The black day
Member
- Oct 8, 2018
- 9
- 16
Miaka 30 ni umri wangu na nipi kwenye hii kazi ya ualimu kwa miaka 9 sasa.Lakini ndoto zangu zote nilizoziwaza za kimaendeleo hata robo hazijatimia zaidi ya kufanikiwa kuanzisha familia ambapo mpaka sasa nina mke na watoto wawili.
Ingawa kuna factors nyingi zinazonivuta nisifikie ndoto zangu mapema kama:-
1:Kuwa tegemeo pekee kwenye familia ya wazazi wangu ambapo tulizaliwa watoto 8 na mimi nikuwa wa 7/8 ingawa sasa tumebaki 6 kwani wengine walishaenda mbele ya haki na wenzangu wote ni wakulima tu wa kile kilimo kisichokuwa na tija na bado kuna mpwa niliyekuwa nikimsomesha aliyehitimu kidato cha 6 mwaka huu.
2:Mazingira duni ya kazi niliyopo ambayo si productive.
3:Mshahara duni.
Hatua nilizozichukua mara kadhaa kupunguza ukali wa maisha ni kukopa mkopo bank na kuanzisha kibiashara cha kioski ambapo mara kadhaa nilianguka na kuamka tena lakini mara ya mwisho nilikuja kuibiwa kila kitu nikabaki mweupe na deni la bank bado bichi kabisa.
Kilichopo sasa my take home salary ni 191,000.
Kutokana na hiki kipato changu cha sasa,ugumu wa kazi ulivyo na mazingira yake,utitiri wa majukumu na madeni naona kabisa itanichukua zaidi ya hata miaka 10 walau kufikia japo nusu ya ndoto zangu.
Ijapo lengo langu tangu mwanzo ilikuwa ualimu utakuwa daraja tu lakini kumbe nimetumbukia.
Zaidi ya ualimu:
1.Ni MC ila mazingira yananifelisha maana nipo kijijini sana na ndoto yangu ni kuwa iwe kazi yangu rasmi.
2.Nimeandika kitabu cha kiingereza ambacho naamini kitakuwa ni muarobaini wa tatizo la ufundishaji wa lugha hii kwa walimu wa shule za msingi na ujifunzaji wa wanafunzi wanaojiandaa na mtihani wa drs la 7 maana kipo full nondo ingawa ndo nimemaliza tu kukiandila,nilifikia hatua ya kuwaza wazo hili pengine kwa uzoefu na ujuzi nilionao katika somo hili ninaweza fanya kitu cha kuniingizia kipato.
3:Ni mtunzi mzuri wa mashairi na nyimbo za kisasa na hata kuimba ingawa sijawa na ujasiri wa kuamua kurekodi nyimbo.
Shida iliyopo naiona kazi ni chungu na ninatamani kuiacha ili nifanye shughuli hizo ila tena nikifikiria kiacha wakati bado sina mtaji nina hofu pengine halu ya maisha inaweza kuwa mbaya zaidi ya hapa maana hata kipato ninachokipata kwa sasa naishia kulipa madeni ya watu binafsi.
Anyway,najua wapo watakaonikejeli lakini kumbuka hili ni tatizo kwangu na ninahitaji msaada wa kipi nifanye au nijilipue wapu ili walau nami siku nufurahie haya maisha.