Naombwa ndoa kwa nguvu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombwa ndoa kwa nguvu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mhafidhina, Apr 6, 2009.

 1. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wanajamii,

  naombeni mawazo yenu kidogo...!

  Nina demu tumefahamiana kama miezi mitatu hivi na huwa hatuonani mara kwa mara. Na kweli bado hatujafahamiana vizuri kabisa, ikiwa ni pamoja na kwamba bado hata "hatujaonja tunda" hata siku moja.

  Hivi siku za karibuni ameanza kuniletea habari kwamba anataka kuolewa na kweli ameshikilia msimamo sana kwani kila ninapokutana nae habari ndio hio, anasema anataka kuolewa, anataka kuolewa.

  Sasa mimi nashindwa kuelewa je? kuna usalama hapa au vipi? Kuna siku nilijaribu kumuuliza past story yake akaniambia asingependa kuizungumzia, laini pia simfahamu kwa undani kabisa na kila nikijaribu kumuuliza huwa ananijibu juu juu halafu mada inarudi pale pale, anataka kuolewa eti kwa sababu umri wake umeenda sana sasa manake kashatia kibindoni miaka 30 anaelekea mwaka wa 31 sasa.

  Pia mimi binafsi ninawasiwasi na kabila analotoka manake ni kuleee kwa "akina Ishomire"

  Wajemeni kuna usalama kweli
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kwa lugha ya siku hizi wanaita 'kuondoa nukhsi!' :) usijilazimishe 'kumsaidia' kilicho nje ya matakwa yako, usijeongeza takwimu ya 'waliotalikiana' baada ya miezi michache.
   
 3. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mkuu ni kweli kabisa mwanamke akishafikia hiyo miaka huwa analazimisha sana kuolewa...ila nakushauri usiwe na haraka sana ya kutaka kumuoa hata kama umempenda vipi..Mpe time kwanza na mjue kwanza yupo vipi...Maana yeye kwanza ilikuwaje akakaa hiyo miaka yote mpaka leo hajaolewa??Au ndio kaachika alafu anataka kukupa pressure??Mkuu fikiria kwanza usichukue uwamuzi wa haraka!!
   
 4. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Demu mjanja amestukia unataka kumpiga uanze, hiyo janja yake kama kweli hauko serious utaingia mitini mwenyewe. Cha muhimu inategemeana unataka nini kwenye life yako.
  Angalia signature yangu hapo chini- inaweza kukusaidia.
   
 5. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180

  Mkuuu huyo demu sio mjanja kabisa ila naona kama anataka kuforce love kwa njia hiyo ya kuolewa ila sio kwamba etii anamapenzi ya dhati...Yeah kama anataka kuolewa anipe nakula alafu natambaa kimtindo unadhani hapo itakuwaje?
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  This is true story!

  Nilimdate mdada fulani kama miezi 3 hivi pia...baada ya kukutana naye huku ughaibuni. Sikuwahi fikiria aje kuwa mwenza wangu nilichukulia tunasaidiana kuondoa ukame. kadri zilivyokwenda alijiweka karibu sana na mimi...alianza kunambia bwana unampango gani na mimi...nilimjibu tunahitaji muda kujuana. Nilianza ulizia profile yake, ndipo nilipogundua aliisha haribu sana huko nyuma na hana sifa nzuri kwenye jamii...nilienda bongo na kuulizia habari zake zaidi...duuu kwa kweli ni balaa...niliporudi nilimwambia bwana lets part for sometime I need concetration na mambo yangu...alikuwa hanielewi, alifata marafiki zangu na hata ndugu zangu wanisaidie nimwelewe...niliweka msimamo na kubadili hata line ya simu...alikuwa analazimisha ahamie kwangu...of latest nikamwambia I am in a serious relation aniache. Akanitumia ujumbe kuwa anaolewa nikamwambia all the best nitakuchangia...bwana wee amenibadilikia eti nimempotezea muda, nikamwambia I never mentioned kuowa bwana...amekuwa adui yangu balaaa ananipakazia ile mbaya...nadhani atanitoa kule zeuchungu maana anapicha zangu....jamani kuolewa ni dili sana wadada?

  masa
   
 7. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Anataka kuolewa na wewe au mtu mwingine? Maana umesema kuwa hamjafahamiana vizuri
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...bahati yenu nyie wenye 'kuonja-onjaring' wanawake wanaong'ang'ania kuolewa hawawabambikii mimba. Miaka ile akishakwambia ana mimba yako utake usitake utapeleka posa, mahari na kupanga siku ya harusi siku hiyo hiyo, kabla katumbo hakajachomoza!
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  tiGoni hamna mimba bwana na mambo ya kinga ndo kabisa!....akisingizia hapo tutafika mbali!
   
 10. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Time to move on...
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ....Ooooppssss! kumbe ni mmoja'po katika wale :)
   
 12. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nilisahau kuwa hatuko sawa, maharamia kweli wanaweza kufanya hivyo. Hapo demu ana-lost kisawasawa!
   
 13. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Masanilo,
  kuolewa uliomwengu wa sasa wala sio dili. Zamani watu ndio waliona dili, lakini dunia ya sasa cha msingi ni elimu kwa mtoto wa kike au kwa mwanamke na kuwa na kazi yake. Mie naona kuolewa sio dili.
   
 14. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dada unacheza wewe. Kwa BongoTZ kuolewa bado big deal. Jamaa mmoja anasema "Mwanamke asipokuwa na mume ni kazi bure. Chumvi ni chumvi na sugar ni sugar"

  Mwanamke wa mawazo hayo anakuwa sana sana yuko kwenye hali moja kati ya hizi; 1) bado mdogo sana hajaanza mambo ya mahusiano na wanaume au 2) ameshindwa kupata mume au 3) ameachika ndoani.

  Pamoja na hela, pamoja na kisomo, marejeo ni kwa mume tu!
   
 15. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  a wapi! Kwa wale wadada walioelimika hata bongo is not a big deal. Ya nini umlazimishe mtu akuoe? kama anaona unafaa si ataanza yy kukutamkia kwamba "Do you marry me?
   
 16. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Big deal, ila mpaka kulazimisha ni 'too much'.
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Duh Pretty... ushaolewa weye?
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sasa na wewe naye; humjui past yake, kabila lake, umemuona three months, hujasema kama ushaua na kama ulii-enjoy

  Tosa hicho kicheche utajuta akiingia ndani, anavua hiyo ngozi ya kondoo halafu anavaa ya nguruwe... ni matopetope tu ndani

  BY THE WAY, KWANINI UPASHE MOTO KIPORO WAKATI KUNA TOTOS KALI KITAA?
   
 19. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #19
  Apr 6, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Jamani inawezekana yuko clean huyo dada ila tu anataka kuujua msimamo wako kwake kwa sababu huwa ni kawaida (si umesema ameshatimiza 30?) Unategemea nini?
   
 20. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #20
  Apr 6, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  . Masanilo Mzee wa t.
   
Loading...