Naona Kula Mgahawani ni nafuu kuliko kupika kwa mtu mmoja

Heri yako unayekula 3000, mimi lunch yangu inarange 7000 hadi 10000, diner the same, niwekee huo mchanganuo tuone kipi afadhali
 
MIMI NILISHAWAHI FANYA MAHESABU HAYO,NILIKUWA NA FRIDGE PIA,,,NIKAPIKA THE FIRST WEEK,NIKAONA GHARAMA ZINAONGEZEKA KWA MARA MBILI NA CHUMBA KINAKUWA KICHAFU( KUTOKUOSHA VYOMBO KWA WAKATI MPKA KESHO YAKE)...NIKAJIONGEZA NIKATAFUTA MAMA NTILIE ANAYEPIKA VIZURI NIKAMPATA,BASI CHUMBA CHANGU KIKAPONA,MIMI NI MTU WA KUSOMA VITABU NA KUFANYA PROJECT ZANGU JIONI KWAIO MUDA WANGU UKAWA UMEPONA....NATHAMINI AFYA YANGU LAKINI PIA MUDA NAUTHAMINI ....teh teh All hail to Mama nitilie's in the City.
 
Mke wangu kaenda kwao kujifungua,kabeba na watoto wakawaone ndugu zao upande wa mama yao,ni holiday season,napika kila siku na kazini naenda siyo kwamba nakwepa gharama la hasha kila nikila mghahawani huwa sipati radha ya chakula ninayoihitaji,najua kupika vizuri mama yangu alinifundisha since nikiwa darasa la tatu,lakini pia kusema gharama za kula gengeni zifanane na za kupika mwenyewe siyo kweli katika kupika mwenyewe huwezi kutumia elfu 60 kila siku Mimi nanunua nyanya na vitunguu vya wiki nzima kwa TSH 5000/=(nyanya 3500 na vitunguu vya 1500)
Mafuta lita tano utasahau kabisa,mchele kg 50,utasahau kabisa,gesi na gunia la mkaa utasahau kabisa hivyo vyote vitagharimu kama (130,000/=)kwa maisha nilipo.Ukiwa na hivyo vyote unaweza ukapitia mbogamboga za majani za mia tano ukala mlo wako safi kabisa.Naomba tu niishie hapo.
elfu 60 kwa siku unalisha hekalu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,
Moja ya changamoto kubwa ninayokumbana nayo ni suala la kupika.

Baada ya Kula Mgahawani kwa muda mrefu, nikaona nianze mchakato wa kupika. Lakini nimegundua kuwa, Kupika chakula cha mtu mmoja ni Gharama kubwa kuliko kula mghahawani.

Mimi bajeti ya chakula cha mchana ni 3000 na jion hivyohivyo, hivyo jumla kuwa 6000 kwa siku.

Lkn nilipo anza kupika nikaona gharama ni zilezile mchanganuo ni kama ifuatavyo,

1. Mchele nusu 1000
2. Mboga za majani 500
3. Mafuta 500
4. Nyanya na vitunguu, hoho 1000
5. Nyama robo 1500
6. Nishati 500

Jumla inakua 5000

Najua wengine watasema vitu unanunua kwa jumla, lkn nimefanya hivyo na ukichukua hesabu zake ni kama hivyo tu.

Sasa hapo hujaweka usumbufu wa kupika, kuosha viombo, kumwagamwaga maji, na muda pia.
Pili kupika kunahitaji ufuatiliaji, mana nishaunguza sana tu.

Je nyie ambao ni mabachela mnaweza save vipi gharama kwa kupika na kuepuka kula mghahawani?

Labda mnaweza nishawishi tena nirudi jikoni mana nilipika wiki mbili nikaacha mpk vitu vikakaribia kuharibika ikabidi nivigawe tu.

kupika ni kazi sana usumbuf mkubwa niuonao ni ukijuwa naenda kupika lazima uwahi kufika nyumbani, mambo ni mengi kwenye kupika utayarishe mchele kama ni kudondoa chua siju vyombo kijiko kiko wapi, chumvi, umenye vitunguu, nyanya wakati haya yako jikoni lazima usimamie then mimi nilichogundua chakula nilichopika mimi sikioni kitamu mpaka kipikwe na mtu mwengine.

nikiwaza hayo tu nagairisha kupika naenda kununua zege la chipsi mayai na juic kaz kwisha.
 
Heri yako unayekula 3000, mimi lunch yangu inarange 7000 hadi 10000, diner the same, niwekee huo mchanganuo tuone kipi afadhali
Mkuu,
Nilikuwa na matumizi makubwa sana, kwa siku nilikuwa napindua 20k kwenye misos tu, hujaweka mafuta..
Nikaona hii balaa, nikaamua kujiunga na Saccos moja ya serikali, ili wawe wananikata kiasi fulan kila mwezi,

Kiukweli baada ya kuweka limit, nikaweza kujishape kwa 12k kwa siku na ninampango wa kufika 10k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ubwege ww hivi nyanya za hiyo bei unapikia kw siku moja huo ni ufala na sifa za kijinga, hivi kweli hoho za bei hiyo tajwa unapika kwa siku moja labda kama akili yako ni ya pumbavu acha ujinga bana ww huna unalojua acha ufala
 
Mkuu,
Nilikuwa na matumizi makubwa sana, kwa siku nilikuwa napindua 20k kwenye misos tu, hujaweka mafuta..
Nikaona hii balaa, nikaamua kujiunga na Saccos moja ya serikali, ili wawe wananikata kiasi fulan kila mwezi,

Kiukweli baada ya kuweka limit, nikaweza kujishape kwa 12k kwa siku na ninampango wa kufika 10k.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hyo saccoss wanapika chakula?
 
Kibachela buku tu inatosha.

Hua nazungusha kiugali changu unga robo 200. Napika kwa kerosine stove (jiko la mchina). Mafuta koroboi 2 150 jumla 300. Yanatosha kuivisha ugali.

Mboga: Nachukua na dagaa mchele wa kulumagia. Japo fungu ni buku niliingia MoU na Mama Chuki awe ananiuzia nusu fungu yaani 500 na kila siku nanunua kwake tu

Sipakui ugali nakula kwenye sufuria tu na dagaa nakula kwenye gazeti lake. Kwahyo kazi yangu ni kuosha sufuria na mwiko tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kibachela buku tu inatosha.

Hua nazungusha kiugali changu unga robo 200. Napika kwa kerosine stove (jiko la mchina). Mafuta koroboi 2 150 jumla 300. Yanatosha kuivisha ugali.

Mboga: Nachukua na dagaa mchele wa kulumagia. Japo fungu ni buku niliingia MoU na Mama Chuki awe ananiuzia nusu fungu yaani 500 na kila siku nanunua kwake tu

Sipakui ugali nakula kwenye sufuria tu na dagaa nakula kwenye gazeti lake. Kwahyo kazi yangu ni kuosha sufuria na mwiko tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha kwa hiyo ww kila siku unakula nguna na dagaa mchele tu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bachela nataka kuwa bachela sababu maisha ya kisela sometimes yananipa raha

Mkuu
Watu tunatumiaga hiyo 1000 kwa siku na tunadunda mtaani

Nunua mkate au maskonzi weka ndani kazi ni kuhakikisha chupa inachai muda wote
Maisha yanaenda mungu siku moja atafanya maisha yawe mepesi usijali mkuu
Acha kuendekeza umasikin, mwili haujengwi kwa matofali utazeeka siku siyo zako ipende afya yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom