Naona Rais Magufuli anataka kufuta kabisa ajira zisizo rasmi nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naona Rais Magufuli anataka kufuta kabisa ajira zisizo rasmi nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by stellahthatcher, Jul 17, 2017.

 1. stellahthatcher

  stellahthatcher Senior Member

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 14, 2015
  Messages: 169
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Serikali yake inafanya kila njia kudisturb atmosphere ya watu waliojiajiri ktk sekta isiyo rasmi. Wamachinga, wauza mkaa, wachoma mahindi, bodaboda, Shoe shiners, waosha magari, madobi etc ni watu wanaopita kipindi kigumu sana ktk utawala huu.

  Serikali imepiga marufuku kuosha magari maeneo ambayo si rasmi kwa ajili ya shughuli hizo. Yani kuanzia sasa ukikutwa unaosha gari eneo ambalo sio car wash unatozwa faini ya TZS 50,000/=. Pamoja na sababu za uchafuzi wa mazingira zilizotolewa, pia serikali imeeleza "issue" ya mapato. Kwamba hawa wanaoosha magari mitaani hawalipi kodi, biashara zao hazijasajiliwa, hawana leseni, wanaipotezea serikali mapato.

  Serikali inaamini magari yote yakioshwa kwenye maeneo maalumu ya kuoshea magari "car wash" zitapata mapato makubwa na kulipa kodi kubwa serikalini. Hii ni habari njema kwa wamiliki wa "Car Wash" na kwa serikali pia. Lakini ni habari mbaya sana kwa vijana waliokua wamejiajiri kwenye biashara hii na ni habari mbaya pia kwa wamiliki wa magari.

  Kwa upande wa ajira naona maelfu ya vijana wakipoteza ajira zao. Hawa wanalazimishwa kwenda kuwa wahalifu. Vijana hawa walikua wanapatikana zaidi maeneo ya mahotelini, Club, bar, au kumbi za starehe. Ukienda pale Seashells Hotel, Rombo Greenview hotel, Coco Beach, au B-Bar Sinza kwenye kitimoto, ukipaki gari yako nje anakuja kijana anakuuliza akuoshee? Ukikubali anakuoshea wakati wewe ukiendelea na shughuli zako nyingine. Ukimaliza unakuta gari tayari.

  Hii ni fursa ya ajira ambayo vijana waliiona. Na gharama zao zilikua nafuu. Ukipeleka gari "Car wash" ni 15,000/= lakini ukiosha kwa vijana hawa ni 3,000/= tu na gari inang'aa. Wana vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kazi hiyo. Kuna vijana walikua wanaosha hadi magari 20 kwa siku, maana yake walikua wanatengeneza karibu 60,000/= kila siku. Kupitia pesa hizo wanalipa kodi ya nyumba, wanasomesha watoto, wanavaa, wanakula etc. Sasa leo wamepigwa marufuku waende wapi?

  Serika inasema vijana hawa hawalipi kodi na hivyo kuipotezea serikali mapato. Ukweli ni kwamba hawakupaswa kulipa kodi ktk mfumo rasmi (direct tax) kwa sababu wao ni sekta isiyo rasmi. Duniani popote kuna ajira rasmi na ajira zisizo rasmi. Waliopo kwenye ajira rasmi hulipa "direct tax" lakini waliopo kwenye ajira zisizo rasmi hulipa "indirect tax" kutokana na vipato vyao.

  Watu kama wachoma mahindi, waosha magari, waziba pancha, mafundi viatu, hawawezi kulipa kodi directly TRA zaidi ya ushuru mdogo wanaotozwa na Halmashauri husika. Hawa ni tabaka la chini ambalo hutakiwi kuwadisturb. Waache watalipa kodi indirectly kupitia bidhaa watakazonunua.

  Muosha magari akiosha magari 10 kwa siku akapata 30,000/= atanunua sukari kupeleka nyumbani tayari amelipa kodi, atanunua nguo tayari kalipa nauli, atalipia umeme tayari kalipa kodi. Sasa kwanini tumlazimishe alipe direct tax TRA? Maana yake ni kwamba wachona mahindi nao waanze kutafuta leseni TRA, wanaobrush viatu nao waanze kusumbuliwa na TRA, waziba pancha nao, makonda wa daladala, bodaboda, wachoma mkaa. Hii si sawa. Hakuna mahali popote duniani wanakofanya upuuzi wa aina hii.

  Nenda hapo Kenya uone walivyo smart kwenye issue ya kodi na namna wanavyotambua sekta rasmi na zisizo rasmi. Pale Fort Jesus, Mombasa kwa nje kuna "Tour Guides" ambao hawajasomea popote. Ni wazee wa kiarabu waliokulia maeneo yale na wanafahamu historia ya ngome hiyo si kwa kusoma bali kwa kuona na kuhadithiwa. Wazee hawa wanafahamu mengi kuliko Tour Guides waliosomea darasani maana wao ni wazawa wa eneo lile.

  Wazee hawa waneamua kujiajiri wenyewe (sekta isiyo rasmi) kwa kuelekeza wageni. Serikali ya Kenya haiwasumbui wala kuwatoza kodi. Inajua watalipa kodi indirectly kupitia bidhaa watakazonunua. Lakini hapa kwetu tunataka hadi bodaboda walipe kodi, hadi wanaotembeza magazeti, na wanaobrush viatu. Tuwasajili TRA tuwape TIN number. Huu ni Wendawazimu.!

  Labda nieleze kwa kifupi madhara ya uamuzi huu wa "kukurupuka" wa serikali kufukuza vijana hawa wanaoosha magari maeneo yasiyo rasmi;

  #Mosi; Kuongezeka kwa wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana (Unemployment rate). Hali hii itafanya ugumu wa maisha kuongezeka, maana si kila muosha magari ataweza kutafuta fursa nyingine au shughuli nyingine ya kufanya. Ukosefu wa ajira ukiwa kwa kiwango kikubwa means hali ya maendeleo ya nchi itadumaa. Ukumbuke moja ya factor zinazopima maendeleo ya nchi ni pamoja na ajira.

  #Pili; mzunguko wa pesa kuzidi kuwa mdogo ktk jamii, na hivyo kusababisha mdororo wa uchumi. Mtu aliyekua anapata 30,000/= kwa siku akatumia kwa mahitaji mbalimbali ya nyumbani kwake means alikua anasaidia pesa kuzunguka. Just imagine kwa Dar peke yake kuna vijana 10,000 waliojiajiri kwenye shughuli hiyo. Kama vijana hao wanapata atleast 30,000/= kwa siku, ni jumla ya TZS milioni 300. Yani kuna TZS Milioni 300 zilikua zinazunguka kila siku kutoka kwa wamiliki wa magari kwenda kwa waosha magari, kutoka kwa waosha magari kwenda madukani, kwenda TANESCO kulipia luku, kwenda Dawasco kulipia maji, kwenda mashuleni kulipia ada etc.

  Lakini kuanzia sasa hiyo circulation imekufa rasmi. Yani pesa zitakuwepo lakini si katika mzunguko huo tena. That means kuna watoto watashindwa kulipiwa ada, kuna watu watashindwa kulipa kodi ya pango, etc. Hii itasababisha pesa kuadimika sana mtaani (intensive scarcity of money) kitu ambacho ni kiashira cha mdororo wa uchumi. Pesa inapaswa kuadimika lakini si kuadimika sana (Scarce but not very scarce).

  #Tatu; Kuongezeka kwa vitendo vya Uhalifu. Kumbuka kundi kubwa la watu waliokua wakifanya shughuli hii ni vijana ambao wengi wao wana nguvu. Hawa hawawezi kukaa "idle". Baadhi yao watatafuta shughuli za kufanya lakini wengine watajiingiza kwenye vitendo vya kihalifu ili kukabiliana na ugumu wa maisha. Hapa serikali inatengeneza bomu ambalo kulipuka kwake ni hatari kubwa kwa jamii. Tutegemee kusikia vikundi vya "Panya Road" "Watoto wa mbwa mwitu" etc vikijirudia.

  #Nne; Kuongezeka kwa tabaka kati ya wenye nacho na wasiokua nacho.

  #Tano; Kuongezeka kwa hali ya Uchafu unaosababishwa na magari mengi kutokuoshwa kwa muda mrefu. Kuanzia sasa kukutana na gari chafu itakua jambo la kawaida. Mtu aliyekua anaosha gari yake kila siku ataosha mara moja kwa wiki. Kwanza hatakua na muda wa kutosha kwenda Car wash kila siku. Mtu anatika kazini saa 12 jioni, anamua kupitia mahali apate chakula hapohapo anaosha na gari yake. Sasa hivi ni ngumu. Pili gharama anayolipa "Car Wash" kwa siku moja, alikua anaitumia kuosha kwa vijana wa mtaani wiki nzima.

  #Sita; Kudorora kwa shughuli nyingi za maendeleo kutokana na watu kupoteza muda. Watu wengi walikua wakitumia muda wa kuosha magari kufanya shughuli nyingine. Una kikao na mtu pale Regency Hotel, unaenda kukutana nae wakati mnaongea gari yako inaendelea kuoshwa. Mkimaliza kikao na gari imeng'ara. Lakini kuanzia sasa watu watalazimishwa kupoteza muda. Uende car wash masaa mawili ukitoka ndo uende Regency kwenye appointment. Kupoteza muda bila sababu.

  Nadhani serikali inapaswa kutizama upya utaratibu huu. Sina tatizo na wamiliki wa "Car Wash." Hoja yangu ni kwamba watu wasilazimishwe kwenda "Car Wash." kuosha magari yao. Kwanza hazitoshi. Takwinu zinaonesha Dar ina magari zaidi ya laki 9, lakini Car wash zote Dar hazifiki 100. Hii ina maana ili kila gari ioshwe inatakiwa Car wash moja ihudumie magari 900 kwa siku. Nani anaweza??

  So tusilazimishe watu kwenda Car Wash. Anayeweza kwenda aende, asiyeweza aoshe gari yake kwa utaratibu mwingine anaoona inafaa ikiwemo kuruhusu hawa vijana waliokua wakiosha maeneo yasiyo rasmi, kuendelea na shughuli zao.

  Ameandika Godlisten Malisa.
   
 2. l

  lolo123 JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 2, 2017
  Messages: 457
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 80
  Lengo la JPM ktk jiji la Dar....ni kulifanya lifanane kimazingira kama New York
   
 3. FAIZHAD

  FAIZHAD JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 20, 2015
  Messages: 858
  Likes Received: 695
  Trophy Points: 180
  Umenena vyema
   
 4. witnessj

  witnessj JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 22, 2015
  Messages: 7,226
  Likes Received: 7,893
  Trophy Points: 280
 5. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,501
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Good analysis .Yaani ningekupa like 100 kama inawezekana
   
 6. I

  Idofi JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 1,591
  Likes Received: 846
  Trophy Points: 280
  wacha tuisome namba tutaonana 2020
   
 7. stellahthatcher

  stellahthatcher Senior Member

  #7
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 14, 2015
  Messages: 169
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Kama ni hivyo kwanini pale Posta wasiweke sehemu kuubwa ya parking halafu waosha magari wasajiliwe kila siku wawe wanalipa kiasi fulani kama Tsh 500 kama ambavyo Daladala zinalipa na wale watu wa Sokoni wenye meza?
   
 8. stellahthatcher

  stellahthatcher Senior Member

  #8
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 14, 2015
  Messages: 169
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Wewe ulijua mapema Wit?
   
 9. wambura marwa

  wambura marwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 7, 2015
  Messages: 2,180
  Likes Received: 1,098
  Trophy Points: 280
  Rais wa wanyonge yupo kazini akiwaminya wanyonge.

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 31,006
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kama shida ni kodi kwa nini wasingeanzisha utaratibu wa hao vijana kulipa serikalini kiasi fulani???

  Hivi hakunaga wabunifu huko eeeh???
   
 11. h

  hardboy JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 2, 2016
  Messages: 796
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 180
  Udiktefa wavhii serikali sasa unaanza kukomaa, hapo inaonekana serikali inataka kuwafukuza mijini wasi na kazi zisjzokuwa rasmi.

  Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
   
 12. umerogwa wewe

  umerogwa wewe JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 8, 2017
  Messages: 424
  Likes Received: 532
  Trophy Points: 180
  Kaletwa na Mungu huyu
   
 13. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,921
  Trophy Points: 280
  Hao vijana si ndio wataajiliwa na hizo car wash. Tuache kuishi bila kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa
   
 14. m

  mwenyeKitu JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 28, 2015
  Messages: 956
  Likes Received: 747
  Trophy Points: 180
  Tuache unafiki hatuwezi kujivunia sekta isiyo rasmi inayojiendea shakala bagala.


  Simply kwa sababu tunaogopa watu watakuwa wahalifu...lazima mianya ya kuishi mjini kiujanja ujanja iminywe ili watu walipe kodi.

  Tukienda ulaya tunaishia kupiga picha miji ya watu. ..kuonyesha mandhari ...ajabu hapa tunataka tuache ukanjanja uendelee uchuuzi kila mahali
   
 15. tamuuuuu

  tamuuuuu JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 10, 2014
  Messages: 9,062
  Likes Received: 5,784
  Trophy Points: 280
  Na bado

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 16. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,240
  Likes Received: 3,602
  Trophy Points: 280
  Hakuna asiyelipa kodi kama akili yako inafikiri sawa sawa!
   
 17. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2017
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Na nikaamua niwe na liosha nyumbani kwangu?

  Sent from my SM-N910C using JamiiForums mobile app
   
 18. m

  mwl JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2017
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 991
  Likes Received: 726
  Trophy Points: 180
  Team Lumumba njooni haraka hakuna haja ya kupiga jaramba.

  Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
   
 19. Kanye2016

  Kanye2016 JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 4, 2016
  Messages: 1,856
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  Tanzania mpya inakuja tuwe wavumilivu
   
 20. B

  Babati JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 7, 2014
  Messages: 31,833
  Likes Received: 25,118
  Trophy Points: 280
  Safari hii mpaka wasusi mtaani watawekewa EFD machine.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...