Naombeni ushauru nadhifu katika hili

thA goD

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
1,941
1,844
Habarini wanajamvi,
Bila kupoteza wakti niende moja kwa moja kwenye mada husika.
Baada ya harakati za kuomba ufadhili wa ada kwa masomo ya diploma pale DIT kugonga Mwamba sasa nawaza kwenda kurudia mtihani wa advance kama plan B,
Masomo ni PCM,olevel nilikuwa na div-one point 17,adv niliambulia div-three point 15 yan EEE flat,je kwa wenye ufahamu wa hili nikitusua nikawapigia one advance nitapata mkopo kweli?
Na kituo gani bora kufanya masomo haya kwa Dar es salaam,nisome kwa mtindo gani nipasue mana nina uchu mnoo pia itanigharimu kiasi gani na muda gani kama resister?
Naombeni munishauri kwa dhati ya moyo mana naamini humu ndani nyote ni GTs.
 
Bila shaka Bios ulipata angalau C Kidato cha nne.
Nenda kachukue diploma ya clinical achana na mambo ya advance. Kama ulipata hiyo while ukiwa shuleni ni vigumu kupanda zaidi ukiwa home.
Kosa wanalolifanya wengi(I included) ni kukimbilia Form five na six.
Ushauri: Kijana wa form 4 kama unauhakika wa kupata angalau C tatu kwa masomo ya sayansi chaguo lako la kwanza kwenye fomu liwe chuo. Hii utamsaidia mzazi na wewe mwenyewe pia.
 
Unapoteza muda chukua cheti cha o level kapige course nyingine na kama unataka fani ya sayansi na kama bio umepiga bomba kachukue hata mambo ya clinical au phamasia kwenye vyuo vya serikali kuliko kupoteza muda na mambo ya kizamani heti advance level

Kumbuka maisha,nyakati na mambo hubadilika na pia umri unaenda ndugu hafu kusoma mpaka huko utakako sio sifa ndio maana now kuna foundation course za cheti na diplom hambazo zitakusaidia kukutengenezea njia kwenda ngazi nyingine hafu kumbuka msomi sio wewe kila mwaka kuna maelfu na makundi ya wasomi ambao graduated na undergraduate wanahitimu,pia kuna maelfu waliokuwepo mtaani kusaka ajira kwa fani zote ujuazo wewe

So unapofanya maamuzi jaribu kuangalia na hali ulivyo na uliyonayo pamoja na kuthamini pia kutathimi muda kabla hujageuka kuwa history

USHAURI WANGU NDIO HUO NA KAA NA NDUGU,RAFIKI AU JAMAA ZAKO AMBAO WASOMI WATKUELEZEA JINSI HALI ILIVYO

SHTUKA KIJANA

NB
KAMA FANI UNAIPENDA LAKINI IMEKUKATAA ACHANAYO NAYO NA KUPANGA NI KUCHAGUA ( plan to fail is failure to plan)
 
Nimekuelewa vyema sana mkuu,tatizo siwez gharamia hizo courses ndo mana hata nakimbilia kurisit.
 
Nimekuelewa vyema sana mkuu,tatizo siwez gharamia hizo courses ndo mana hata nakimbilia kurisit.
Kwan huko kurisiti utarisiti bure? Unahisi pesa utakayoitumi kwa kipindi chote cha maandalizi haiwezi kutosha kwa kulipa ada ya chuo?

Mm nilikua kama wewe ila hakuna kitu nilichojilaumu kama kwenda kusoma advance
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom