domokaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2010
- 3,545
- 1,719
Kwetu Tabora, Mkoa Mkubwa pengine kuliko wote nchi hii ndiko kunakoweza kuwa na watu waliolala kuliko mkoa wowote Tanzania.
Mkoa uliokuwa na shule muhimu kabisa katika nchi hii lakini mkoa uliotoa wasomi wachache ukilinganisha na idadi ya watu wake. Mkoa wenye asali na misitu asili, wenye tumbaku na mbegu ya ku ya iana ya kipekee duniani, mkoa wenye ng'ombe na mali asili nyingi, mkoa wenye watu warefu waliojaza misuli wake kwa waume lakini sina hakika sana na uwezo wa ubongo wetu.
Tabora isiyokuwa na barabara ya kutufikisha makao makuu ya mkoa kutoka popote pale duniani, mkoa wenye uwanja wa ndege wa matope. mkoa wenye mji wenye mtaa mmoja, mkoa ambao majumba yake yanazidi kwisha na kumongonyoka badala ya kushamiri. Mkoa ambao watu wake wanaogopa kujenga na hat akurudi kwao kwa kuogopa kulogwa.
Mkoa wa Tabora wenye wabunge wasiofanya lolote lakini wanoheshimiwa na kuabudiwa. Mbunge mmoja maarufu sana ana aliwahi kuwa na cheo kikubwa labda kidogo afadhali yeye maana akiendakwao huwanunulia wananchi wake maji madogo ya kilimanjaro, angalau wenye bahati hunywa maji ya kilimanjaro angalau mara moja kwa mwaka.
Hebua angalia wabunge wa bunge lilopita walifanya nini. Hebu Munagalie mnyamwezi yule aliyekuwa Igunga kabla hajajing'atua? Muangalia yule aliyekuwa bosi wa Bunge wamaifanyia nini tabora? Leo wanyamwezi eti wamemchagua mnyamwezi mwenzao muonesha bastola na almanusura nzega nao wamchague mnyamwezi mwezao yule mtoto wa kisomali lakini wakaishia kumchagua mnyamwezi mwenzao mrundi andrea.
Wanyamwezi bado hatujui mkoa wetu unaelekea wapi, hatuna elimu hatuna chochote. Mimi huwa najiuliza hao wanaosema wanyakyusa na wahaya walipata vyeo eti kwa kuwa mikoani kwao kulikuwa na shule kila siku huwa najiuliza kulikuwa na shule ngapi kushinda mkoa wa Tabora? Kagera nimefika na kuishi, Mbeya nimefika na kuishi lakini kila nikiangaza kulinganisha na Tabora sioni.
Inawezekana kumbe siyo uwepo wa shule ndio unaofanya watu waelimike kumbe hata uwezo wa ubongo. Sasa sishangai kuwa kila nikijaribu kufanya jambo sifanikiwi, inawezekana wanyamwezi tuna matatizo ya kurithi katika vichwa vyetu.
Hebu fikiri miaka hamsini kila siku mtu anakuahidi kukujengea lambo la maji na wewe unamkubalia tu eee, eti iko siku atalijenga!