MeruA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2017
- 1,391
- 2,125
Mke wangu kaenda kwao kujifungua,kabeba na watoto wakawaone ndugu zao upande wa mama yao,ni holiday season,napika kila siku na kazini naenda siyo kwamba nakwepa gharama la hasha kila nikila mghahawani huwa sipati radha ya chakula ninayoihitaji,najua kupika vizuri mama yangu alinifundisha since nikiwa darasa la tatu,lakini pia kusema gharama za kula gengeni zifanane na za kupika mwenyewe siyo kweli katika kupika mwenyewe huwezi kutumia elfu 60 kila siku Mimi nanunua nyanya na vitunguu vya wiki nzima kwa TSH 5000/=(nyanya 3500 na vitunguu vya 1500)
Mafuta lita tano utasahau kabisa,mchele kg 50,utasahau kabisa,gesi na gunia la mkaa utasahau kabisa hivyo vyote vitagharimu kama (130,000/=)kwa maisha nilipo.Ukiwa na hivyo vyote unaweza ukapitia mbogamboga za majani za mia tano ukala mlo wako safi kabisa.Naomba tu niishie hapo.