Naona Rais Magufuli anataka kufuta kabisa ajira zisizo rasmi nchini | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naona Rais Magufuli anataka kufuta kabisa ajira zisizo rasmi nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by stellahthatcher, Jul 17, 2017.

 1. stellahthatcher

  stellahthatcher Senior Member

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 14, 2015
  Messages: 169
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Serikali yake inafanya kila njia kudisturb atmosphere ya watu waliojiajiri ktk sekta isiyo rasmi. Wamachinga, wauza mkaa, wachoma mahindi, bodaboda, Shoe shiners, waosha magari, madobi etc ni watu wanaopita kipindi kigumu sana ktk utawala huu.

  Serikali imepiga marufuku kuosha magari maeneo ambayo si rasmi kwa ajili ya shughuli hizo. Yani kuanzia sasa ukikutwa unaosha gari eneo ambalo sio car wash unatozwa faini ya TZS 50,000/=. Pamoja na sababu za uchafuzi wa mazingira zilizotolewa, pia serikali imeeleza "issue" ya mapato. Kwamba hawa wanaoosha magari mitaani hawalipi kodi, biashara zao hazijasajiliwa, hawana leseni, wanaipotezea serikali mapato.

  Serikali inaamini magari yote yakioshwa kwenye maeneo maalumu ya kuoshea magari "car wash" zitapata mapato makubwa na kulipa kodi kubwa serikalini. Hii ni habari njema kwa wamiliki wa "Car Wash" na kwa serikali pia. Lakini ni habari mbaya sana kwa vijana waliokua wamejiajiri kwenye biashara hii na ni habari mbaya pia kwa wamiliki wa magari.

  Kwa upande wa ajira naona maelfu ya vijana wakipoteza ajira zao. Hawa wanalazimishwa kwenda kuwa wahalifu. Vijana hawa walikua wanapatikana zaidi maeneo ya mahotelini, Club, bar, au kumbi za starehe. Ukienda pale Seashells Hotel, Rombo Greenview hotel, Coco Beach, au B-Bar Sinza kwenye kitimoto, ukipaki gari yako nje anakuja kijana anakuuliza akuoshee? Ukikubali anakuoshea wakati wewe ukiendelea na shughuli zako nyingine. Ukimaliza unakuta gari tayari.

  Hii ni fursa ya ajira ambayo vijana waliiona. Na gharama zao zilikua nafuu. Ukipeleka gari "Car wash" ni 15,000/= lakini ukiosha kwa vijana hawa ni 3,000/= tu na gari inang'aa. Wana vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kazi hiyo. Kuna vijana walikua wanaosha hadi magari 20 kwa siku, maana yake walikua wanatengeneza karibu 60,000/= kila siku. Kupitia pesa hizo wanalipa kodi ya nyumba, wanasomesha watoto, wanavaa, wanakula etc. Sasa leo wamepigwa marufuku waende wapi?

  Serika inasema vijana hawa hawalipi kodi na hivyo kuipotezea serikali mapato. Ukweli ni kwamba hawakupaswa kulipa kodi ktk mfumo rasmi (direct tax) kwa sababu wao ni sekta isiyo rasmi. Duniani popote kuna ajira rasmi na ajira zisizo rasmi. Waliopo kwenye ajira rasmi hulipa "direct tax" lakini waliopo kwenye ajira zisizo rasmi hulipa "indirect tax" kutokana na vipato vyao.

  Watu kama wachoma mahindi, waosha magari, waziba pancha, mafundi viatu, hawawezi kulipa kodi directly TRA zaidi ya ushuru mdogo wanaotozwa na Halmashauri husika. Hawa ni tabaka la chini ambalo hutakiwi kuwadisturb. Waache watalipa kodi indirectly kupitia bidhaa watakazonunua.

  Muosha magari akiosha magari 10 kwa siku akapata 30,000/= atanunua sukari kupeleka nyumbani tayari amelipa kodi, atanunua nguo tayari kalipa nauli, atalipia umeme tayari kalipa kodi. Sasa kwanini tumlazimishe alipe direct tax TRA? Maana yake ni kwamba wachona mahindi nao waanze kutafuta leseni TRA, wanaobrush viatu nao waanze kusumbuliwa na TRA, waziba pancha nao, makonda wa daladala, bodaboda, wachoma mkaa. Hii si sawa. Hakuna mahali popote duniani wanakofanya upuuzi wa aina hii.

  Nenda hapo Kenya uone walivyo smart kwenye issue ya kodi na namna wanavyotambua sekta rasmi na zisizo rasmi. Pale Fort Jesus, Mombasa kwa nje kuna "Tour Guides" ambao hawajasomea popote. Ni wazee wa kiarabu waliokulia maeneo yale na wanafahamu historia ya ngome hiyo si kwa kusoma bali kwa kuona na kuhadithiwa. Wazee hawa wanafahamu mengi kuliko Tour Guides waliosomea darasani maana wao ni wazawa wa eneo lile.

  Wazee hawa waneamua kujiajiri wenyewe (sekta isiyo rasmi) kwa kuelekeza wageni. Serikali ya Kenya haiwasumbui wala kuwatoza kodi. Inajua watalipa kodi indirectly kupitia bidhaa watakazonunua. Lakini hapa kwetu tunataka hadi bodaboda walipe kodi, hadi wanaotembeza magazeti, na wanaobrush viatu. Tuwasajili TRA tuwape TIN number. Huu ni Wendawazimu.!

  Labda nieleze kwa kifupi madhara ya uamuzi huu wa "kukurupuka" wa serikali kufukuza vijana hawa wanaoosha magari maeneo yasiyo rasmi;

  #Mosi; Kuongezeka kwa wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana (Unemployment rate). Hali hii itafanya ugumu wa maisha kuongezeka, maana si kila muosha magari ataweza kutafuta fursa nyingine au shughuli nyingine ya kufanya. Ukosefu wa ajira ukiwa kwa kiwango kikubwa means hali ya maendeleo ya nchi itadumaa. Ukumbuke moja ya factor zinazopima maendeleo ya nchi ni pamoja na ajira.

  #Pili; mzunguko wa pesa kuzidi kuwa mdogo ktk jamii, na hivyo kusababisha mdororo wa uchumi. Mtu aliyekua anapata 30,000/= kwa siku akatumia kwa mahitaji mbalimbali ya nyumbani kwake means alikua anasaidia pesa kuzunguka. Just imagine kwa Dar peke yake kuna vijana 10,000 waliojiajiri kwenye shughuli hiyo. Kama vijana hao wanapata atleast 30,000/= kwa siku, ni jumla ya TZS milioni 300. Yani kuna TZS Milioni 300 zilikua zinazunguka kila siku kutoka kwa wamiliki wa magari kwenda kwa waosha magari, kutoka kwa waosha magari kwenda madukani, kwenda TANESCO kulipia luku, kwenda Dawasco kulipia maji, kwenda mashuleni kulipia ada etc.

  Lakini kuanzia sasa hiyo circulation imekufa rasmi. Yani pesa zitakuwepo lakini si katika mzunguko huo tena. That means kuna watoto watashindwa kulipiwa ada, kuna watu watashindwa kulipa kodi ya pango, etc. Hii itasababisha pesa kuadimika sana mtaani (intensive scarcity of money) kitu ambacho ni kiashira cha mdororo wa uchumi. Pesa inapaswa kuadimika lakini si kuadimika sana (Scarce but not very scarce).

  #Tatu; Kuongezeka kwa vitendo vya Uhalifu. Kumbuka kundi kubwa la watu waliokua wakifanya shughuli hii ni vijana ambao wengi wao wana nguvu. Hawa hawawezi kukaa "idle". Baadhi yao watatafuta shughuli za kufanya lakini wengine watajiingiza kwenye vitendo vya kihalifu ili kukabiliana na ugumu wa maisha. Hapa serikali inatengeneza bomu ambalo kulipuka kwake ni hatari kubwa kwa jamii. Tutegemee kusikia vikundi vya "Panya Road" "Watoto wa mbwa mwitu" etc vikijirudia.

  #Nne; Kuongezeka kwa tabaka kati ya wenye nacho na wasiokua nacho.

  #Tano; Kuongezeka kwa hali ya Uchafu unaosababishwa na magari mengi kutokuoshwa kwa muda mrefu. Kuanzia sasa kukutana na gari chafu itakua jambo la kawaida. Mtu aliyekua anaosha gari yake kila siku ataosha mara moja kwa wiki. Kwanza hatakua na muda wa kutosha kwenda Car wash kila siku. Mtu anatika kazini saa 12 jioni, anamua kupitia mahali apate chakula hapohapo anaosha na gari yake. Sasa hivi ni ngumu. Pili gharama anayolipa "Car Wash" kwa siku moja, alikua anaitumia kuosha kwa vijana wa mtaani wiki nzima.

  #Sita; Kudorora kwa shughuli nyingi za maendeleo kutokana na watu kupoteza muda. Watu wengi walikua wakitumia muda wa kuosha magari kufanya shughuli nyingine. Una kikao na mtu pale Regency Hotel, unaenda kukutana nae wakati mnaongea gari yako inaendelea kuoshwa. Mkimaliza kikao na gari imeng'ara. Lakini kuanzia sasa watu watalazimishwa kupoteza muda. Uende car wash masaa mawili ukitoka ndo uende Regency kwenye appointment. Kupoteza muda bila sababu.

  Nadhani serikali inapaswa kutizama upya utaratibu huu. Sina tatizo na wamiliki wa "Car Wash." Hoja yangu ni kwamba watu wasilazimishwe kwenda "Car Wash." kuosha magari yao. Kwanza hazitoshi. Takwinu zinaonesha Dar ina magari zaidi ya laki 9, lakini Car wash zote Dar hazifiki 100. Hii ina maana ili kila gari ioshwe inatakiwa Car wash moja ihudumie magari 900 kwa siku. Nani anaweza??

  So tusilazimishe watu kwenda Car Wash. Anayeweza kwenda aende, asiyeweza aoshe gari yake kwa utaratibu mwingine anaoona inafaa ikiwemo kuruhusu hawa vijana waliokua wakiosha maeneo yasiyo rasmi, kuendelea na shughuli zao.

  Ameandika Godlisten Malisa.
   
 2. Ifumange

  Ifumange JF-Expert Member

  #41
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 21, 2016
  Messages: 563
  Likes Received: 537
  Trophy Points: 180
  Kama nawaona wale vijana wa car wash pale ukonga recreation center

  Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
   
 3. SDG

  SDG JF-Expert Member

  #42
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 28, 2017
  Messages: 7,463
  Likes Received: 7,673
  Trophy Points: 280
  Wafanyakaz hewa uliwaona?Hao walowaweka hewa wameshtakiwa wapi?Kuna kesi yoyote ya mtu kuweka watumish hewa?
  Mi nadhan hewa ni wale wanaoambiwa watapangiwa kaz maalum,hewa ni wale wanaotumbuliwa ila bado wanalipwa,hewa ni wale waoambiwa wapishe uchunguz usioisha na wanaendelea kula mshahara.


  May Allah bless Me and You
   
 4. o

  oblac Senior Member

  #43
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 25, 2016
  Messages: 169
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Good
   
 5. o

  oblac Senior Member

  #44
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 25, 2016
  Messages: 169
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Hao wanalipa kodi indirect
   
 6. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #45
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,722
  Likes Received: 2,131
  Trophy Points: 280
  Kuna uzi humu watu wanasifia usafi wa miji ya wenzetu kama Kigali. Car wash zisizo rasmi ni uchafu!, maji yanatiririka ovyo kisa ajira!
   
 7. Mr.Junior

  Mr.Junior JF-Expert Member

  #46
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 8, 2013
  Messages: 8,957
  Likes Received: 4,559
  Trophy Points: 280
  Si Mchezo....!!!!
   
 8. U

  UCD JF-Expert Member

  #47
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 3,386
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  Nafikiri ni uelewa mdogo katika maswala ya uchumi ndugu yangu Malisa. Sasa hao waosha magari kama takwimu zako ziko sawa basi tutegemee car wash kuongezeka ili hao waosha magari waajiriwe huko ili walipwe vizuri na benefit zingine kama bima za afya na wawekewe na pesa kwenye mifuko ya jamii kwa ajili ya maisha yao ya baadae hii ina maana zaidi kuliko wanavyofanya sasa hivi. Akiugua ndo basi pia wakumbuke wanazidi kuzeeka. Kwa system ya kuajiriwa ina maana na faida zaidi kuliko mfumo wa sasa ulioueleza hapo juu. Think beyond the box mkuu!!
   
 9. Madam Mwajuma

  Madam Mwajuma Verified User

  #48
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 13, 2014
  Messages: 6,564
  Likes Received: 4,766
  Trophy Points: 280
  Kama maeneo sio rasmi kwa nini wafanye kazi hapo? Aende ajisajili afanye kazi kiuhalali alipe kodi.
   
 10. n

  ndeambase JF-Expert Member

  #49
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2016
  Messages: 630
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 80
 11. marxlups

  marxlups JF-Expert Member

  #50
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 8,129
  Likes Received: 2,991
  Trophy Points: 280

  Je na wale abiria wanaozidi kwenye mabasi, hawana ticket japokuwa nauli wanakuwa wamelipa, je wanalipa wapi kodi?

  Bus linatoka Dar linakwenda Moro limezidisha abiria 7 x tshs 7000 = 49,000
  Kampuni ina mabasi 12 yanapiga trip kwa siku (49,000 x 12 = 588,000 kwa siku)
  Tshs 588,000 x siku 7 = 411,6000 kwa wiki
  Tshs 411,6000 x wiki 4 = 16,464,000 kwa mwezi
  Tsh 16,464,000 x 12 = Tshs 197,568,000 kwa mwaka hazijalipwa kodi na kampuni moja

  197,568,000 x idadi ya kampuni sinazofanya biasha katika njia hiyo utajua ni kiasi gani serikali inapoteza kwenye kodi, linganisha na hiyo kodi ya waosha magari
   
 12. k

  kamwamu JF-Expert Member

  #51
  Jul 17, 2017
  Joined: May 18, 2014
  Messages: 1,436
  Likes Received: 647
  Trophy Points: 280
  Ajira zisizo rasmi zinalindwa na kufumbiwa macho sana. Vinginevyo huijui sheria ya nguvu kazi. Usiombe serikali ikaitekeleza.
   
 13. mohamedi-2

  mohamedi-2 Member

  #52
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 15, 2015
  Messages: 69
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 25
  Kuhusu panya road kwetu kitunda juzi usiku wamevamia vijana karibia 20 wamevunja geti lajirani yangu wamekomba kilakitu namapanga wakamkata Jirani yangu yaani sijui tunapoelekea niwapi.

  Sent from my X-TIGI_JOY8 using JamiiForums mobile app
   
 14. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #53
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,921
  Trophy Points: 280
  Sasa inakuwaje wanajiajiri kiholela bila kufuata taratibu kama kuwa na leseni na eneo maalum la kufanyia biashara. Serikali isiruhusu uholela holela, lazima tubadilike wanaoshindwa kumudu life mjini mliambiwa mwisho July
   
 15. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #54
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,921
  Trophy Points: 280
  Haiwezekani mtu unaishi kwenye big city unaamka asubuhi na kopo la maji tu unaanza kutafuta magari yamepaki unaosha. Huu ni uchafuzi wa miji na faini iongezwe
   
 16. Lutsala

  Lutsala JF-Expert Member

  #55
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 21, 2014
  Messages: 548
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 60
  Unaposema huyo anayeosha magari atakwenda kuwa jambazi ina maana alishakuwa jambaz kwa kuwa MTU huwez amka vuuup ukawa jambazi

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 17. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #56
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,920
  Likes Received: 1,191
  Trophy Points: 280
  Ahaa wapi! NewYork wanauzia bidhaa ndani ya barabara na njia za watembea kwa miguu? Halafu Trump anasema ruksa!? Maybe NewYork aina ya Call me J.
   
 18. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #57
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,920
  Likes Received: 1,191
  Trophy Points: 280
  Pia haiwezekani mtu unaishi Big City unatoka na Jiko na Sufuria na mkaa unaenda kusema njia za mwendokasi au njia za wapiga kwa miguu unasema unatafuta rizki. Huu ni uharibifu wa miundombinu ya bilions na uchafuzi wa mazingira.
   
 19. nyanimzungu

  nyanimzungu JF-Expert Member

  #58
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 4, 2017
  Messages: 1,239
  Likes Received: 870
  Trophy Points: 280
 20. Prince Kunta

  Prince Kunta JF-Expert Member

  #59
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 27, 2014
  Messages: 9,084
  Likes Received: 7,309
  Trophy Points: 280
  Ukiwa na utawala wa wenye ubinafsi badala ya kuwa na uongozi bora basi ni kawaida kutokea hali kama hiyo
   
 21. Prince Kunta

  Prince Kunta JF-Expert Member

  #60
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 27, 2014
  Messages: 9,084
  Likes Received: 7,309
  Trophy Points: 280
  Si huwa mnaamasisha kujiajiri nyie
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...