Naona nguvu kubwa ambayo wenzangu wa CCM wanayoitumia kumnanga Lazaro Nyalandu

nyalandu aliondoka lini? na huko ccm alifukuzwa lini? acha uongo hilo bunge limemtema wapi wakat spika hajui wala hajapata barua ya nyalandu kweli kawayumbisha
Mkuu huyo unaemjibu haeleweki, uwezo wa kujenga hoja hana ni mweupe sana utajichosha bure.
 
Tuhuma zote za Nyalandu zilianzishwa na CHADEMA. Hakuna hata siku moja CCM walimuanzishia tuhuma Mh. Nyalandu. Kinachoshamgaza ni ujasiri wa Nyalandu kuhamia chama kilichomtuhumu kwa nguvu nyingi na kumnyang'anya tonge mdomoni akiwa waziri na hivyo kuiokoa serikali na nchi kupoteza mapato kibao. Na pia inashtua kuona CHADEMA kumpokea bila kukanusha kuwa tuhuma walizoanzisha kuhusu Nyalandu zilikuwa fake yaani feki
 
Wewe jamaa umeongea vizuri sana..sikutarajia kuna mwana ccm anaweza waambia wenzake ukweli.....
Wewe baki ccm hukohuko uwafundishe wenzako waache ushabiki
 
Je kama Nyalandu leo anaonekana ni mwizi au fisadi licha ya kuwa hakuna vithibitisho ,vipi akina ngereja,Chenge,akina Muhongo si wako ccm wameishafukuzwa au kuchukuliwa hatua yoyote,?
Mmmmmh ,vilaza wakikujibu njo nikupe 50000
 
Ndugu nyalandu, ulipokwenda (Chadema), si sehemu ya Wewe kua na kinga dhidi ya makosa uliyofanya wizara ya maliasili.
Awamu ya tano haitakua na msalie mtume kwa wabadhilifu na wahujumu uchumi, utashughulikiwa popote utakapokwenda dunia hii.

Ulipokimbilia ndio sehemu iliolalamika Sana kuhusu udhalimu uliokua unaufanya wizarani, Lema, Msigwa na wengine wengi wanafahamu ulichokifanya ulipokua waziri wa maliasili na utalii. Jiandae kisaikolojia kujibu tuhuma zinzokukabili.
 
Nchi hii mpaka ccm iondoke madarakani ndio matatizo yetu yatapungua
Cha kwanza tuiondoe ccm kwanza kwa kuwa hata ashuke malaika kutoka mbinguni kuja kuwa ccm anamsahau kabisa na Mungu na alikotoka
 
Naona dawa inawaingia kwei kweli, nahisi siku magufuli akienda cuf au chadema mtasema aliuza nyumba za serikali yaani hamtaacha kumpiga madongo
 
Nchi hii mpaka ccm iondoke madarakani ndio matatizo yetu yatapungua
Cha kwanza tuiondoe ccm kwanza kwa kuwa hata ashuke malaika kutoka mbinguni kuja kuwa ccm anamsahau kabisa na Mungu na alikotoka

Kuiondoa CCM bila kujua atachukua nani itakuwa utaahira mkubwa. Wanasiasa wenyewe wanaoharibu ndio wanacheza kila upande...bora zimwi likujualo. Halikuli ukakwisha.

Wapinzani nadiriki kusema bado sana...they think they can survive by eating left overs!! Hakunaga hicho kitu.
 
Acha kuwatisha wahalifu mlionao huko ccm kwamba wakihama chama watashtakiwa. Mkiwashitaki wakati bado wako kwenye chama chenu tutaona kweli ccm ni safi. Uchafu mnauona mtu akiwa nje ya ccm, shame.
 
Anaandika kada wa CCM Mansour Jumanne,
LEO JPM ATAMFUKUZA HUYU CCM

"Naona nguvu kubwa ambayo wenzangu wa CCM wanayoitumia kumnanga Lazaro Nyalandu.

Naona namna ambavyo rafiki zangu akina Muro ,Polepole,na makada wengine wa ccm wakifukua nyaraka za nyuma na tuhuma za Ufisadi dhidi ya Nyalandu

Binafsi uwa naangalia mambo kwa jicho la Social Ethics na hapa uwa naangalia Dentelogical, Teleological na Situational Ethics, kwa maana ya Empacts ,Final results na Situation .Je kwanini Nyalandu amehama ? Ingekuwaje Nyalandu angebaki ccm? Matokeo ya nyalandu kiacha chama tawala yatakuwa ni yapi?

Sasa kwa kuzingatia misingi hii lazima uzame kwenye Critical thinking ,ili uwaze zaidi na kuwazua na hapa utakutana na Logic,Reasoning nk na hapa ndio unapata nafasi ya kujiuliza mambo mengi ,maswali mengi nk mfano

1.Mwaka 2015 nani alimpitisha Nyalandu kwenye kura za maoni?

2.Kama Nyalandu alikuwa na shida kwanini hakukatwa ?

3.Je rais Rais Magufuli alimnadi Nyalandu 2015?

4.Je Nyalandu kuna kipindi wabunge waliwahi kupinga bajeti kwa ajili ya wizara aliyowahi kuifanyia kazi?

5.Baada ya Rais Magufuli kupata Urais alianza kusafisha Chama je Nyalandu aliwahi kufukuzwa?

6.Je Nyalandu amewahi kutuhumiwa na Chama cha mapinduzi kwenye Kashfa yoyote?

7.Je kama Nyalandu leo anaonekana ni mwizi au fisadi licha ya kuwa hakuna vithibitisho ,vipi akina ngereja,Chenge,akina Muhongo si wako ccm wameishafukuzwa au kuchukuliwa hatua yoyote,?

Sasa baada ya Chritical Thinking lazima tuingie kwenye Fallacy na hapa ndipo fallacy inachukua nafasi ,je kama Lazaro ni mwizi na alikuwa ccm na hawakumfanya kitu kwahiyo je CCM wote ni WEZI?kama Nyalandu alikuwa CCM na Nyalandu wanasema ni fisadi kwaiyo ccm wote ni Mafisadi? Hii ndio fallacy jumuishi inavyotuhukumu.

Ila baada ya Fallacy lazime twende kuitimisha sasa kwa kujipima katika theory zetu na hapa ndipo BULLET THEORY Ufanya kazi zaidi hasa kwa kuassume kuwa Watu hawajui lolote,ni mafala ni mataila,ni mazwazwa ,ni malofa sasa je kupitia theory hii Issue ya kuhama kwa Nyalandu CCM tunavyomshambulia wakati alikuwa kwetu tunataka kuaminisha Dunia kuwa watanzania ni mafala ,mataila,mazwazwa,malofa,mambumbu kwa mujibu bullet theory?

Ndugu zangu kwa sasa lazima CCM tubaki basi maana yake turejeshe majeshi nyuma na kujipanga upya alafu tuje tena na hoja nzito dhidi ya tuhuma alizotoa Nyalandu dhidi ya Chama chetu .

Wasalaam,
Mansour Jumanne,
The Watcher.
Social ethics you remind me of St.Apia kuna siku Mwanafunzi aliandika andiko katika gazeti moja ambalo halikumpendekza padre mmoja na jopo lake. Huyu jamaa alikuwa rafiki yangu sana huyu sr. mzambia kama sikosei na ama kusahau ambaye alikuwa anafundisha comparative religion chuoni akaniita akaniuliza kwa msingi ya social ethics unadhani huyu anafaa adhabu gani. The answer was sijasoma andiko hilo na hivyo sina la kusema juu ya adhabu inayomstahili MTU huyu mnayemsema. Akaniuliza he waamini katika injili? Jibu likawa naamini katika mungi anayejali usawa wa watu wote. Basi nami nikaambiwa tembea toka nje ila usijaribu kugombea nafasi yeyote hapa chuoni. Nami nikasema basi na jamani ya mungu aliye mkweli na asiye na unafiki katika maisha anitangulie na awe nanyi pia. Walimpitisha rais wa chuo ambaye Leo ni mbunge na alikuwa kwenye kamati moja hivi juzi ambayo kwa imani yangu ilidanganya
 
Back
Top Bottom