Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Siku hizi kila jumapili katika kanisa la Mchungaji Gwajima inaendeshwa ibada iitwayo Makonda Attack. Watu wa dini mbalimbali wakiwemo hata waislam huwa wanahudhuria ibada hii, vyombo vingi vya habari pia wanahudhuria.
Ni jambo la kushangaza kuona wakati wa ibada hii mchungaji Gwajima akimsifu Rais Magufuli na wakati huo huo akimshambulia mteule wake Paul Makonda.
Ni wakati muhimu kwa serikali kuona haya manyumba ya ibada yasitumike kwenye mambo ya kisiasa yanaweza kusababisha nchi yetu kuwa na vyama vya kisiasa vyenye dalili za udini.
Kama Gwajima ana tuhuma dhidi ya Makonda kuna njia ya kuongea na waandishi wa habari na hata kwenda mahakamani lakini si kutumia ibada ya jumapili kushambulia viongozi wa serikali. Mheshimiwa Makonda wewe ndio kiongozi wa mkoa wa Dar hakuna haja ya kuzunguka na clip ya mwanamke aliyezaa na Gwajima. Una uwezo wa kufuta usajili wa kanisa hilo kama inatumika kwa dhamira nyingine. Mnakumbuka wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Gwajima alimuunga nani mkono kwahiyo msitegemee atabadilika.
Na ushauri wangu kwa Mchungaji Gwajima vua hilo joho la utumishi wa mungu halafu uingie kwenye ulingo wa kisiasa.