Naombeni utaratibu wa kubadili jina la mtoto kwenye cheti cha kuzaliwa

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
685
484
Naomba mwenye kujua utaratibu huo anijuze mfano mtoto kwenye cheti ni Paul Kayuguyugu na Mimi ninataka aitwe Paulo Kayuguyugu.
 
Unahitaji kwenda kwa Registrar of Titles na vielelezo kamili vikiwemo cheti cha kuzaliwa mtoto; kitambulisho chako baba mtoto na cha mama mtoto; barua ya maelezo kwa nini mnataka kubadilisha jina; barua ya kiapo kwamba wazazi wote wawili mmekubaliana kubadilisha jina la mtoto; barua za wadhamini wawili ambao ni ndugu zenu wazazi waliomuona mtoto alipozaliwa na kwamba ndiye yeye hasa anayebadilishwa jina; na barua ya mjumbe wa unapokaa kuthibitisha kwamba anakufahamu na unayoyasema ni kweli. Utahitajiwa kulipia gharama kidogo za kiutawala.

Unaweza pia kupitia kwa mwanasheria. Hiyo ni rahisi zaidi kwani atashughulikia masuala mengi lakini atakutoza ushuru kwa kazi yake. Hata kama unamtumia mwanasheria, bado utahitaji hivyo vielelezo nilivyovitaja hapo juu. Utakachokuwa umepunguza ni ile bughudha tu ya kuambiwa hivi na vile kwa kuwa mwanasheria ndiye atashughulikia hayo.

Pamoja na kumtumia mwanasheria, siku ya mwisho utahitajiwa kufika wewe mwenyewe na mwanasheria wako kutia sahihi na kuchukua alama za vidole.
 
Ng'wanamalundi
Unaongea sana mlamu, cheti cha kuzaliwa cha nini wakati kinahitajika cheti kipya kwa jina jipya!!

Muhimu ni kujua mtoto ana umri gani, kama ni mdogo piga chini hicho tengeneza cheti kipya.

Huko shule anza kubadilisha kwenye madaftari, akifika darasa la mtihani kitaifa ni lazima mzazi utashirikishwa utoe jina sahihi mtoto asajiliwe.

Imeisha hiyoooo!
 
Ukienda ofisi husika unapata details zote sio kazi ngumu. Utakwenda mahakamani kwa kiapo then unarudi ofisini wanakubadilishia
 
Katafteni tu kipya wanatoa hzo process mnazotaka kufata mtajichosha bure na mtoto under five ni bure
 
m
Unahitaji kwenda kwa Registrar of Titles na vielelezo kamili vikiwemo cheti cha kuzaliwa mtoto; kitambulisho chako baba mtoto na cha mama mtoto; barua ya maelezo kwa nini mnataka kubadilisha jina; barua ya kiapo kwamba wazazi wote wawili mmekubaliana kubadilisha jina la mtoto; barua za wadhamini wawili ambao ni ndugu zenu wazazi waliomuona mtoto alipozaliwa na kwamba ndiye yeye hasa anayebadilishwa jina; na barua ya mjumbe wa unapokaa kuthibitisha kwamba anakufahamu na unayoyasema ni kweli. Utahitajiwa kulipia gharama kidogo za kiutawala.

Unaweza pia kupitia kwa mwanasheria. Hiyo ni rahisi zaidi kwani atashughulikia masuala mengi lakini atakutoza ushuru kwa kazi yake. Hata kama unamtumia mwanasheria, bado utahitaji hivyo vielelezo nilivyovitaja hapo juu. Utakachokuwa umepunguza ni ile bughudha tu ya kuambiwa hivi na vile kwa kuwa mwanasheria ndiye atashughulikia hayo.

Pamoja na kumtumia mwanasheria, siku ya mwisho utahitajiwa kufika wewe mwenyewe na mwanasheria wako kutia sahihi na kuchukua alama za vidole.
mwanasheria atamwandikia deed poll then ataenda wizara ya ardhi watamsajili shughuli inakua imeusha
 
Baba ya mtoto anataka aitwe Paulo badala ya Paul
Baba mtoto nae mshamba jamani, Paulo ndo jina gani sasa? Paul lipo vizuri.
Halafu si angeshughulikia yeye cheti cha kuzaliwa tangu mwanzo? Au aende yeye mwenyewe akabadili.
Mwambie asitusumbue.
 
Back
Top Bottom