Naona kuna shida ya ajira au kupata fedha. Jimbo moja watia nia zaidi ya 500. Au siasa imekuwa ya yeyote anayeweza?

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
914
1,000
1. Magufuli alisema kazi ya urais ni kazi ngumu sana anatamani aondoke hata leo, lakini bado kachukua fomu ya kuomba kuongoza dola (sio fomu ya kuomba nafasi ya chama kuwa mgombea). Na tena fomu ilikuwa moja tu.

2. Naona wakuu wa mikoa, wilaya, DED na wateule karibia wote wanataka kuwa wabunge sijajua huko bungeni kuna nini? Kinachokimbiliwa

3. Jimbo moja watia nia wanazidi 500 kwa vyama vyote najiuliza nafasi moja ya kazi wanaomba ni zaidi ya 500 shida ni kubwa ya ajira na walio na ajira hazina maslai kwa jicho lingine hivyo kipato cha uchumi wa kati ni wazi hakigawanywi sawa kwa taifa.

4. Je, kwenye nafasi za kisiasa kuvamiwa na watu wengi hivi ni dalili gani kwa taifa?

A) Inalipa kuliko kazi nyingine zote
B) Vigezo vya kujua kusoma na kuandika kiswahili vinavutia wengi hata wasio kwenda shule
C) Ni kazi rahisi?
D) Ukosefu wa ajira nchini?
 
Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
28,770
2,000
Tatizo lipo kubwa sana tutahakikisha ufumbuzi unapatikana.

Kwasasa hivi ni aibu kubwa sana
Hili jambo kwa sasa kama mzaha vile Ila ni tatizo!
 
Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,504
2,000
dosama,
#SeriousJoke

Tume ya utumishi wa bunge inatangaza nafasi 393 za uwakilishi wa wananchi ambazo ziko wazi kuanzia tarehe 16/6/2020.

SIFA ZA MWOMBAJI:
- Awe raia wa Tanzania
- vAwe na umri wa miaka 21 au zaidi
- Ajue kusoma na kuandika kwa Kiswahili
- Awe mwanachama wa chama cha siasa.
- Uzoefu si lazima

MASHARTI YA AJIRA:
- Muda wa kazi: Miaka 5
- Kituo cha kazi: Dodoma
- Eneo la kazi: kwa wananchi
- Anaripoti kwa: Spika wa bunge
- Uwezo wa kusafiri nje/ndani ya nchi: Angalau 50% ya muda wake..

MASLAHI:
- Mshahara: TZS 3.8M kwa mwezi
- Posho: TZS 8M kwa mwezi
- Posho ya Kikao: TZS 240K kwa siku
- Posho kujikimu: TZS 120K kwa siku
- Pensheni: TZS 240M baada ya miaka mitano
- Bima ya afya ya daraja la kwanza kwako na familia yako
- Safari za nje
- Mshahara hauna makato ya Bima ya afya wala mifuko ya hifadhi ya jamii.

KUTUMA MAOMBI:
Maombi yote yatumwe kwa wananchi wa majimbo husika kwa kutumia ushawishi wa vyama vya siasa. Mwombaji awe tayari kuanza kazi kuanzia November 1 mwaka 2020.!
 
gilldenu

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
2,785

Kama ndo iko hivi acha tu watu watangaze nia.
 
sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,511
2,000
dosama,

Mkuu ni sahihi kabisa. Hivi akili ya mtu mmoja bila ushindani si inakuwa arrogant imelala usingizi wa pono?
Miaka 5 ijayo hatutakuwa na usultani. Labda kuwakumbusha wengine tafuta nchi au kazi nyingine ikiwa utaendekeza upuuzi wa leo.
 
IPECACUANHA

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
3,158
2,000
1. Magufuli alisema kazi ya urais ni kazi ngumu sana anatamani aondoke hata leo, lakini bado kachukua fomu ya kuomba kuongoza dola (sio fomu ya kuomba nafasi ya chama kuwa mgombea). Na tena fomu ilikuwa moja tu.

2. Naona wakuu wa mikoa, wilaya, DED na wateule karibia wote wanataka kuwa wabunge sijajua huko bungeni kuna nini? Kinachokimbiliwa

3. Jimbo moja watia nia wanazidi 500 kwa vyama vyote najiuliza nafasi moja ya kazi wanaomba ni zaidi ya 500 shida ni kubwa ya ajira na walio na ajira hazina maslai kwa jicho lingine hivyo kipato cha uchumi wa kati ni wazi hakigawanywi sawa kwa taifa.

4. Je kwenye nafasi za kisiasa kuvamiwa na watu wengi hivi ni dalili ganinkwa taifa?

A) inalipa kuliko kazi nyingine zote
B) vigezo vya kujua kusoma na kuandika kiswahili vinavutia wengi hata wasio kwenda shule
C) ni kazi rahisi?
D) ukosefu wa ajira nchini
Jibu la maswali hapo juu ni Imani katika "goli la mkono"
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom