa mahitaji mbalimbali ya nyumbani kwake means alikua anasaidia pesa kuzunguka. Just imagine kwa Dar peke yake kuna vijana 10,000 waliojiajiri kwenye shughuli hiyo. Kama vijana hao wanapata atleast 30,000/= kwa siku, ni jumla ya TZS milioni 300. Yani kuna TZS Milioni 300 zilikua zinazunguka kila siku kutoka kwa wamiliki wa magari kwenda kwa waosha magari, kutoka kwa waosha magari kwenda madukani, kwenda TANESCO kulipia luku, kwenda Dawasco kulipia maji, kwenda mashuleni kulipia ada etc.

  Lakini kuanzia sasa hiyo circulation imekufa rasmi. Yani pesa zitakuwepo lakini si katika mzunguko huo tena. That means kuna watoto watashindwa kulipiwa ada, kuna watu watashindwa kulipa kodi ya pango, etc. Hii itasababisha pesa kuadimika sana mtaani (intensive scarcity of money) kitu ambacho ni kiashira cha mdororo wa uchumi. Pesa inapaswa kuadimika lakini si kuadimika sana (Scarce but not very scarce).

  #Tatu; Kuongezeka kwa vitendo vya Uhalifu. Kumbuka kundi kubwa la watu waliokua wakifanya shughuli hii ni vijana ambao wengi wao wana nguvu. Hawa hawawezi kukaa "idle". Baadhi yao watatafuta shughuli za kufanya lakini wengine watajiingiza kwenye vitendo vya kihalifu ili kukabiliana na ugumu wa maisha. Hapa serikali inatengeneza bomu ambalo kulipuka kwake ni hatari kubwa kwa jamii. Tutegemee kusikia vikundi vya "Panya Road" "Watoto wa mbwa mwitu" etc vikijirudia.

  #Nne; Kuongezeka kwa tabaka kati ya wenye nacho na wasiokua nacho.

  #Tano; Kuongezeka kwa hali ya Uchafu unaosababishwa na magari mengi kutokuoshwa kwa muda mrefu. Kuanzia sasa kukutana na gari chafu itakua jambo la kawaida. Mtu aliyekua anaosha gari yake kila siku ataosha mara moja kwa wiki. Kwanza hatakua na muda wa kutosha kwenda Car wash kila siku. Mtu anatika kazini saa 12 jioni, anamua kupitia mahali apate chakula hapohapo anaosha na gari yake. Sasa hivi ni ngumu. Pili gharama anayolipa "Car Wash" kwa siku moja, alikua anaitumia kuosha kwa vijana wa mtaani wiki nzima.

  #Sita; Kudorora kwa shughuli nyingi za maendeleo kutokana na watu kupoteza muda. Watu wengi walikua wakitumia muda wa kuosha magari kufanya shughuli nyingine. Una kikao na mtu pale Regency Hotel, unaenda kukutana nae wakati mnaongea gari yako inaendelea kuoshwa. Mkimaliza kikao na gari imeng'ara. Lakini kuanzia sasa watu watalazimishwa kupoteza muda. Uende car wash masaa mawili ukitoka ndo uende Regency kwenye appointment. Kupoteza muda bila sababu.

  Nadhani serikali inapaswa kutizama upya utaratibu huu. Sina tatizo na wamiliki wa "Car Wash." Hoja yangu ni kwamba watu wasilazimishwe kwenda "Car Wash." kuosha magari yao. Kwanza hazitoshi. Takwinu zinaonesha Dar ina magari zaidi ya laki 9, lakini Car wash zote Dar hazifiki 100. Hii ina maana ili kila gari ioshwe inatakiwa Car wash moja ihudumie magari 900 kwa siku. Nani anaweza??

  So tusilazimishe watu kwenda Car Wash. Anayeweza kwenda aende, asiyeweza aoshe gari yake kwa utaratibu mwingine anaoona inafaa ikiwemo kuruhusu hawa vijana waliokua wakiosha maeneo yasiyo rasmi, kuendelea na shughuli zao.

  Ameandika Godlisten Malisa.
   
 2. wambagusta

  wambagusta JF-Expert Member

  #61
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 28, 2014
  Messages: 1,728
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Tatizo LA watanzania wengi atujatembea kutembea kwetu mikoani khebu tujaribu kutoka nchi za nje kuhusu hili LA car wash na pancha kuchukuwa kodi TRA wapo sahihi kabisa nchi za huku ng'ambo mambo hayo ya car wash bubu hamna pia kuhusu ilo la fundi viatu machinga nk unatudanganya mkuu acha kutumika
   
 3. d

  don xxx JF-Expert Member

  #62
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 14, 2013
  Messages: 1,116
  Likes Received: 898
  Trophy Points: 280
  Well said
   
 4. M

  Mlakon Member

  #63
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 5, 2017
  Messages: 68
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 25
  Ujumbe umewafikia.
   
 5. Prince Kunta

  Prince Kunta JF-Expert Member

  #64
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 27, 2014
  Messages: 9,084
  Likes Received: 7,309
  Trophy Points: 280
  Je, hili bandiko lingeandikwa na Lizaboni?
   
 6. S

  Sexless JF-Expert Member

  #65
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 11, 2017
  Messages: 3,693
  Likes Received: 5,741
  Trophy Points: 280
  Anataka jiji la Dar lifanane na Chatto.
   
 7. Wonderful

  Wonderful JF-Expert Member

  #66
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 8, 2015
  Messages: 7,495
  Likes Received: 5,206
  Trophy Points: 280
  Ok ebu tusaidie,Jee waweke post sehemu gani labda???
  Nadhani ni njema kama ungesema mnazi mmoja pale.
   
 8. N

  Nyanjomigire JF-Expert Member

  #67
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 28, 2013
  Messages: 1,612
  Likes Received: 1,067
  Trophy Points: 280
  Kama sera ya viwanda ingekuwa reality, changamoto kama hizi ni wazi zingepungua sana. Halmashauri ya jiji ndo lenye jukumu la kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli mbali mbali.

  Sasa pale ambapo hawajatenga hayo maeneo, je nani alaumiwe? Viwanja vyote waliuzia madalali (Speculators), sasa vijana waoshee magari wapi???
   
 9. data

  data JF-Expert Member

  #68
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 17,690
  Likes Received: 7,608
  Trophy Points: 280
  Huwezi kuwaona ccm hapa
   
 10. GJHariohay

  GJHariohay JF-Expert Member

  #69
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 24, 2013
  Messages: 1,008
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Rais wa wanyonge. Wanyonge babaa umewapatia, jenga chato yako

  Sent from my Infinix HOT 4 using JamiiForums mobile app
   
 11. utandu

  utandu JF-Expert Member

  #70
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 6, 2014
  Messages: 1,465
  Likes Received: 2,138
  Trophy Points: 280
  Mfumo rasmi wenyewe kwa sasa majanga matupu sijui jamaa anataka tujue nini maana hali mbaya mbaya kupita Maelezo
   
 12. TEAM VIBAJAJI

  TEAM VIBAJAJI JF-Expert Member

  #71
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 9, 2016
  Messages: 1,424
  Likes Received: 1,590
  Trophy Points: 280
  Jamani hivi zile namba tulizokua tukiziimba mlikua bado hamjazijua tu
   
 13. B

  Bazilio JF-Expert Member

  #72
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 1, 2017
  Messages: 632
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80
  Lisu kesha jua kosa la boss wake
  Hivo anatanguliza salam baadae aje na kusema siniwaambia mmeona yupo mahakamani

  Sent from my GT-I9500 using JamiiForums mobile app
   
 14. Brodre

  Brodre JF-Expert Member

  #73
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 2,115
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  Tatizo la hao waosha magari ni moja ukiwakatalia tu wasioshe gari lao fahamu ukirudi kama hautakuta sidemirror imeondoka basi jua hamna indicator kwenye gari yako
   
 15. Nyanya mbichi

  Nyanya mbichi JF-Expert Member

  #74
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 3,587
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
 16. A

  Allineando JF-Expert Member

  #75
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 7, 2016
  Messages: 1,702
  Likes Received: 803
  Trophy Points: 280
 17. Nyanya mbichi

  Nyanya mbichi JF-Expert Member

  #76
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 3,587
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
 18. Nyanya mbichi

  Nyanya mbichi JF-Expert Member

  #77
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 3,587
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
 19. Musoma Yetu

  Musoma Yetu JF-Expert Member

  #78
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 11, 2016
  Messages: 2,311
  Likes Received: 1,789
  Trophy Points: 280
  Ndo kwanza anaanza!! Lazima akili ziwakae vizuri. Mwakani ntakuja bongo, miezi kama hii! Hope nitaoa wanawake bure au kwa kumnunulia chakula. Naimani hata shilingi itakuwa imeporomoka sana, so ntakuwa tajiri wa muda na hii midola yangu
   
 20. Musoma Yetu

  Musoma Yetu JF-Expert Member

  #79
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 11, 2016
  Messages: 2,311
  Likes Received: 1,789
  Trophy Points: 280
  Ndo kwanza anaanza!! Lazima akili ziwakae vizuri. Mwakani ntakuja bongo, miezi kama hii! Hope nitaoa wanawake bure au kwa kumnunulia chakula. Naimani hata shilingi itakuwa imeporomoka sana, so ntakuwa tajiri wa muda na hii midola yangu
   
 21. bukoba boy

  bukoba boy JF-Expert Member

  #80
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 15, 2015
  Messages: 5,063
  Likes Received: 2,616
  Trophy Points: 280
  Hizo ni Sheria,Income Tax.Hao wanapata kipato,tena halali.kama unasema kwa siku mmoja apate 30000 sasa kwa mwezi si 900,000 hiyo?hiki sio kipato?Si mlikua mnasema vyanzo vya kodi viongezwe ili kuongeza mapato?Ndio vinaongezwa hivo,haiwezekani mfanyakazi halmashauri apate 400,000 alipe income tax ila muosha magari anaepata 900,000 asilipe.Nyumbu wahed.

  Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app


  Haya mambo ya uchumi Malisa shallow sana,akomalie tu uandishi wa habari.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...