Naona fahari kuwa Mtanzania na Daima na popote nitajifaharisha kuwa ni Mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naona fahari kuwa Mtanzania na Daima na popote nitajifaharisha kuwa ni Mtanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtu wa Pwani, Oct 18, 2010.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwa kweli fahari yangu kuu ndani ya moyo wangu ni Tanzania na kamwe si kuiona Zanzibar iliogawika kati ya Zanzibar na Tanganyika

  najisikia fahari nisemapo nchi yangu Tanzania ambayo ina visiwa vizuri vya kuvutia vya Zanzibar na kujisifia Mlima kilimanjaro na mbuga na maziwa mbali mbali yalipo tanganyika


  najionea fahari iliojaa kwenye moyo wangu nikiuangalia utajiri wa nchi yangu tanzania kwa mali asili ziliopo bara na pwani(zanzibar)


  kazi ilio mbele yetu ni watanzania kujua utajiri tulionao na kutumia akili zetu kuifanya Tanzania yenye neema inawaneemesha watanzania wote

  ni jukumu letu kuifanya Zanzibar zaidi ya Hongkong au singapore for sake of all

  ni jukumu letu kuifanya Tanganyika kuwa zaidi ya German au england

  nguvu ya nchi hizi zikiunganishwa na watu wake kuangalia zaidi opportunities tulizo nazo badala ya kukaa na kuota utengano tutakua mbali

  wakati umefika kwa kila mtanzania kujituma zaidi na zaidi na kuhimizana kua tanzania kwanza na kujenga Tanzania yenye matumaini


  tanzania ndipo kwetu

  hakuna pengine katu

  asitudanganye mtu

  naipenda tanzania ndani ya moyo wangu
   
Loading...