Naona mwanamke ndio anafaa kuongoza Bunge linaloendana na Rais Samia Suluhu. Tunao Gaudencia Kabaka, Anna Mghwira n.k

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Kiu ya Rais wetu ni kuona Bunge linajadili vitu kwa upana na kwa kuwa bunge chini ya Spika Ndugai anaonekana kuzidiwa lakini anashindwa kusema asaidiwe kwa sababu Mhe. Rais anapenda kuona kuona wanaozidiwa wanaomba kusaidiwa lakini hafanyi hivyo basi kwa niaba yake tunaomba Mhe. Rais msaidie.

Naamini ili kupata bunge lenye uwezo wa kujadili hoja kwa mapana inatakiwa apatikane spika mwenye uwezo mkubwa na akipatikana Spika mwanamke itapendeza sana.

Kwa ni Spika mwanamke?
Mwanamke kwa asili ni kiumbe anayependa haki itendeke na kutenda siku zote kwa haki, na zaidi ya yote mwanamke ni msimamizi mzuri wa taratibu, kanuni na sheria bila kujali mwanamke huyo ni nani, sifa hizi ni za jumla.

Katika Bunge, Spika anaonekana kupwaya kwa sababu hasimamii kanuni, taratibu na sheria ipasavyo hivyo kufanya bunge kuacha kujadili hoja za kitaifa. Sababu hii pekee inatosha kufanya Ndugai apumzike/apumzishwe kwa maslahi mapana ya nchi.

Ndani ya nchi tunao wanawake wengi wenye uwezo wa kusimamia mhimili wa bunge lakini naomba tuwaangalie hawa wawili kwa kuanzia, Mhe. Gaudencia Kabaka na Anna Mngwira.

Mhe Kabaka akiwa ni mwenyekiti wa UWT taifa ameonesha uwezo mkubwa wa kuongoza kwa ufanisi jeshi hilo la wanawake Tanzania. Ana uzoefu mkubwa wa kuongoza kwa kuangalia uzoefu wa nafasi alizowahi kushika.. Kwa uchache huu ana uwezo wa kuongoza bunge la JMT.

Anna Mngwira, ni mkuu wa mkoa wa kiliamanjaro kwa sasa lakini pia amewahi kuwa mwenyekiti wa ACT Taifa na Mgombea Urais kupitia ACT, 2015. Mwanamke kuongoza taasisi ya kisiasa kwa ngazi ya taifa na kugombea urais ni uwezo mkubwa. Inaonesha ana utashi na uwezo mkubwa wa kuongoza bunge na kuleta matokeo makubwa.

Kwa maslahi mapana ya nchi yetu, Ndugai apumzike na bunge kukabidhiwa mwanamke.
 
Je katika sifa zote, Wana shahada ya Sheria? Maana hicho ndio kigezo kikuu cha kuwa spika, Naibu spika au Katibu wa Bunge.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom