Naona dalili zote za Zitto kurudishiwa nafasi zake zote za uongonzi ndani ya CHADEMA

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,949
4,633
Wakuu kunakila hali ya mh.zitto kurudishiwa nafasi zake zote za uongozi kwenye chama chake hii inatokana na ziara anazofanya dr slaa mikoani na kukutana na upinzani mkali ambao hakuutegemea wazee wa chama cha chadema wameagiza maridhiano yafanyike zitto aruhusiwe kugombea uenyekiti na kurudishiwa nafasi zake zote za uongozi.

Hii inakwenda sambamba na wenzake wote waliofukuzwa na wao watarejeshewe nafasi zao na kuombwa radhi kwa kuzushiwa uongo, chadema wamegundua kuwa endapo zitto atafukuzwa anaweza kukiua chama mapema kabisa ndipo walipoamua bora arudishiwe nafasi zake zote na kuombwa radhi.

jukumu la kumaliza tatizo hili amepewa pf baregu na wenzake,ngoja tusubiri safari inaendelea.
 
Kumbe ameandika Gamba- SIMIYU YETU! Napitaaa. Makamanda hatumtaki ZZK magamba simmchukue?
 
Arudishwe ili asikiue mapema??!! Kumbe mnajua kazi ya Zitto dhidi ya CHADEMA na mmeanza kukili hadharani??!!

Zitto atafute tu wazandiki wenzie na waunde coalition Yao kwa fungu la CCM ili wafanye ajira yao kwa uhuru kwani ndani ya CHADEMA hatoheshimika,thaminika wala aminiwa tena iwe na uma wa wananchi au viongozi wenzie na naamini hata CCM hawamuamini Zitto sana kwani wanajua udhaifu wake)rejea taarabu za mbaali za Pinda juzi bungeni) lakini kwa kuwa ndio reliable traitor ndani ya CHADEMA and potential then inabidi tu wamtumie huku mkifanya kila janja janja na fitini ili mmsaidie asifukuzwe!!
 
Kama mliweza kumsikiliza slaa akiwa kakonko aliongea kwa hofu kubwa na kudai kuwa zitto hajafukuzwa anaweza kurudishiwa nafasi zake za uongozi wakati huo huo vikao bikiendelea vya kutaka arudishwe kwenye uongozi huku chadema wenyewe wanakili kuwa bila zito chadema kitayumba.
 
Kumbe ameandika Gamba- SIMIYU YETU! Napitaaa. Makamanda hatumtaki ZZK magamba simmchukue?
Baada ya siku 14 kuisha utayakumbuka maneno yangu na utanikumbuka kama humtaki zitto jiandae kuhama chadema anarudi na nguvu mpya zitto hafukuziki ndani ya chadema.
 
Hakika nguvu ya Zitto imedhihiri ndani ya CHADEMA
Viongozi wote wa chadema wanamgwaya zitto baada ya kupata tarifa za kuanza mazungumzo ya zitto kurudishiwa nafasi zake sasa Lisu anaumwa kwa hofu make walimbeza kwa kejeli wanawaza akirudi itakuwaje?
 
Unasema wenzake wapi? Na yule Dr.aliyeandika kuwa alishajiuzulu tangu mwaka 2010 ?
Kwamba kina Juliana Shonza, Mwampamba, Nyakarungu, Chagulain, Madiwani watano wa Arusha, Ali Chitanda, Mwigamba, Kisandu, Kafulila, Danda Juju, Thomas Nyimbo, Johna Shibuda, Eddo Makata, Said Arfi, Habib Mchange, Henry Matata, na Chagulani Adams wote waombwe radhi? .....Naamini mtoa hoja ana akili timamu
 
Zitto ni zaidi ya Chadema hilo lipo wazi wala halina mushkel.
 
Baada ya siku 14 kuisha utayakumbuka maneno yangu na utanikumbuka kama humtaki zitto jiandae kuhama chadema anarudi na nguvu mpya zitto hafukuziki ndani ya chadema.
Ha ha ha ha mwaka huu mtapata uchizi.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom