Naona 99.9% Yanga anashinda dhidi ya Morrison

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,576
18,894
Kwanza kabisa mimi ni mshabiki wa Simba nakiri hili lakini hapa sitachambua kama mshabiki wa Simba bali Kama mshabiki wa Soka.Kwa Hili sakata linaloendelea naona kabisa BM hatachomoka kwenye Hili sakata ukiangalia kwa makini utaona hili.

BM Amejitia kitanzi mwenyewe

Wakati BM alikuwa akihojiwa kwa njia ya simu na Wasafi FM kupitia kipindi Cha sports Arena hapo ikiwa hajaingia mgogoro na Yanga alikiri kabisa amesaini mkataba na Yanga na akasema kabla ya kusaini Yanga alikuwa anatakiwa na team 3 za South Africa ikiwemo team ya Ajax Capetown. Huu Ni mkataba ule wa miezi 6 baada ya Yanga kuridhika na huduma Yake wakataka kumuongezea mkataba ndipo BM akasaini kwa miaka miwili baada ya kusaini BM akaongezea akasema baada ya yeye kusaini akawa anapewa maneno kwamba team ya Yanga hailipi mishahara wachezaji wake kwa wakati,haiendeshwi kiprofessionalism ndipo akaona Bora awaombe kuvunja mkataba nao huku Kuna baadhi ya offer akawa amepokea ikiwemo ya Simba.

Ukiachana na hapo tukaona email ya BM mtandaoni akiomba Yanga kucancel extension ya mkataba.kwenye Hili unajiuliza Kama ajasaini mkataba na Yanga inakuaje kwenye email yake anaomba acancel extension ya mkataba wake?

So ukitazama kwa ujumla wake bila ushabiki unaona kabisa jamaa anajifunga mwenyewe kwa Hali kama hii unaanzaje kumuamini BM?

Kwa upande wa Simba
Uongozi wangu wa Simba ulifanya kosa kubwa Sana kumtambulisha kumsajili Morrison mapema wangesubiri kwanza kesi ya Yanga na BM iishe Kama walivyoshauriwa na "Senzo" lakini kwa akili ya uswahili wa viongozi wakaenda against. Kwa maana hii Kama Yanga itashinda lazima watafungua kesi dhidi ya Simba kumsajili mchezaji wao mwenye "mkataba".
 
Kwa kifupi tu ni kwamba Morrison alijichanganya na tamaa za mikataba ya hapa na pale,ata yule Eng Ers aliwahi kusema pale Wasafi kwamba BM alimfuata akamwambia kwamba amepata tm yenye mkataba mnono hivyo anaomba avunje mkataba na hapo ndipo ugumu ulipo kuja akaanza mgomo wa kutosafiri na tm to Shinyanga kucheza na Mwadui, so hapa BM anajaribu kuukana mkataba wake wa halali na Yanga, sidhan kama this time atabakia salama,maana ata huko alikotoka ilikuwa n vurugu tu, Pale Orlando Pirates, Mara As Vita.

kote huko aliacha Gumzo na inavyoonekana akifika sehem anaanza vurugu ili mkataba uvunjwe ili awe free agent na apige pesa,BM anatumia ujanja wa watu wa A.Magharibi kupiga pesa.
 
hivi inawezekana kucheza mechi za ligi bila mkataba????
Hapana mkuu,na hata hivyo BM alionywa na Tff kwamba hakuna mchezaji anayecheza ligi ya Tanzania pasipo na mkataba na leseni ya kaz kwa foreigner-hili karipio la Tff kwa Morrison ilikuja mara baada ya BM kusema kwamba alichezeshwa bila mkataba na Yanga pale tu alipoingia Nchini na Tff iliudhibitishia adhira kwamba huyu jamaa n mchezaji halali wa Yanga,hapa ninachokiona mimi Tff inataka kubalance mzani, maana Simba inaweza kujikuta kwenye matatzo kwasababu ya kumsahinisha mchezaji ambaye ana mkataba na timu nyingine.
 
Hapana mkuu,na hata hivyo BM alionywa na Tff kwamba hakuna mchezaji anayecheza ligi ya Tanzania pasipo na mkataba na leseni ya kaz kwa foreigner-hili karipio la Tff kwa Morrison ilikuja mara baada ya BM kusema kwamba alichezeshwa bila mkataba na Yanga pale tu alipoingia Nchini na Tff iliudhibitishia adhira kwamba huyu jamaa n mchezaji halali wa Yanga,hapa ninachokiona mimi Tff inataka kubalance mzani,maana Simba inaweza kujikuta kwenye matatzo kwasababu ya kumsahinisha mchezaji ambaye ana mkataba na timu nyingine.
Mkuu mbona unajichanganya?
 
Mimi Morrison nasema Email account yangu ilidukuliwa hivyo sikuwahi kuomba ku cancel contract. Vile Vile sijawahi kuwa na Oral contract na yanga kwa hiyo nilichosema kwenye redio sio mkataba. Onesheni wapi nilisaini na lini ..haya kwako mtoa maada.
 
Hili swala bado ni gumu kwa Yanga hata kama wakishinda hii kesi, mchezaji hata awe na mkataba na timu kama hataki kuchezea hiyo timu watalazimika kuuvunja mkataba au kumuuza kwa hasara kwasabab mchezaj kama hana utayari wa kuchezea timu yako ataleta viroja vya kila aina hata kutohudhuria mazoezi, tulishaona hata kwa Angel Di Maria alichofanya pale Man utd, kwaiyo katika hili Yanga still ni losers kwa vyovyote.
 
Atapigwa faini na klabu ambayo itamfanya hata anaemnunua apate ugumu, mie ni simba ila naona kama uyu Morison kuna uhuni mahali nae kachangia
 
Hili swala bado ni gumu kwa Yanga hata kama wakishinda hii kesi, mchezaji hata awe na mkataba na timu kama hataki kuchezea hiyo timu watalazimika kuuvunja mkataba au kumuuza kwa hasara kwasabab mchezaj kama hana utayari wa kuchezea timu yako ataleta viroja vya kila aina hata kutohudhuria mazoezi, tulishaona hata kwa Angel Di Maria alichofanya pale Man utd, kwaiyo katika hili Yanga still ni losers kwa vyovyote.
Yanga Hana Cha kupoteza Mkuu, Anachotaka Yanga ni kuwaaminisha UMMA kuwa yule ni mchezaji wake halali then ndio watajua wapambane nae vipi anaweza pigwa benchi Hadi akili ikamkàa sawa au akauzwa sehemu nyingine kwà Pesa nzuri tu!
 
Hivi nikisema Nimekufa nakuwa nimekufa kweli na wewe utaamini nimekufa kwa vile nimesema nimekufa?

Mambo ya kisheria lazima yaangaliwe
 
Hili swala bado ni gumu kwa Yanga hata kama wakishinda hii kesi, mchezaji hata awe na mkataba na timu kama hataki kuchezea hiyo timu watalazimika kuuvunja mkataba au kumuuza kwa hasara kwasabab mchezaj kama hana utayari wa kuchezea timu yako ataleta viroja vya kila aina hata kutohudhuria mazoezi, tulishaona hata kwa Angel Di Maria alichofanya pale Man utd, kwaiyo katika hili Yanga still ni losers kwa vyovyote.
Refer conflict ya kakolanya vs Zahera au Adebayor Vs Tottenham spurs. Ukiwa na mkataba na ukaleta jeuri unaweza pigwa bench had mkataba wako utapoisha cha muhim ni team tu ikupe benefits zako
 
Back
Top Bottom