Naona Kula Mgahawani ni nafuu kuliko kupika kwa mtu mmoja

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,302
23,020
Wakuu,
Moja ya changamoto kubwa ninayokumbana nayo ni suala la kupika.

Baada ya Kula Mgahawani kwa muda mrefu, nikaona nianze mchakato wa kupika. Lakini nimegundua kuwa, Kupika chakula cha mtu mmoja ni Gharama kubwa kuliko kula mghahawani.

Mimi bajeti ya chakula cha mchana ni 3000 na jion hivyohivyo, hivyo jumla kuwa 6000 kwa siku.

Lkn nilipo anza kupika nikaona gharama ni zilezile mchanganuo ni kama ifuatavyo,

1. Mchele nusu 1000
2. Mboga za majani 500
3. Mafuta 500
4. Nyanya na vitunguu, hoho 1000
5. Nyama robo 1500
6. Nishati 500

Jumla inakua 5000

Najua wengine watasema vitu unanunua kwa jumla, lkn nimefanya hivyo na ukichukua hesabu zake ni kama hivyo tu.

Sasa hapo hujaweka usumbufu wa kupika, kuosha viombo, kumwagamwaga maji, na muda pia.
Pili kupika kunahitaji ufuatiliaji, mana nishaunguza sana tu.

Je nyie ambao ni mabachela mnaweza save vipi gharama kwa kupika na kuepuka kula mghahawani?

Labda mnaweza nishawishi tena nirudi jikoni mana nilipika wiki mbili nikaacha mpk vitu vikakaribia kuharibika ikabidi nivigawe tu.
 
General Mangi, Bachela nataka kuwa bachela sababu maisha ya kisela sometimes yananipa raha

Mkuu
Watu tunatumiaga hiyo 1000 kwa siku na tunadunda mtaani

Nunua mkate au maskonzi weka ndani kazi ni kuhakikisha chupa inachai muda wote
Maisha yanaenda mungu siku moja atafanya maisha yawe mepesi usijali mkuu
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom