Naombeni ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni ushauri

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Godfrey Mwaja, Jan 3, 2011.

 1. G

  Godfrey Mwaja Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari ndugu zangu, mimi nina Girlfriend wangu tumekuwa pamoja kwa muda wa mwaka mmoja sasa. ki ukweli nimetokea kumpenda sana binti huyu hasa kutokana na uhusiano wetu na jinsi nilivomkuta akiwa hajawahi kufanya mapenzi na mwanaume yeyote, tofauti yetu ni dini yeye ni msabato nami mlutheri. mwanzoni mwa mapenzi yetu tulikubaliana wakati kufunga ndoa atabadili dhehebu na kufuata langu, baadae tena akasema hapana bora kila mtu abaki na dhehebu lake, mimi nikasema sawa, pili akakataa tusifanye mapenzi tena mpaka ndoa pia nikamkubalia, lakini kwa sasa hivi ananiambia kuwa imani yao hairuhusu kuishi na mtu wa dhehebu lingine pia hayuko tayari yeye kubadili dhehebu pia anasema kwao hawatamkubalia kubadili, kwa hiyo anataka mimi ndo nibadili dhehebu na kama itashindikana yupo tayari tuachane, wakati huohuo anadai kuwa ananipenda sana ndio maana ananiomba nibadili dhehebu, na mimi binafsi siwezi kubadili kuwa msabato, naombeeni ushauri.
   
 2. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  dah
  karne gan i?
  wote wakristu?dhehebu tu?
  HAMPENDANI.
   
 3. G

  Godfrey Mwaja Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nampenda sanaaaa, yaani tatizo imani na sheria za kisabato ndo zinanishinda.
   
 4. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mnapendana au mnadiniana?Ukishaona udini unachukua hatamu basi ujue hapo mapenzi hakuna
   
 5. LD

  LD JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mnapendana lakini Dini imeleta kasoro kwene Penzi lenu,
  Mbaya zaidi wote Wakristo ila madhehebu tofauti,

  Mpaka sasa bado hamjaweza kuweka mambo sawa ninyi wenyewe ktk hilo.

  Ushauri wa kwanza, Muombe Mungu akusaidie katika hilo, isije kuwa ni mtego wa Ibilisi ili msifike mwisho wa malengo yenu.
  Ukishaomba kwa kumaanisha, Ongea tena na huyo mpendwa wako, juu ya mtazamo wa Imani ya familia yako unayoitarajia.

  Halafu fanya maamuzi kutokana na majibu utakayopata kwake, na jinsi nafsi, roho, na moyo wako vinavyotamani.
   
 6. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Huyo anaBIP..... Mwambie abadilishe yeye......
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  true love exceeds everything and anything!
   
 8. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,807
  Likes Received: 1,975
  Trophy Points: 280
  unajua kwanini anakuzingua ni kwasababu hujamchakachua, jitahidi ushawishi akupe mwenyewe utaona

  lakini ndugu yangu wewe ndugu yangu unaambiwa kuna bikira wakati hujapata game, kama changa la macho je?
   
 9. T

  Tall JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.kumbuka utaishi na mke si dhehebu.
  2.wasabato na warutheri wote wanamtambua yesu kuwa ni masihi.
  3.ameanza taratibu kukuomba ubadili hiki,nawe unakubali,akisema wewe ni ndio darling.......hata ukimuoa atabadili mambo yako mengi.
  4.nawaelewa sana wasabato,pia nawaelewa sana walutheri...dhehebu lingine kumuoa msabato ni issue. Ukimuoa ukiwa mlutheri waweza kuwa unakunywa pombe na kubugia kiti moto vitu ambavyo ni fauolo kwa wasabato.
  5.hutampata huyo bila kubadili dini. Lakini usimlaumu si yeye ni waadventista wenzie ndio waliotilia mkazo uamuzi huo.
  6.kama unampenda......hutegemei kukutana na mtu kama yeye hapa duniani.......badili dhehebu.hutajuta.
  7.kama umri wako ni chini ya miaka 30,mtafute mzee asie msabato au mlutheri mweleze kwa kina tatizo lako.
   
 10. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Thats a joke, convert mkristo to mkristo, kweni kanisa gani haiwezi kufungisha ndoa?
   
 11. T

  Tall JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.usile nguruwe
  2.usinywe pombe au kuvuta sigara.
  3.usifanye kazi siku ya jumamosi.
  4.ubatizwe kwenye maji mengi.
  Kipi kigumu hapo mkuu?????????
  Sheria gani inakushinda?
   
 12. W

  Wakuchakachua JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tall u wapi mbona kimya mzee?????
   
 13. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mnh kama mtu umezoea kitimoto na pombe lazima haya masheria yakushinde,,,wengine hawali samaki wenye magamba sijui,majani ya chai napo ni ishu nilisikia......
  kama anafuata dini basi hata chupi asingekuvulia, huyo dada anapima msimamo wako ,ukionyesha kulegea hata ndani yeye ndio atakuwa mwenye maamuzi na sio wewe!...jifanye unampiga chini muone atafanya nini kama anakupenda atakubembeleza mrudiane kama hakupendi atauchuna tu,akiuchuna ujue haikuwa bahati yako...tafuta mwingine anayefit lifestyle yako!...akikubembeleza mwonyeshe msimamo wako kuwa unataka kumwoa ila mbaki dini tofauti......nawajua wasabato kibao wameolewa/wameoa madhehebu mengine.......sidhani kuwa na mtu wa dhehebu tofauti na lako itakupa tabu kuishi kikristu kama umedhamiria...
   
 14. M

  MABAGHEE JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwani mlipokutana mara ya kwanza ulimuuliza ni dini gani au ulimwambia tu anampenda?masharti ya ubaguzi wa dini si mazuri. Wewe ulimpenda kwa jinsi alivyo na si kwasababu ya imani yake. Halafu kubadili dini si suala la chapchap ni process. Niliwahi kuwekea masharti hayo nikakataa. Kama wasabato wenzake wangemwona si wangemwomba uchumba huko kanisani?akimaliza hilo atakuuliza kabila gani wewe etc. Dunia imebadilika sharti hilo halina nafasi. Watoto wa wachungaji wa SDA mbona wanaolewa na wasiowasabato?
   
 15. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  tatizo yeye hakupendi saaaana km unavyompenda,mapenzi ni two way trafic...pima kama unaweza ishi na mtu asiyekupenda kama unavyompenda???mengine changanya na zako!
   
 16. P

  Popompo JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mkuu kama unaona hutaweza kuishi bila yeye.badili dhehebu funga ndoa zalisha mtoto mmoja then rudi dhehebu lako!upo hapo!akili kumkichwa mkuu anakupenda sema anataka kukucontrol kwa remote!atakuwa mpole haswa!jaribu hutajuta!
   
 17. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Muombe Mungu,usitumie akili za kibinadamu kwenye hili.Take time,usiwe na haraka sana,pengine si wako Mungu kampangia msabato mwenzie na wewe kakupangia mtu mwingine au hata mimi...LOL.Chonde chonde usiende kuwa msabato then akishazaa urudi lutheran,unacheza na Mungu si mkeo na hii inaweza ku-gharimu ndoa baadaye.Mungu akutangulie,akupe busara na hekima kwenye hili.all the best!
   
 18. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,913
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Kama unampenda basi badili dini mukulu ili umuoe, Ila uwe makini huko mbeleni aije kuambia ubadili na vitu vingine eti utamaduni wao ndo unamtaka hivyo..... all the best
   
 19. H

  Hute JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,045
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  piga chini huyo msabato, kwanza ni msabato masalia tu. anajifanya ana dini wakati ameshatoa bikira kwako, sasa dini yake iko wapi? mnafiki huyo, hao ndo mafarisayo wanaojifanya kwa nje wazuri kumbe ndani ni makabuli yaliyojaa mifupa....wasabato watakusumbua sana, ata infect hadi watoto wako..mimi watoto wangu hata wewezi kwenda kusoma shule hata ya secondari au primary ya wasabato kwasababu wakiwa infected na sheria zao za agano la kale, wanakuwa kama wameuza akili kwa bei chee. achana nao...hao ni mafarisayo na masadukayo ambao hata sio wakristo..WASABATO SIO WAKRISTO, sio wanafunzi wa Yesu Kristo, ni wanafunzi wa Musa....so na wewe kama unataka umkane Kristo ili uwe mwanafunzi wa Musa..endelea kupoteza muda.

  Pili, wewe pia ni mnafiki sana, nyie walutheran pia ni wanafiki na ndio maana asilimia sabini ya wanaofunga ndoa za kilutheran wanakuwa na mimba kwenye shela la ndoa...okokeni, mnaenda kanisani kufanya nini sana, ulutheran ni ticket yako ya kwenda mbinguni?...mbona dini yenu ya kinafiki sana...mimi nilizaliwa huko lutheran kwenye familia ya kichungaji..wachungaji wazinzi ni asilimia hamsini...maaskofu wenu wachawi ajabu..fungukeni macho jamani.
   
 20. H

  Hute JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,045
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  upo tayari kuacha kitimoto? hawali kitimoto wala kambare hao...hahahaha.
   
Loading...