Naona kuna haja ya kundeleza baazi ya mila zetu jamani!!!

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,232
Unajua kuna mambo mpaka leo mimi sielewi sijui tulilogwa kuyaacha au tulilazimishwa.

Mfano mtu akienda kwa mganga wa jadi akapata tiba yake na kujiondokea bila sijui mambo ya ramli au oo Fulani kakuroga,sizani kama kuna tatizo lakini watu utasikia uyu nae mshirikina?

Mfano unaenda kwa mganga then kwenye kajioo kake kadogo anakuonyesha aliyekuibia mali zako.Iyo inatofauti gani na kamera za bank na maeneo mengine zina tofauti gani na za uyu mganga wa kienyeji au kwa sababu kuna tunguli na manyoya pembeni which is the same ata zile za mzungu kuna specification kama ni komputa utaambiwa iwe Pentium 4,mara RAM 512 AU CPU speed iwe not less than 1gb yale yale tuu.

Kuna waganga wanaweza kukupa dawa za kulind nyumba yako either kwa kutumia nyuki au watu wabaya wajapo wanakuta bahari.

Au unakuwa na shamba lako la mazao mwizi akijitokeza kubeba mazao aliyoiba ghafla nyoka anamzonga mpaka anatua,au akiuweka kichwani hautelemki mpaka mhusika aje.Tena mambo kama ayo yalikuwa yanatia discipline wizi wa kijingajinga hautokei.
Au kama wenzangu wa Sumbawanga umemtia mtu mimba alafu unaikataa wanailudisha kwa mwanaume mpaka usalimu amri.

Ukichunguza unakuta kwa mambo hayo jamii ikawa na adabu na heshima sio nowdays kubakana,mimba wizi wa kipumbavu pumbavu

Iyo ni mifano tuu ila yapo mengi tuu mazuri ila kuboresha baadhi ya mambo.

Naona kuna haja ya kuendeleza baadhi ya jadi zetu ingawa si zote
 
kuheshimu wakubwa,wazee,wagonjwa na wajawazito......wazazi kutorohusu watoto wao kukaa(sexy) kingono zaidi kwani kunachangia kuwaharibu kimaadili(MAVAZI,MISEMO,MAKUNDI,MIZIKI,NK).........wakubwa kubaki kuwa wazazi wa kila mtotoo na pindi watoto wanapokanywa wazazi husika wsije juu......kuenzi ngoma za asili yetu kwani hukumbusha asili ya jamii husika...........(
 
Tunakoelekea ndio tunazidi kuchanganyikiwa zaidi ..Tutokapo tunapajua lakini tuendapo hahahaha..
Kufanya matambiko ya kujinja mbuzi na kondoo ..kuomba miungu ya mababu zetu itusaidie ...:D

kaaz kweli kweli
 
kweli baba ......

hehhe nimeipenda ya kupewa walinzi wasionekana kwa macho ;)
 
Back
Top Bottom